Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Hakuna dini ya kweli na hakuna imani ya kweli. Kama n muhumini wa ukristo yaani ni mfuasi wa dini ya kiksristo utakubaliana na ukwel kuwa yesu alipokuja hakuwa kwenye dini yoyote isipokuwa alihubiri kwa kutumia torati ya musa ya zamani hizo. Lkn baada ya kuondoka wale wafuasi wake 12 (motume 12) walielekezwa wakahubiri habari njema za yesu sio wakasambaze dini ya ukristo NO. N wakahubiri habari za yesu na ikaelezwa kila atakayeamini na kubatizwa ataokoka. Inamaana atakayeamini na kubatizwa n mfuasi wa kristo, sio amejiunga na dini ya ukristo. Kwahyo mpk hapo utaona ukristo sio dini ni kufuata na kuyaishi maisha sawa na aliyoyaishi yesu na yaliyofundishwa na mitume wale 12. Mpaka hapo niambie dini ya kweli ni ipi

Sasa kuwaunganisha wahumini pamoja ili kuwatengeneza kama jumuhia wasaidiane na kutambulika kourahisi ndio linakuja kuanzishwa dini ya wakristo. Kwahyo dini ni utaratibu ulioanzishwa na watu. Kwahyo kabla ya dini watu walikuwa kwenye imani pekee dini hazikuwepo
Mkuu nisave hii maelezo yako yamenyooka na yanaeleweka sana.
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....

Ukitaka kujua Dini ndani na nje SOMA!
Tatizo wengi sikiliza maneno ya watu wanafikiri ndio DINI
Jaribu ISLAM utanishukuru baadae!
 
Kwanini isiwezekane ? Na kabla hatujafika mbali Mungu yupi sababu kuna wanaoamini Mungu mmoja na wengine wanaamini Miungu; na wewe leo unaweza ukaja na mchanyato wako kulingana na Imani yako itakavyokutuma...,

Kwahio kulingana na Imani yako hilo linaweza lisiwezekane; ingawa logically sababu hii ni imani na hao wanaoamini vinginevyo hawana Hati Miliki na Imani hivyo vyovyote wewe swaga tu..., Ila sisi kama Jamii baki, so long as Imani yako sio Kero kwetu basi vyote ni Kosher...
 
Hakuna dini ya kweli na hakuna imani ya kweli. Kama n muhumini wa ukristo yaani ni mfuasi wa dini ya kiksristo utakubaliana na ukwel kuwa yesu alipokuja hakuwa kwenye dini yoyote isipokuwa alihubiri kwa kutumia torati ya musa ya zamani hizo. Lkn baada ya kuondoka wale wafuasi wake 12 (motume 12) walielekezwa wakahubiri habari njema za yesu sio wakasambaze dini ya ukristo NO. N wakahubiri habari za yesu na ikaelezwa kila atakayeamini na kubatizwa ataokoka. Inamaana atakaye Kwahyo mpk hapo maisha sawa na aliyoyaishi yesu na yaliyofundishwa na mitume wale 12. Mpaka hapo niambie dini ya kweli
Nakubaliana na hili mkuu...
Dhehebu nililokuwemo lina kawaida ya kuhubiri lengo ni kugeuza watu wawe wa hlo dhehebu, binafs nimekuwa nikiona s sahhi, badala yake waambiwe kuhusu UFALME WA MUNGU na kile utawafanyia na kile wafanye kuurithi, ambacho ni kuacha dhambi na kumfuata kristo..

Mkuu ahsante maneno yako yamenisaidia sana, nilipanga kugeukia ATHEISM
 
Jibu haya hili swali kwanza:

- Mungu ana utaratibu wa kuabudiwa, na ili umuabudu lazima ujue utararibu wake; Je utamfahamuje?
Mungu hana utaratibu wa kuabudu isipokuwa ana utaratibu wa anavyotaka uishi kulingana naye. Anaeleza amri ya kwanza na kuu ni UPENDO baada ya kumpenda na kuwapenda wengine ACHA (DHAMBI) sio uache uovu ni uache dhambi kwsbb dhambi n kwenda kinyume na maagizo ya mungu na kufanya maovu n kwenda kinyume na utamaduni unaoishi ndani yake ambao umetengenezwa na jamii.
Ukifanya jambo nafsi yako ikaumia na ikikukataza usifanye na ukalazimisha kufanya ni dhambi ila ukifanya ubaya nafsi ikawa kimya sio dhambi ila kwa mujibu wa kamatazo ya jamii yako ni kufanya mabaya.

Sauti ya onyo la kutofanya dhambi binadamu yyte anayo awe muislamu, mpagani au mkristo wote wanayo na wanaisikia ndio maana mtu unaskia anasema nlitaka kufanya hv ika roho ikaniuma (roho ikaniuma - SAUTI YA MUNGU IKAMKATAZA) angefanya ndo ingekuwa dhambi sasa.
 
Ili uweze kuelewa jua kwamba Muumba wako hana dini wala dhehebu, dini na dhehebu zimeletwa na mtu au mwanadam,

Pia elewa kwamba majira hii Muumba wako anaishi ndani ya Moyo wako as long as umekubali kusamehewa bure (Isaya 43:25, Isaya 56:15,ufunuo 21:3).
 
Mungu hana utaratibu wa kuabudu isipokuwa ana utaratibu wa anavyotaka uishi kulingana naye. Anaeleza amri ya kwanza na kuu ni UPENDO baada ya kumpenda na kuwapenda wengine ACHA (DHAMBI) sio uache uovu ni uache dhambi kwsbb dhambi n kwenda kinyume na maagizo ya mungu na kufanya maovu n kwenda kinyume na utamaduni unaoishi ndani yake ambao umetengenezwa na jamii.
Ukifanya jambo nafsi yako ikaumia na ikikukataza usifanye na ukalazimisha kufanya ni dhambi ila ukifanya ubaya nafsi ikawa kimya sio dhambi ila kwa mujibu wa kamatazo ya jamii yako ni kufanya mabaya.

Sauti ya onyo la kutofanya dhambi binadamu yyte anayo awe muislamu, mpagani au mkristo wote wanayo na wanaisikia ndio maana mtu unaskia anasema nlitaka kufanya hv ika roho ikaniuma (roho ikaniuma - SAUTI YA MUNGU IKAMKATAZA) angefanya ndo ingekuwa dhambi sasa.

Hakuna kitabu cha dini chochote ambacho akijaeleza namna ya kumwabudu, ujuaji maandazi
 
Nakubaliana na hili mkuu...
Dhehebu nililokuwemo lina kawaida ya kuhubiri lengo ni kugeuza watu wawe wa hlo dhehebu, binafs nimekuwa nikiona s sahhi, badala yake waambiwe kuhusu UFALME WA MUNGU na kile utawafanyia na kile wafanye kuurithi, ambacho ni kuacha dhambi na kumfuata kristo..

Mkuu ahsante maneno yako yamenisaidia sana, nilipanga kugeukia ATHEISM
Nahisi umezaliwa miaka ya 90 kurudi nyuma na uliushuhudia ule ukristo halisi ambao sio dini. Ule ambao hata mtoro wa shule ya msingi alikuwa na uwezo wa kumwombea mtoto mwenzake mapepo yamepanda na akatulia. Halafu kinachokutesa ni hiki cha leo upako unakaa kwenye maji, mafuta, vitambaa na chupi za upako waumini wamebakia magalasa matupi yasiyo nannguvu wala msaada kwa jamii
 
Ha ha ha! Lazima Uwe na mechanism ya kumfaham, nayo ni Dini!
Nadhani Mungu amejifunua kwetu kwa njia 2.
moja ni uumbaji na ya pili ni biblia yaani NENO lake...
so unasema nikichunguza nature/uumbaji na kusoma na kuichunguza biblia inatosha... kumbuka haya bila kuwa backed na matendo mema ni bure....
 
Inawezekana tena sana.Nadhani kwenye barua za mtume Paulo kuna sehemu kajibu maana ya kanisa la kweli ni nini.Anaongelea nafsi yako na moyo wako(na sio hizi sijui RC,EAGT,PAG n.k kama ntakuwa siko sahihi unaweza kusoma zile nyaraka)

Kabla ya haya madhehebu watu walikuwa wakifanya ibada tu vizuri kwa Mungu na kujibiwa.Nani anaweza kutoa ushahidi kwamba Ibrahim,Jacob,Isaac walikuwa wakristo wa madhehebu fulani lakini mbona walikuwa wakiwasiliana na Mungu tu vizuri.

Nadhani mitume wote waliotajwa katika biblia hawakuwa na dhehebu lolote.Hii inaweza kuwa sawa mpaka kwenye Quran(Japo kwenye Quran sina uhakika,wenye kujua vizuri watakupa majibu sahihi)
 
Hakuna kitabu cha dini chochote ambacho akijaeleza namna ya kumwabudu, ujuaji maandazi
Vitabu vimeeleza utamaduni wa waarabu wanavyomuabudu mungu na ukristo wayahudi wanavyomuabudu mungu. Haujasema mungu mwenyewe ameaaagiza wamwabudu hivi

Utaratibu wa kuabdu ulipaswa kutolewa kwa adam ila tunaona mpk waizrael wanapelekwa utumwani hakuna utaratibu wa kuabdu uliokuwepo isipokuwa kulikuwa na taratibu mbalimbali za kutoa sadaka na za kuabduku kwa nyakati tofauti tofauti na kwa mitume tofauti tofauti. Utaratibu mmoja haukuwepo.

Mimi naamini utaratibu wa kumwabudu mungu n kwa kupenda watu na kuishi kwa kufuata ile sauti ya ndani (inner voice)(ambayo kwakwel n sauti ya mungu mwenyewe)) zaidi ya hapo kutoa kwa jamii (ndio sadaka)
Hakuna kitabu cha dini chochote ambacho akijaeleza namna ya kumwabudu, ujuaji maandazi
 
Nahisi umezaliwa miaka ya 90 kurudi nyuma na uliushuhudia ule ukristo halisi ambao sio dini. Ule ambao hata mtoro wa shule ya msingi alikuwa na uwezo wa kumwombea mtoto mwenzake mapepo yamepanda na akatulia. Halafu kinachokutesa ni hiki cha leo upako unakaa kwenye maji, mafuta, vitambaa na chupi za upako waumini wamebakia magalasa matupi yasiyo nannguvu wala msaada kwa jamii
Ahahah kuna hadi chupi za upako, aiseee

Mimi ni wa 98 mkuu.. Japo naona kuna kitu hakipo sawa katka dini za leo..... Tofauti na yale yaliyo kwenye biblia..

Mfano yohana 3:16 kumuamini YESU ndn msingi wa kukombolewa na si kuwa muumini hodari wa dini...

Yaani ukiangalia kwa umakini badala watu wamuamini/kumuabudu Mungu wao wanaabudu dini na wachungaji wao, jambo ambalo si sawa,.
 
Inawezekana tena sana.Nadhani kwenye barua za mtume Paulo kuna sehemu kajibu maana ya kanisa la kweli ni nini.Anaongelea nafsi yako na moyo wako(na sio hizi sijui RC,EAGT,PAG n.k kama ntakuwa siko sahihi unaweza kusoma zile nyaraka)

Kabla ya haya madhehebu watu walikuwa wakifanya ibada tu vuzuri kwa Mungu na kujibiwa.Nani anaweza kutoa ushahidi kwamba Ibrahim,Jacob,Isaac walikuwa wakristo wa madhehebu fulani lakini mbona walikuwa wakiwasiliana na Mungu tu vizuri.

Nadhani mitume wote waliotajwa katika biblia hawakuwa na dhehebu l sina uhakika,wenye kujua vizuri watakupa majibu sahihi)
Ahsante mkuu, mpaka majuzi hapa nilijuliza hvi noah aliyeokoka gharika je alikuwa mTAG,PAG Au RC?

Ukiangalia kwa kina kilichompa kibali mbele ya Mungu ni uadilifu wake na si udini.,.
 
Ahahah kuna hadi chupi za upako, aiseee

Mimi ni wa 98 mkuu.. Japo naona kuna kitu hakipo sawa katka dini za leo..... Tofauti na yale yaliyo kwenye biblia..

Mfano yohana 3:16 kumuamini YESU ndn msingi wa kukombolewa na si kuwa muumini hodari wa dini...

Yaani ukiangalia kwa umakini badala watu wamuamini/kumuabudu Mungu wao wanaabudu dini na wachungaji wao, jambo ambalo si sawa,.
Hili ndio tatizo la kuanzishwa kwa dini. Kwasababu dini ni jumuhia (kusanyiko la watu wenye lengo la kumwabudu mungu) sasa hili kusanyiko likamchagua askofu (kiongozi wao). Serikali ikaanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa hizi jumuhia zijiendeshe (kusaidia) kwenye uchaguzi mgombea akaenda kuomgea na askofu aruhusiwe kuomba kura kwa wahumini wa baba paroko. We baba paroko ulyekula ruzuku kuanzka january hadi october, November utakataa kumruhusu aongee na kanisa kuomba kura?
Hapo ndipo lengo la imani likabadika kutoka kumwambudu mungu na kuwa jumuhia ya wakristo walio ndani ya dini ya kikriato. Imani imeshaondoka imebakia jumuhia kwsbb ya kuruhusu imani kuingiliwa na siasa na kuzaa dini
 
Ahsante mkuu, mpaka majuzi hapa nilijuliza hvi noah aliyeokoka gharika je alikuwa mTAG,PAG Au RC?

Ukiangalia kwa kina kilichompa kibali mbele ya Mungu ni uadilifu wake na si udini.,.
Haya madhehebu ni institutions zilizo jishikiza kwenye dini.Kuna uwezekano zikapotea lakini bado watu wakabaki kufanya ibada tu vizuri na Mungu akajibu maombi yao
 
Kwa kweli BIBLIA ninaitilia mashaka...

Nikitazama ufanisi(COMPLEXITY) uliopo duniani na ulimwenguni kwa ujumla inakuwa vigumu kufikia mkataa wa kuwa Mungu hayupo..
Nini kinakufanya uamini dunia imeumbwa na Mungu ikiwa hujui Mungu alipotokea?

Ikiwa unaweza kuamini ulimwengu uliumbwa na Mungu ambaye chanzo chake hakijulikani unashindwaje kuamini kwamba hata Ulimwengu chanzo chake hakijulikani?

Ikiwa unaamini Mungu alijiumba unashindwaje kuamini pia ulimwengu ulijiumba?

Infact hakuna anayejua jambo lolote kuhusiana na Chanzo cha Maisha na Ulimwengu, Wote tumejikuta tu tupo duniani.

Ukisoma biblia utashangaa kuona hata kitabu cha Mwanzo hakikuandikwa na Adam mwenyewe 🙄🙄
 
Back
Top Bottom