zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
- Thread starter
- #21
Hapana hakuchagua kwa sababu wao ni bora zaidi au walizaliwa sehemu fulani tu ya dunia soma hapaHahaa...Taifa Teule, sasa iweje Mungu ambaye hana upendeleo awe na taifa teule tena? Ina maana kuna watu wengine wanakuwa na maana zaidi kwake kisa wamezaliwa sehemu fulani ya Dunia tu na sio matendo yao?
Kumb. Torati 7:7-8
7 BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu.
Ukisoma hapa utaona Mungu hakuona wana maana yeyote bali aliwachagua sababu ya agano lake na Abraham maana kipindi cha Abraham dunia ilikuwa imegeukia upagani na miungu ya babeli chini ya Nimrod ila Abraham pekee ndio alikuwa ameshikilia imani ya huyo MUNGU.
Ni sawa na wewe ukiwa bado hujachagua chama cha siasa lakini ukaona CCM inakuletea maendeleo,inakujali shida zako,inasikiliza maoni yako je ukifika wakati wa uchaguzi 2020 utachagua chama gani?? Si utaenda CCM?? same to God naye aliwachagua sababu walikuwa waaminifu kwake.
Tena ukitaka kujua Mungu hachagui watu sababu ni wa maana kuliko wengine pitia hapa
1 wakorintho 1:27
27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko