Je, Israel kwa sasa iko tayari kushambulia vituo vya ki Nuclear vya Iran?

Israel kasema ataenda kupiga vinu vyote vya Iran bila kushirikiana na USA..
Vyanzo vingi vya habari wanadai kuwa safari hii Israel itatumia fighter jets nyingi za kisasa zenye uwezo mkubwa.
Israel akaanzisha vita na Iran peke yake hata masaa 24 hayaishi Teraviv yote itageuka majivu

Vile vidron vitoi vilivyorushwa na Iran kipindi kile asilimia 90 alisaidiwa na marekani na uingereza kupunguza madhara

Marekani mwenyewe amefyata Mkia maana ameambiwa Mimi Iran sio kama hao wengine unao piganaga nao ukipiga kwangu na Mimi napiga Pentagon na uwezo huo ninao
 
Hayo mawazo huwa mnayatoa wapi?Teh teh teh! Saddam Hussein na scuds zake alijitambisha hivyohivyo.😂😂😂
 
Ndoto
 
Elewa kuwa Israel ina aircraft tankers (Boeing 707s) ambazo F-16, F-15, F-35 etc zinajaziwa mafuta zikiwa angani. Bila hizo, Israel isingeweza ku bomb Iran na Yemen (houthis)
F-15 za Israel zaweza kubeba bunker buster bombs ndio maana lazima ziwe escorted na tankers kwani mzigo mzito wa bombs unapunguza range ya ndege
 
Nani anakudanganya kwamba Israel ina ndege aina ya F-15/F-16 tu.

Sasa subiri utakuja kuona mwenyewe na ole wao Iran wajifanye kususia mazungumzo yao na Marekani kitu ambacho wameshaogopa kufanya.
 
Kuna uwezekano mkubwa wewe umekula Maharage ya jana!!
 
Wewe unapoishia kufikiri Israel ndiyo inaingia hapo kwa kwenda mbele kwa hiyo ukae kwa kutulia au wewe hujui kuwa IDF IS THE MOST MORAL ARMY IN THIS PLANET?
 
(Israel -Yemen) Km 2507,wamemkabidhi Houth kijiti wacheze nae wakijua fika huko umbali hautampa ufanisi,wanajua kuchezea akili za Israel.
How wanajua kucheza na akili za Israel?
 
Ni kwamba unadhani tu hawana au uliona hawana hivyo vifaa?
kiongozi, Iran vinu vyao vipo chini ya milima, halafu bado juu ya hivyo vinu wameweka concrete uwezo wa kuzuia shambulizi la kombora kama bunker buster..

Kabla kombora halijakutana na concrete lazima li penetrate kwenye mlima wenye miamba migumu, lipite kwenye concrete halafu liende ndani zaidi likifika lilipuke kwa ndani... bunker buster ni delay fuse..

Kinachopelekea bunker buster kupenya kwenye ardhi kwenda ndani zaidi ni vitu vifuatavyo...
1-Hard casing(uimara wa material, hutumia tungsten, au steel alloy,) material magumu sana kuzuia lisivunjike.

2-Uzito wa bomu.(Bunker buster zina uzito mkubwa sana ili kufanya liingie ndani zaidi ya ardhi)

3-umbo la bomu(bunker buster imechongoka mbele ili ku penetrate kwenye ardhi ngumu.)

4-Kasi ya kushuka, hii inaongeza uwezo wa kupenya kwa kina zaidi ardhini...

Kumbuka bunker buster ni gravity bombs, hutegemea mvutano wa dunia, yaani linaachiwa kama jiwe au free falling body, japo machache sasa wanatumia rocket na gps...

Hapo kwenye uzito ndipo mada yangu na hoja ilikuwa, je F-16 /F-15 n.k zina uwezo wa kubeba bunker buster kutoka Israel hadi Iran? kumbuka bunker buster kama GBU-28 uzito wake ni tani 2, hili la kisasa wanaita GBU-57 ni tani 13.6 ndilo wanasifu linaweza kupenya ndani zaidi ya ardhi laini kwa mita 60, na kwenye zege hupenya mita 8-20 kutegeme na ugumu wa zege... sasa tafakari mlima ambao una zaidi ya kilomita 3 au 4 na kuendelea halafu kuna zege la kufa mtu chini yake..

F16 yenyewe uzito wake ni tani 8 na pointi je inaweza kubeba tani 13 hadi Iran?
GBU-57 inabebwa na B-2

Halafu hio milima yenye vinu vya nuclear imezungukwa na air defenses, bunker buster inavyopigwa lazima B-2 iende usawa wa huo mlima halafu iachie hilo bomu lianze kushuka hadi kwenye target..
Hapo air defense zita dela na hio B-2...

Israel haina B-2 spirit kumbuka...

Bunker buster ya kulipua vinu vya Iran inapaswa kuwa na uzito zaidi ya tani 13 (GBU-57)... na hapo bado Iran wana vinu vya nuclear kwenye milima tofauti na sehemu tofauti...

Ndio maana nasema hapa kwa hoja Israel haina huo uwezo, nipingwe kwa hoja...
Hata Israel ipewe ruhusa iingie Iran kushambulia hivyo vinu kwa shambulizi moja, hawana ndege za kubeba hilo bomu, hata wakiazimishwa B-2 na US bado hilo bomu halitofika level ya hivyo vinu ....

Na hata ikifika level ya hiko kinu bado Iran wana vinu sehemu tofauti...

Ni impossible 100%...
 
Hii ndiyo taabu ya watu kuvamia fani za watu!! Mwenyewe hapo hata mgambo tu hujawahi kupitia nakushangaa leo unaongelea mambo mazito ya kijeshi ambayo hata uwezo nayo huno matokeo yake unachanganya tu Sentesi!!
Kabla kombora halijakutana na bunker buster lazima li penetrate kwenye mlima wenye miamba migumu, lipite kwenye concrete halafu liende ndani zaidi likifika lilipuke kwa ndani... bunker buster ni delay fuse..
Angalia sasa unavyochanganya madensa!!! Acheni kuvamia fani za watu wengine mnatutia aibu !!!
 
Nani anakudanganya kwamba Israel ina ndege aina ya F-15/F-16 tu.

Sasa subiri utakuja kuona mwenyewe na ole wao Iran wajifanye kususia mazungumzo yao na Marekani kitu ambacho wameshaogopa kufanya.
Israel ina bomber ya kubeba bomu lenye uzito zaidi ya tani 13, na hio ndege isafiri hadi Iran na kurudi hadi Israel?
Vitu vingin zungumzeni kwa hoja acheni movies za hollywood, zungumza realistic..

Mi nakupa facts we unaimba taarabu...

Israel haina strategic bombers kama B-2, B-1 au B-52 , lakini inatumia ndege za kivita zenye uwezo wa kubeba mabomu mazito na kufanya mashambulizi ya kina ni kama bombers ndogo kwa mazingira ya Mashariki ya Kati.

Katika ndege waliyonayo ambayo ina uwezo mkubwa wa kubeba mizigo mizito na kusafiri umbali mrefu ni F-15i inabeba hadi tani 11.. hebu tueleze wana ndege gani nyingine yenye huo uwezo?
Na hapo inabidi kuwe na drop tanks au air refueling kwa kutumia ndege kama KC-46 Pegasus au KC-707...

Wekeni hoja acheni ngonjera na propaganda, vita si movie...

Kumbuka F-15I inabeba mizigo mizito kuliko F-35 Adir ambayo tani 8.2 kwa external na internal, F-35 mizigo na silaha inabeba kwa ndani ili iwe stealth, lakini ikibebeshwa tani 8.2 zote inabidi mizigo mingine ikae kwa nje na hapo inakuwa sio stealth tena.. je iatapenya anga la Iran...? kwanza haitofika kwa maana hata bunker buster moja ya GBU-57 uenye tani 13 haina uwezo wa kubeba...

Twendeni na hoja tuache taarabu..
 
Wewe unapoishia kufikiri Israel ndiyo inaingia hapo kwa kwenda mbele kwa hiyo ukae kwa kutulia au wewe hujui kuwa IDF IS THE MOST MORAL ARMY IN THIS PLANET?
Acha taarabu za Khadija Kopa, weka nondo , weka hoja, kama umeishiwa hoja sema...
Unazungumzia movies za hollywood sisi tunazungumza kwa hoja...

Kwanza we ni mweupe na hata kukujibu nakuwa nakuonea..
 
Kuna watu humu jamiiforums naweza kupingana nao kwa hoja, na hizi mada tulishajadili humu miaka nyuma..

Wewe ni taarabu tu huwa unaimba.. hujui hochote kuhusu geopolitics na masuala ya kijeshi... ni mahaba juu ya Israel yamekujaa..
 
F-15I ndio ndege ya Israel yenye uwezo mkubwa wa kubeba mzigo mzito takribani tani 11... Itaweza kubeba GBU-28 yenye tani 2, GBU-28 uwezo wa kupenya concerete kwa mita 6 tu, yaani hii itumike labda kuchimbua mashimo baadhi ya Hamas...

GBU-57 ndio bunker buster itapenya mita 8-20 na uzito wake ni tani 13, hapo tayari F-15I haina uwezo kubeba huo mzigo..

Tufanye imebeba hio F-15I ikaachiwa makusudi iingie Iran iachie hilo kombora la bunker buster, halitofika kwenye kinu kilicho chini ya mlima... sana sana wataua mijusi na nyoka huko milimani, hata level ya zege hilo bomu halifiki, F-15I itaweza kukimbia mashambulizi ya air defenses?

Vitu vingine mnafurahisha sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…