Hakuna shida.
Kwanza inategemea upo eneo gani maana maeneno yanatofautiana,hapa namaanisha kuna maeneno kama mbagala,buguruni nk upatikanaji wa material sio ghali hivyo kuifanya biashara inakua unfauu kidogo.
1.Eneo nililopo mimi(hapa sitataja jina) vyakula vinavyopikwa wanauza elfu 1500 ila shida havina ubora hata kidogo.Mimi nikaamua kitu cha kwanza kuzingatia ni ubora wa chakula kwa bei ile ile.Kuna sehemu nafanya kazi wanauza ugali buku mzuri sana na faida wanapata sasa nikajiuliza kwanini kule buku jero na material rahisi kupatikana lakini chakula kibaya.
[emoji117]Wapishi wangu niliwaambia wapike chakula kizuri na kitamu(hapa sasa lazima uwe na mpishi mzuri maana kuna wengine kupika hawajaui)..niliwaambia waweke viungo vyote vinavyohitajika ili chakula kiwe na ladha nzuri,kitu ambacho wanafanya
[emoji117]Jambo la pili kwenye kila sahahni mimi naiongezea thamank kwa kuweka tunda(kipande cha ndizi au tikitikiti au tunda lolote huwa nabadilisha badilisha).
[emoji117]Hapa niliweza kufanya hivyo kwa sababu sinunui mahitaji reja reja nanunua jumla kuanzia mchele,unga na vitu vingine kisha nawauzia kwa kupima mfano wakitaka kupika wali labda kilo kumi watapima kilo kumi na baada ya biashara watatoa hela ya kilo 10.
[emoji117]Supu yangu nauza buku(nyama tatu) standard ila naweka na viazi hata kimoja au viwili pia na karoti kidogo(nina mpango wa kuongeza kipande cha mkate huko siku za usoni).
2.Usafi,hapa ni muhimu zaidi migahawa mingi usafi ni sifuri hawazingatii kabisa.Mimi niliwaambia nikienda nikakuta sehemu chafu basi watawajibika(hapa upate watu wasafi maana wengine hawana usafi hata ufanyaje ni wachafu).Sehemu yangu usafi ni wa hali ya juu kuanzia mazingira ,vyombo mpaka wahudumu(wawili tu).
3.Nidhamu,wanaongea na watu vizuri na pia nimewapiga marufuku kuhusu tabia ya umalaya(hapa nimewachukua watu ambao umri umesogea kidogo 25+ hivyo hawana utoto utoto..wanaongea na mteja vizuri na kwa nidhamu.
4.Muonekano wa sehmu yako hapa ndo kuna usafi,fenicha unazotumia na jengo..
Nimeandikwa kwa ufupi lazima ujiulize inawezekana vipi lakini jibu ni hili
[emoji117]Wakati naanza kufanya sikua na lengo la faida kwanza ,mimi niliangalia huduma kwanza ndo maana nilitaka kutoa kile ambacho nilikikosa nikenda kwenye mgahawa mingine.
[emoji117]Faida inakuja kadri unavyouza ukiuza sahani nyingi basi unapata pesa nyingi..kwa sasa wafanyakazi nimewaambia tunafanya kwa miezi mitano tuone trend ikoje na ninaboresha vitu kidogo kidogo na biashara inapokua nzuri zaidi basi na malipo yatapanda.
[emoji117]Faida ninayopata ukiondoka pesa zao na mahitaji mengine kwa siku inabik si chini ya elfu 10k+ kutegemea na siku, kitu ambacho kwangu nimeridhika na nina ona mafanikio hivyo nafanya jitihada kuongeza thamani.
[emoji117]Mpaka sasa nauza chakula tu,siuzi juice soda wala vitafunwa.Pesa hiyo inapatikana kwa kuuza wali,ugali na supu pekee.Nikianza kuuza vinywaji nk itapanda mara dufu maaana wateja wakija juice,soda na maji huwa nanunua kwingine(najichanga nipate friza kubwa).
Ukweli wakati naanza sikufikiri kama nitapata faida ila mimi binafsi napenda biashara,hivyo sikuwaza faida kwanza ila huduma.
Kwa machache hayo nadhani umeelewa.
Nb:ila inakupasa ufatilie mzee usikae kama muhindi kuagiza tu ,kwangu faida ya 10K+ sio ndogo hivyo nafatilia kama roho yangu na katika hao wafanya kazi jitahidi umtafute mtu anayeijua hiyo biashara manaa kwenye upimaji hapo ndo kuna bao.
Nipe mbinu rafiki na Mimi nataka kufanya hii biashara eneo x hapa DSM