Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Kwa kweli BIBLIA ninaitilia mashaka...

Nikitazama ufanisi(COMPLEXITY) uliopo duniani na ulimwenguni kwa ujumla inakuwa vigumu kufikia mkataa wa kuwa Mungu hayupo..
Biblia haina shaka yoyote wewe umepofushwa na biblia ya shetani iliyopo.kwenye madhehebu ya dini hiyo ni potovu..yenye kusema mungu anazo nafsi 3 😁
 
Ee mwanadamu, Yeye amekuonesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! ~Mika 6:8

Adili, rehema na imani (Mathayo 23:23)

Self-control, faith, and compassion (James 1:26, 27).

1 Wakorintho 13:13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Nadhani mkuu haya yote yanawezekana bila kuwa na mafungano na dini/dhehebu lolote..
 
Ahsante mkuu..
Dini niliyokuwemo kuna indocrination ya hatari, maana tumekuwa tukiambiwa kuwa ndo dini ya kweli, ukitoka basi ujue umemuacha Mungu na ujiandae kuharibiwa..nilikuwa humo kwa miaka 20, haya yameniathiri mpaka nimeacha kusali kibinafsi nahsi labda kwa kuwa nimeacha mambo ya dini basi hata Mungu atakuwa asikilizi...
CHUKIZO LA UHALIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU NI HAYO MADHEHEBU NA WAUSIKA WAKE
 
Hapa sijaelewa unaweza kutafsiri tafadhali...
Hiyo ni dini ya asili,Mimi ninajipanga kuachana na dhehebu langu na Hawa watu ibada ni dakika 59 tuu,hakuna sadaka hakuna Dhaka wao ni kumtui Mungu wa kweli hakuna mambo ya akazaliwa bila na nani na nani sijui,nimebakisha jumuia tuu huko kwa zamani nikimalizana nao nakuwa huru,hayo maneno tuu hapo juu ukiarudia kwa dakika tatu mfulizona ukasali PA1 kila kitu kinakutii hata madeni yanakuogopa magonjwa madigo yote yakukimbia.
"SENDE ESUPRIY DEWO OCHI AGALIYAREPTY MIOKA"
 
Inawezekana kwasababu dini ni kifurushi cha utamaduni na imani. Ila uhusiano kati ya mungu na mwanadamu ni imani.
Unaweza kutembea umevaa majuba, kanzu na hijabu na ukawa unaimani katika kristo yesu inawezekana. Yaani utamaduni wa kiislamu na imani ya kikristo. Hii ipo sana.

Mfano: wale waumini wa makanisa haya ya mitume na manabii wote wanaenda kanisani ila kuna maimuma, asha, mwajuma pia isaka na yakobo. Wanavaa suruali (mavazi ya kipagani) na wanamuabudu yesu na majina yao ni asha.

Kwahyo chakuhitimisha mungu haitaji dini yako, anahitaji imani yako ambapo imani n uhusiano wa wewe na yeye. Ndio sbb adam hakupewa dini ila alikuwa akiongea na mungu na mungu alikuwa akimtembelea saa za jion na wanae kain na abeli walikuwa na utamaduni wa kutoa sadaka za mazao na wanyama kwa mungu. Pia hawakuwa na dini walikuwa na utamaduni tu na imani
 
Biblia haina shaka yoyote wewe umepofushwa na biblia ya shetani iliyopo.kwenye madhehebu ya dini hiyo ni potovu..yenye kusema mungu anazo nafsi 3...
Mkuu dhehebu nililokuwepo hawafundisi utatu.... Siamini katika utatu binafsi yupo Mungu mkuu mweza wa yote ishu yangu ni kuachana dini,.

sema biblia za hii dini nimeziondoa kwangu maana zinanikumbusha niliyoyapitia kwenye hyo dini...
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
kila kitu Kina utaratibu wake , ata simu lazima uchague line moja
 
Inawezekana kwasababu dini ni kifurushi cha utamaduni na imani. Ila uhusiano kati ya mungu na mwanadamu ni imani.
Unaweza kutembea umevaa majuba, kanzu na hijabu na ukawa unaimani katika kristo yesu inawezekana. Yaani utamaduni wa kiislamu na imani ya kikristo. Hii ipo sana.

Mfano: wale waumini wa makanisa haya ya mitume na manabii wote wanaenda kanisani ila kuna maimuma, asha, mwajuma pia isaka na yakobo. Wanavaa suruali (mavazi ya kipagani) na wanamuabudu yesu na majina yao ni asha.

Kwahyo chakuhitimisha mungu haitaji dini yako, anahitaji imani yako ambapo imani n uhusiano wa wewe na yeye. Ndio sbb adam hakupewa imani ila alikuwa akiongea na mungu na mungu alikuwa akimtembelea saa za jion na wanae kain na abeli walikuwa na utamaduni wa kutoa sadaka za mazao na wanyama kwa mungu. Pia hawakuwa na dini walikuwa na utamaduni tu
Ahsante mkuu...
 
Mkuu dhehebu nililokuwepo hawafundisi utatu.... Siamini katika utatu binafsi yupo Mungu mkuu mweza wa yote ishu yangu ni kuachana dini,.

sema biblia za hii dini nimeziondoa kwangu maana zinanikumbusha niliyoyapitia kwenye hyo dini...
Utatu mtakatifu upo ila siyo utatu wa nafsi 3 za Mungu ...nafsi ya mungu ni moja tu
 
Ushirika na waamini wenzio ndio huunda umoja wa mafungamano na Mungu. Mungu hakutuumba kuishi na kutenda pekeyetupekeyetu tunategemeana kwa kila nyanja.
Kujitenga na jumuiya ya waamini wenzako ni ubinafsi.

Kama viungo vya mwili vinavyotegemeana ndivyo waamini huunda mwili mmoja Kwa kutegemeana.
" Mtu hawezi kuwa na Mungu kama Baba kama hayupo na Kanisa kama Mama". Rudi kundini katika udhaifu na ubora ndio tunakamilishana pamoja.
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
 
CHUKIZO LA UHALIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU NI HAYO MADHEHEBU NA WAUSIKA WAKE
Unasemea lile yesu alitaja kwenye mathayo 24:15? Kumbe ni hzi dini.. Ahsante mkuu sikujua. SIsi tumekuwa tukifundishwa na UMOJA WA MATAIFA(UN)
 
Ushirika na waamini wenzio ndio huunda umoja wa mafungamano na Mungu. Mungu hakutuumba kuishi na kutenda pekeyetupekeyetu tunategemeana kwa kila nyanja.
Kujitenga na jumuiya ya waamini wenzako ni ubinafsi.

Kama viungo vya mwili vinavyotegemeana ndivyo waamini huunda mwili mmoja Kwa kutegemeana.
" Mtu hawezi kuwa na Mungu kama Baba kama hayupo na Kanisa kama Mama". Rudi kundini katika udhaifu na ubora ndio tunakamilishana pamoja.
Ni kundi gani au dhehebu gani ni sahhi?
 
Mkuu dhehebu nililokuwepo hawafundisi utatu.... Siamini katika utatu binafsi yupo Mungu mkuu mweza wa yote ishu yangu ni kuachana dini,.

sema biblia za hii dini nimeziondoa kwangu maana zinanikumbusha niliyoyapitia kwenye hyo dini...
Kuna kitu kinaitwa pure religion unakijua ni nini ...ni kujua mema na mabaya kisha kutenda mema na kuacha mabaya ...huo ndiyo msingi mkuu wa dini ya kweli na ya haki
 
Sawa mkuu, je ni dini/dhehebu gani lililo sahh??
Hakuna dini ya kweli na hakuna imani ya kweli. Kama n muhumini wa ukristo yaani ni mfuasi wa dini ya kiksristo utakubaliana na ukwel kuwa yesu alipokuja hakuwa kwenye dini yoyote isipokuwa alihubiri kwa kutumia torati ya musa ya zamani hizo. Lkn baada ya kuondoka wale wafuasi wake 12 (motume 12) walielekezwa wakahubiri habari njema za yesu sio wakasambaze dini ya ukristo NO. N wakahubiri habari za yesu na ikaelezwa kila atakayeamini na kubatizwa ataokoka. Inamaana atakayeamini na kubatizwa n mfuasi wa kristo, sio amejiunga na dini ya ukristo. Kwahyo mpk hapo utaona ukristo sio dini ni kufuata na kuyaishi maisha sawa na aliyoyaishi yesu na yaliyofundishwa na mitume wale 12. Mpaka hapo niambie dini ya kweli ni ipi

Sasa kuwaunganisha wahumini pamoja ili kuwatengeneza kama jumuhia wasaidiane na kutambulika kourahisi ndio linakuja kuanzishwa dini ya wakristo. Kwahyo dini ni utaratibu ulioanzishwa na watu. Kwahyo kabla ya dini watu walikuwa kwenye imani pekee dini hazikuwepo
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....

Jibu haya hili swali kwanza:

- Mungu ana utaratibu wa kuabudiwa, na ili umuabudu lazima ujue utararibu wake; Je utamfahamuje?
 
Back
Top Bottom