NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Hakuna MUNGU wa waIslam na wakristo.Ila kuna nabii Mohamed na MASIHI Issa bin MariamSasa kama we ni Mwislam Unavyoabudu kupitia ALLAH huoni ukimuona mkristo anaomba kupitia YESU au YEHOVA anaabudu miungu mingine na sio MUNGU. na Kinyume chake pia.
Au we umeona Mungu wa hizi dini wanafanana wapi?
Hawa walitumwa na MUNGU kwa kazi maalum.
Aliyetangulia alikuwa Masihi Issa Bin Mariam wayahudi mnaowasifia walivyomsulubu ikapita miaka 570 MUNGU akamtuma Mtume Mohamed.
Issa Bin Mariam alileta Injili na Mohamed alileta Quoran.
Wote hawa wanatokea tawi la Nuhu,Ibrahim na ndo maana hizi dini mbili zinaitwa dini za Ibrahim
Huyo mnayemuita YESU ni jina tu liloletwa na Wazungu Jesus waswahili tukasema YESU.
ila ujue nikuambie jina la nabii yeyote linatakiwa litamkwe kama liivyo.
Ndio maana muislam aliyebobea kwenye dini hawezi kukwambia anamuabudu YESU ila atakuambia anamuabudu Issa Bin Mariam.Na waislam wanakubali alizaliwa bila kuwa na baba wa kibayolojia na ndio maana wanatamka Issa bin Mariam.Ila Mohamed alizaliwa na baba na mama.
Mwisho wa yote MUNGU wa wakristo ni huyo huyo wa waislam