Hili la Machawa naliona kwamba lina hatari ya kukua na kuwa tatizo baadae. Linanikumbusha green brigade na red brigade! Chawa wa viongozi mbalimbali au wa vyama mbalimbali wanaweza wakakua mpaka wakaota mapembe. Wakianza kupigana huko mitaani kwa ajili wa Ma Boss wao, itakuwa shida. Tunajenga Makundi yanayopingana na kusigana kwenye jamii. Nadhani idea ya Machawa tuiache mapema.
Kuhusu kufufuka, halipo Hilo. Ila unaweza kusema hajatokea Kiongozi akatugawa Nchi hii kama Mwendazake. Mpaka Leo tumegawanyika. Hakuna legacy ambayo iko contested kama yake tangu tupate Uhuru. Legacy kubwa zaidi ni ya Baba Wa Taifa. Lakini haijaigawa Nchi hata kwa asilimia 5 ya mgawanyo uliosababishwa na awamu iliyopita. Wala hatutapata majibu kama Hawa waliopo wamepatia au la mpaka awamu hii iishe. Lakini kwa vyovyote vile, tunaonekana kuwa kwenye njia Bora na salama zaidi kuliko mwanzo.