Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafurahi kuwaona watu km nyie ktk zama hizi[emoji120]Dini zimetumika kudumaza akili za mwaafrika. Mungu wa kiaafrika hakua na mpango huo.
Dini ni janga la Africa.
Swali fikirishi.Nimekuwa nikijiuliza hilo swali apo juu mara kadhaa kama tusingetawaliwa kuanzia waarabu mpka mkoloni mzungu inamaanisha hizi dini zisingekuepo.Je,hayo yalitokea kama mapenzi ya Mungu?
Maswali kama haya huwa hayana mantikikama tusingetawaliwa
Sahihi kabisa.Yako mengi sana ya kujifunza kwenye suala la dini
Kwanza kabisa dini zetu za kitamaduni zilikuwa na miiko yake, nzuri na mibaya.
Mfano mauaji ya twins, sadaka za binadamu nk. Lakini licha ya yote hayo dini hizi hazikuwa static, yaan hakuna Mungu mmoja, bali wengi wenye masharti totauti tofauti na ukihamia eneo fulani Basi utalazimika kuabudu Mungu wa huko.
Hivyo basi huu pia ulikuwa mwanya wa Hawa wakoloni kutumia Mungu wao kuturubuni.
Tunachoweza kufanya kwa sasa ni kuendelea kuamini kwa jinsi kila mmoja anavyoona inafaa kwake. Maana zaidi ya miaka 500 ya kutawaliwa unategemea dini zetu tutazikumbuka? Ngumu sana.
Kama kwenye kabila lako au ukoo wako bado mnaendeleza dini za kitamaduni Basi mzi tathmini muone Kama zinafaa. Ila leo Mimi kutoka Singida uniambie kuabudu mila za wachaga kweli siwezi kabisa. Hapa kwenye dini kila mmoja afuate msimamo wake.
Ushauri. Waafrika tuache kurogana na kuoneana wivu wa kijinga. Hii ni shida sana. Baadhi ya maeneo Kuna wachawi hatari na hawapendi maendeleo ya wengine. Tupendane waafrika