Amesimulia ‘Aaishah (Mama wa Waumini): (رضي الله عنها):
Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa ndoto njema usingizini na alikuwa haoni ndoto isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana, na alipendezeshwa kujitenga. Alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akimwabudu (Allaah Pekee) mfululizo kwa siku nyingi kabla ya kwenda kwa familia yake. Na anachukua chakula cha safari cha kutosha, na kisha alirejea kwa (mkewe) Khadiyjah (رضي الله عنها) kuchukua chakula tena mpaka ukweli ulishukia alipokuwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika alimjia na alimtaka asome. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akajibu, “Mimi sio msomaji.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kusema: “Malaika akanishika kwa nguvu na akaniminya kwa nguvu mpaka nikapata tabu. Kisha aliniachia, na tena akanitaka nisome na nikamjibu, ‘Mimi si msomaji’. Baada ya hapo akanishika tena akaniminya kwa mara ya pili mpaka nikapata taabu. Kisha akaniachia akasema:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾
Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
Amemuumba mwana Aadam kutokana na pande la damu linaloning’inia.
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote. [Al-‘Alaq: 1-3]
Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alirejea na Wahyi, na huku moyo ukidunda kwa nguvu. Kisha alikwenda kwa Khadiyjah bint Khuwaylid (رضي الله عنها) akasema, “Nifunikeni! Nifunikeni” Wakamfunika mpaka hofu ikatoweka, kisha akamueleza kila kitu kilichojiri akasema, “Naogopa nafsi yangu, kuna kitu (kibaya) kinaweza kunitokea.” “Khadiyjah (رضي الله عنها) akajibu, “Hapana kamwe! Wa-Allaahi, Allaah Hatokudhalilisha. Wewe una mahusiano mazuri na ndugu na marafiki, na unawasaidia masikini na mafukara, unawakirimu wageni wako na unawasaidia waliofikwa na majanga.” Kisha Khadiyjah (رضي الله عنها) alifuatana naye kwa binami yake, Waraqah bin Nawfal bin Asad bin Abdil-‘Uzzah, ambaye wakati wa Jahiliyya (kabla ya Uislam) alikuwa Mkristo na alikuwa akiandika kwa hati za Hebrew. Aliandika kutoka Injiyl kwa Hebrew kiasi alichowezeshwa na Allaah. Alikuwa mzee na alipoteza uoni (kipofu). Khadiyjah (رضي الله عنها) alimwambia Waraqah: “Sikiliza Hadithi (kisa) ya mpwa wako. Ee binami yangu!” “Waraqah akauliza, “Ee mpwa wangu! Umeona nini?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alielezea yote aliyoyaona. Waraqah akasema, “Huyu ni yule yule anayehifadhi siri (Malaika Jibriyl) ambaye Allaah alimpeleka kwa Muwsaa. Natamani ningekuwa kijana, na niishi mpaka pale watu wako watakapokufukuza.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza, “Je, Watanifukuza?” Waraqah akasema, “Mtu yeyote aliyeleta kitu kama ulicholeta alikabiliwa na misukosuko; na kama nitaikuta siku utakayofanyiwa uadui nitakuhami kwa nguvu zote.” Lakini baada ya siku chache Waraqah alifariki dunia na Wahyi ulisita kwa muda.
Wapi wamesema akitaka kujinyonga?