Je, ilichukua muda gani kuanza kupata faida katika biashara yako?

Pwenti namba 2:
Mungu aweza yote.
Mungu atosha
 
Ahsante mkuu , naona hii biashara inatoka sana , hasa kwa hao wasio na mchanga na wale waliokaangwa
 
Duu kweli ulidhamiria kwenda kupikwa 😂😂😂😂
 


Hivi hizi issue za iman kumbe zpogo kweli!!!
 
Hakuna shida.

Kwanza inategemea upo eneo gani maana maeneno yanatofautiana,hapa namaanisha kuna maeneno kama mbagala,buguruni nk upatikanaji wa material sio ghali hivyo kuifanya biashara inakua unfauu kidogo.

1.Eneo nililopo mimi(hapa sitataja jina) vyakula vinavyopikwa wanauza elfu 1500 ila shida havina ubora hata kidogo.Mimi nikaamua kitu cha kwanza kuzingatia ni ubora wa chakula kwa bei ile ile.Kuna sehemu nafanya kazi wanauza ugali buku mzuri sana na faida wanapata sasa nikajiuliza kwanini kule buku jero na material rahisi kupatikana lakini chakula kibaya.

[emoji117]Wapishi wangu niliwaambia wapike chakula kizuri na kitamu(hapa sasa lazima uwe na mpishi mzuri maana kuna wengine kupika hawajaui)..niliwaambia waweke viungo vyote vinavyohitajika ili chakula kiwe na ladha nzuri,kitu ambacho wanafanya

[emoji117]Jambo la pili kwenye kila sahahni mimi naiongezea thamank kwa kuweka tunda(kipande cha ndizi au tikitikiti au tunda lolote huwa nabadilisha badilisha).

[emoji117]Hapa niliweza kufanya hivyo kwa sababu sinunui mahitaji reja reja nanunua jumla kuanzia mchele,unga na vitu vingine kisha nawauzia kwa kupima mfano wakitaka kupika wali labda kilo kumi watapima kilo kumi na baada ya biashara watatoa hela ya kilo 10.

[emoji117]Supu yangu nauza buku(nyama tatu) standard ila naweka na viazi hata kimoja au viwili pia na karoti kidogo(nina mpango wa kuongeza kipande cha mkate huko siku za usoni).

2.Usafi,hapa ni muhimu zaidi migahawa mingi usafi ni sifuri hawazingatii kabisa.Mimi niliwaambia nikienda nikakuta sehemu chafu basi watawajibika(hapa upate watu wasafi maana wengine hawana usafi hata ufanyaje ni wachafu).Sehemu yangu usafi ni wa hali ya juu kuanzia mazingira ,vyombo mpaka wahudumu(wawili tu).

3.Nidhamu,wanaongea na watu vizuri na pia nimewapiga marufuku kuhusu tabia ya umalaya(hapa nimewachukua watu ambao umri umesogea kidogo 25+ hivyo hawana utoto utoto..wanaongea na mteja vizuri na kwa nidhamu.

4.Muonekano wa sehmu yako hapa ndo kuna usafi,fenicha unazotumia na jengo..

Nimeandikwa kwa ufupi lazima ujiulize inawezekana vipi lakini jibu ni hili
[emoji117]Wakati naanza kufanya sikua na lengo la faida kwanza ,mimi niliangalia huduma kwanza ndo maana nilitaka kutoa kile ambacho nilikikosa nikenda kwenye mgahawa mingine.

[emoji117]Faida inakuja kadri unavyouza ukiuza sahani nyingi basi unapata pesa nyingi..kwa sasa wafanyakazi nimewaambia tunafanya kwa miezi mitano tuone trend ikoje na ninaboresha vitu kidogo kidogo na biashara inapokua nzuri zaidi basi na malipo yatapanda.

[emoji117]Faida ninayopata ukiondoka pesa zao na mahitaji mengine kwa siku inabik si chini ya elfu 10k+ kutegemea na siku, kitu ambacho kwangu nimeridhika na nina ona mafanikio hivyo nafanya jitihada kuongeza thamani.

[emoji117]Mpaka sasa nauza chakula tu,siuzi juice soda wala vitafunwa.Pesa hiyo inapatikana kwa kuuza wali,ugali na supu pekee.Nikianza kuuza vinywaji nk itapanda mara dufu maaana wateja wakija juice,soda na maji huwa nanunua kwingine(najichanga nipate friza kubwa).

Ukweli wakati naanza sikufikiri kama nitapata faida ila mimi binafsi napenda biashara,hivyo sikuwaza faida kwanza ila huduma.

Kwa machache hayo nadhani umeelewa.

Nb:ila inakupasa ufatilie mzee usikae kama muhindi kuagiza tu ,kwangu faida ya 10K+ sio ndogo hivyo nafatilia kama roho yangu na katika hao wafanya kazi jitahidi umtafute mtu anayeijua hiyo biashara manaa kwenye upimaji hapo ndo kuna bao.
Nipe mbinu rafiki na Mimi nataka kufanya hii biashara eneo x hapa DSM
 
Anyway nikitulia nitaongezea jambo apo kwenye namba 2 kuongeza ufahamu kidogo
"it is not what it is"
 
vipi mkuu ulofanikisha hilo dili?
Na jee kisa cha kutaka kufanya hvyo ili ikusaidie nini? Au cheo boss[emoji4][emoji4]
 
Sijawahi kutumia ushirikina kwenye biashara yangu mimi
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Vipi mkuu matokeo halikuwa chanya?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hili jibu lili-deserve likes nyingi na quotes za maana.

Ni jibu linaloweza hata kuwasaidia watu wengine kwny biashara zao hata kama sio za mambo ya misosi,maana ume-add value kwny karibu kila kitu unachokifanya kwny biashara.

More future success brother.
 
Biashara ni ngumu sana!

Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2020 nilianzisha biashara ya kuuza mafuta ya petrol visiwa vya mkoa wa Mwanza, biashara ambayo awali nilikuwa nikiifanya kipindi nasoma chuo!!

Kifupi muuzaji aliyekuwa akunisaidia kipindi hicho ndo yule yule niliamua kuendelea naye! Basi nikachukua mzigo kama drum kumi! Makadirio ilikuwa mzigo ujakae mwezi mmoja (1)

Nilikuja kupata changamoto hatari, mzogo ulikaa miezi 6 bila kuisha, nilijiuliza maswali mengi sana, nikimuuliza msaidizi wangu anadai hali ni mbaya sana, lakini palikuwa na mwenzangu aliyekuwa akifanya biashara ya aina hiyo yeye biashara zake zilikuwa zikienda sawa!

Nilitafakari sana nikaamua kuachana nayo maana nilijifunza kitu kimoja kwamba biashara ni "usimamizi mzuri" na huwezi kusimamia biashara yako inayoanza kama upo nayo mbali! Hivyo, ukiachilia mamnl mengine kama ndo unaanza biashara hakikasha unakuwa karibu nayo sana kwa zaidi ya 95%. Unaweza kumwachia mtu pale tu unapokuwa na uhakika tayari mizizi imeota na kushika vizuri!
 
[emoji120]
 
Amini Kwamba..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu feyzal ulianza na capital ya kiasi gani

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Miezi mitatu ya mwanzo,nilipoanza nilihisi kushidwa kabisa ikabidi ni amishe biashara hapo nimekula mtaji sehem,sina faida,nikahamia kwingine nikapanga vitu kwenye frem,mda huo sina pakulala naunga unga ili ifike asubuhi niingie mzigoni,kuna kipindi nilitaka kuacha kabisa ila nikakomaa,miaka mitatu sasa inafika sahiz ndo naanza kuona faida kwakipindi cha miezi mitatu tu nimetoa kiasi kukubwa tu cha pesa na sijaathili mtaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…