Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Mynd177

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
2,817
Reaction score
5,141
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
 
Ni sawa na kuuliza kama inawezekana kukaa katika nchi fulani bila kuwa na utambulisho ama uhusiano wowote nayo.

Unaelewa kwa nini Trump anawatimua wahamiaji haramu?

Kuwa muumini wa Mungu ni wajibu wenye kifurushi - huwezi kuutekeleza mwenyewe mwenyewe. Kama kila mtu angejikata kivyake, wewe ungemjuaje Mungu?

Faida ya kufanya ushirika na jamii ya waumini wengine: unakua kiroho, unasaidika kijamii, unawasaidia wengine kijamii na kukua kiroho, unahusika direct or indirectly kuitangaza injili ulimwenguni (Waebrania 10:23-25).
 
Hapo utakuwa unaabudu Miungu mingine ambayo ni dhambi.
Sasa Mungu wa kweli anapatikana dhehebu gani, maana nimetumia zaidi ya miaka 20 kwenye dhehebu ambalo nilidhani ndo dini ya kweli lakini baada kufanya utafiti nimevunjika moyo na mambo ya dini....

Kwa kweli kama Mungu atagawa uzima wa milele kwa kutazama mafungamano na hzi dini naona kabisa ntashndwa...
 
Ni sawa na kuuliza kama inawezekana kukaa katika nchi fulani bila kuwa na utambulisho ama uhusiano wowote nayo.

Unaelewa kwa nini Trump anawatimua wahamiaji haramu?

Kuwa muumini wa Mungu ni wajibu wenye kifurushi ambao hauwezi kutekeleza mwenyewe mwenyewe.
Aaaah nadhani ni bora kugeukia ATHEISM...

Maana kama Mungu anaruhusu watu waovu (kwa maoni yangu) wanaolawiti watoto, waroho wa madaraka, wazinzi, waongo, wasiojali kuongoza makanisa naona ntashndwa kua mwabudu...

yote kwa yote Hivi Mungu ni wa dini gani? naomba msaada..
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
Sende esupriy dewo ochi agalialec mioca
 
Dini ni matendo yako mkuu. Hata kama ni muudhuriaji mzuri wa ibada lakini matendo ni ya ajabu ajabu haileti maana yeyote hasa kipindi hiki ambacho madhehebu mengi yapo kwa ajili ya kupiga hela na show off. Fanya kazi kwa bidii Saidia wasiojiweza, fundisha wasiokuwa na elimu, lisha wasiokuwa na chakula na matendo mengine kama hayo kadri ya uwezo na moyo wako. Hii ni njia nzuri ya kuabudu kuliko kwenda kupakwa mafuta.
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
Ndiyo inavyo takiwa ukishakuwa ndani ya madhehebu tu haiwezekani kumu abudu Mungu bali unakuwa unamwabudu SHETANI MFANO WA MUNGU ....Madhehebu ni HEKALU LA SHETANI IBILISI.. ndiyo maana ya haya maandiko 👉CHUKIZO LA UHALIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU..

💥💥💥Hivyo swali lako lilitakiwa liwe hivi ..je INAWEZEKANA KUMUABUDU MUNGU UKIWA KWENYE MADHEHEBU ? ....jibu ni HAPANA💥💥💥
 
Kwanini unasema unaamini Mungu yupo?

Kwa ufahamu wako Mungu ni nani na alitoka wapi?

Usitumie vitabu vya dini kujibu kwasababu umesema vina udhaifu.
Jamaa hataki dini ila bado anatumia scriptures za dini kuelezea mungu.
Problem kubwa iliyoko kwenye dini na ambayo inaweza msingi wa confusion inayoletwa na dini ni "Personification of God"
 
Kwanini unasema unaamini Mungu yupo?

Kwa ufahamu wako Mungu ni nani na alitoka wapi?
Kwa kweli BIBLIA ninaitilia mashaka...

Nikitazama ufanisi(COMPLEXITY) uliopo duniani na ulimwenguni kwa ujumla inakuwa vigumu kufikia mkataa wa kuwa Mungu hayupo..
 
Aaaah nadhani ni bora kugeukia ATHEISM...

Maana kama Mungu anaruhusu watu waovu (kwa maoni yangu) wanaolawiti watoto, waroho wa madaraka, wazinzi, waongo, wasiojali kuongoza makanisa naona ntashndwa kua mwabudu...

yote kwa yote Hivi Mungu ni wa dini gani? naomba msaada..
Hapa ndio kiini cha hoja yako Masta, kwingine kote ulikua unazunguka mbuyu tu...

Amini katika Mungu wa Kweli na Wa Haki!!
 
yote kwa yote Hivi Mungu ni wa dini gani? naomba msaada..
Ee mwanadamu, Yeye amekuonesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! ~Mika 6:8

Adili, rehema na imani (Mathayo 23:23)

Self-control, faith, and compassion (James 1:26, 27).

1 Wakorintho 13:13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
 
Ndiyo inavyo takiwa ukishakuwa ndani ya madhehebu tu haiwezekani kumu abudu Mungu bali unakuwa unamwabudu SHETANI MFANO WA MUNGU ....Madhehebu ni HEKALU LA SHETANI IBILISI..
Hivyo swali lako lilitakiwa liwe hivi ..je INAWEZEKANA KUMUABUDU MUNGU UKIWA KWENYE MADHEHEBU ....jibu ni HAPANA.
Ahsante mkuu..
Dini niliyokuwemo kuna indocrination ya hatari, maana tumekuwa tukiambiwa kuwa ndo dini ya kweli, ukitoka basi ujue umemuacha Mungu na ujiandae kuharibiwa..nilikuwa humo kwa miaka 20, haya yameniathiri mpaka nimeacha kusali kibinafsi nahsi labda kwa kuwa nimeacha mambo ya dini basi hata Mungu atakuwa asikilizi...
 
Back
Top Bottom