Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Daudi alikuwa nabii? Mbona nyie waongo
Matendo ya mitume ya mitume 2:29-30
Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petu mpaka leo. Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.



Kwa hiyo na hapo wamedanganya au?
 
Hana sifa za kuwa Mungu
BIBLIA SIO HIYO QURAN YENU ,

YESU NI MUNGU NA ANA SIFA ZA KUWA MUNGU ,

USHAHIDI HUU HAPA👇👇👇

1. Umilele – Yesu ni wa milele kama Mungu.

Mungu: “Bwana, wewe mwenyewe umekuwa makao yetu kizazi baada ya kizazi. Kabla milima haijazaliwa, wala hujaiumba dunia na ulimwengu, Naam, tangu milele hata milele, wewe ndiwe Mungu.” (Zaburi 90:1-2)

Yesu: “Mimi ndimi Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.” (Ufunuo 22:13)


2. Uwepo Kila Mahali (Omnipresence) – Yesu yupo kila mahali kama Mungu.

Mungu: “Je! Mtu ye yote aweza kujificha mahali pasipo mimi kumuona? Asema Bwana. Je! Mimi sijazijaza mbingu na dunia?” (Yeremia 23:24)

Yesu: “Kwa maana walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:20)


3. Ujuzi wa Yote (Omniscience) – Yesu anajua yote kama Mungu.

Mungu: “Hakuna kiumbe kilichofichika machoni pake; lakini vitu vyote viko uchi na wazi mbele zake yeye aliye na mambo yetu.” (Waebrania 4:13)

Yesu: “Sasa tunajua ya kuwa wewe unajua mambo yote, wala hunahitaji mtu akuulize; kwa sababu hiyo twasadiki ya kwamba umetoka kwa Mungu.” (Yohana 16:30)


4. Uweza wa Yote (Omnipotence) – Yesu ana uweza wote kama Mungu.

Mungu: “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu liwezalo kunishinda?” (Yeremia 32:27)

Yesu: “Yesu akawaangalia, akawaambia, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu; kwa maana mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” (Mathayo 19:26)


5. Uumbaji – Yesu aliumba vyote kama Mungu.

Mungu: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” (Mwanzo 1:1)

Yesu: “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” (Yohana 1:3)


6. Kusamehe Dhambi – Yesu ana mamlaka ya kusamehe dhambi kama Mungu.

Mungu: “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitayakumbuka dhambi zako.” (Isaya 43:25)

Yesu: “Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (akamwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwalie godoro lako, uende zako nyumbani kwako.” (Marko 2:10-11)


7. Kutoa Uzima wa Milele – Yesu anatoa uzima wa milele kama Mungu.

Mungu: “Kwa maana kwa wewe chanzo cha uzima; Katika nuru yako tutaona nuru.” (Zaburi 36:9)

Yesu: “Mimi ndimi huo mkate wa uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kamwe; naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” (Yohana 6:35)


8. Kuhukumu Ulimwengu – Yesu ni hakimu kama Mungu.

Mungu: “Kwa maana Mungu ndiye atakayemleta kila kazi hukumuni, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” (Mhubiri 12:14)

Yesu: “Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote.” (Yohana 5:22)


9. Kupokea Ibada – Yesu anastahili kuabudiwa kama Mungu.

Mungu: “Bwana, Mungu wako, utamwabudu, umtumikie yeye peke yake.” (Mathayo 4:10)

Yesu: “Nao wakamsujudia, wakamwambia, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.” (Mathayo 14:33)


Sifa hizi zinathibitisha
kuwa Yesu ni Mungu, mwenye mamlaka, uweza, na ukuu sawa na Baba.
 
Kumbe ataye kuja ni mtu na wala siyo Mungu???a
 
Kwa hiyo alirithi uungu kutoka kwa Mungu mwingine
Yesu ni Mrithi wa Vyote , usimfananishe na Marehemu Muhammad kijana

Waebrania 1:2
“Mwisho wa siku hizi amesema nasi katika Mwana, aliyemweka kuwa MRITHI wa vyote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.”

Waebrania 1:8-9
“Lakini kwa habari ya Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya adili ni fimbo ya ufalme wako. Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo, Mungu, Mungu wako amekutia mafuta Kwa mafuta ya furaha kupita wenzi wako.”


Aya hizi zinathibitisha ukuu wa Yesu kama Mungu, Mrithi wa vyote, na aliyepewa heshima ya kipekee na Baba
 
Kwa nini mwanzo ulisema ni binadamu wa kawaida
Yesu ana Sifa 100% za ubinadamu, na 100% Uungu

Hapa kuna aya zinazothibitisha kuwa Yesu alikuwa binadamu kama sisi:

Waebrania 2:14
"Basi, kwa kuwa watoto wameushiriki mwili na damu, yeye naye vivyo hivyo alishiriki katika hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi."

Waebrania 4:15
"Kwa maana hana mkuu wa makuhani asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi."

Aya hizi zinaonyesha kuwa Yesu alishiriki ubinadamu wetu kikamilifu, akapitia majaribu kama sisi, lakini hakutenda dhambi.
 
Yesu: “Kwa maana walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:20)
Kwa maana kama hawajakusanyika kwa jina lake basi yeye hayupo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…