Major hapo Israel imeonyesha mfano na wenye uelewa wameelewa. Iran imerusha makombora na drones 330 hivi, madhara yaliyoonekana ni madogo sawa na hamna. Mechi zilichezwa viwanjani, ndege ziliruka kwenye airports, kazi ziliendelea maofisini na viwandani.
Waisraeli wakafanya advertisement ya uwezo wao. Wakaweka air corridor Syria (kwa kulazimisha sio kwa kuomba). Wakaenda Iraq wakapenya anga, wakafika mpakani wakaachia air launched ballistic missiles zikaenda deep into Iranian territory na kushambulia air defense system asset ya kinu cha nyuklia na kufanya damage. Hilo ni tangazo kwamba uwezo tunao msitujaribu.
Kwenye hatua za kushambulia vinu vya kinyuklia, Iran na Israel zinajua hatua ya kwanza ni kushambulia air defense systems zake. Then ndio sites zishambuliwe, Israel imefanya hivyo bila kujulikana wameona matokeo tu.