blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
Je’ ni kweli kila kitu ni mpango wa Mungu? Kwa muujibu wa biblia yapo maandiko mengi ambayo kwakweli yana hitaji tafakari nzito, kuyaelewa. baadhi ya maandiko ya biblia…Ni kama haya.
4 ‘’Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya’’. Methali 16
“Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu,” inasema Biblia. Mfalme Sulemani mwenye hekima wa kale, ambaye aliandika maneno hayo, aliendelea kusema kwamba kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kujenga na wakati wa kubomoa, wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia. Mwishowe akasema: “Mtendaji ana faida gani katika jambo analofanyia kazi ngumu?”—Mhubiri 3:1-9
13 Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake. Mhubiri 7
10 Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu,
11 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
12 aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.
13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.
16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?
20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? Warumi 9.
1 Bwana akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako.
2 Utanena hayo yote nikuagizayo; na ndugu yako Haruni atanena na Farao, ili awape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.
3 Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri.
4 Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa hukumu zilizo kuu. Kutoka 9.
Je' inawezekana kila binadamu kabla ya kuzaliwa tiyari Mungu anamjua na hata mwisho wake anaujua?
Kama mambo ndivyo yalivyo mbona sisi tunalaumiana?
NB: Mods naomba hii maana isiamishwe kwenye jukwaa la dini sababu siyo ya kidini.