Nashukuru kwa hoja na ukaribisho wako.
Naomba ukumbuke agano la jipya ni marejeo ya agano la la kale kwa wale walioandika agano jipya.
Wakichofanya ni ku compare yale yaliosemwa zamani yawe katika wakati uliopo.
Paulo Alikua anawaambia warumi si kwamba Neno la Mungu limetenguka kwa sababu si wote waisraeli walio uzao wa israel (naiongeza mimi si wote walio wakristo watokanao na kristo)
Alichokua akiangalia Mungu ni Ahadi rejea sura 9-9 warumi.
Naomba niegemee agano la kale zaidi sura ya 31- 3 Yeremia Mungu anasena hivi "naam nimekupenda kwa upendo wa milele"
Mkuu nadhani unaelewa maana ya neno milele.
Na aliekua akiambiwa amependwa kwa upendo wa milele ni israeli alie mzao wa ibrahim kulingana na warumi 9:9 "maana ahadi ni yenyewe ni hii, wakati maalam nitarudi nae sara atapata mtoto".
Sura ya 31:20 yeremia anaandika "je efrahim si mwanangu mpendwa? Maana kila nisemapo neno ninamkumbuka sana, kwa sababu hio moyo wangu unataabika kwaajili yake BILA SHAKA NITAMREHEMU. Asema Bwana.
Mpaka hapo mkuu unaona nafasi ya Rehema ilivyo kubwa mpaka moyo wa Mungu unataabika kwaajili ya mzao wa israel.
Mungu alitoa ahadi ya Upendo wa milele kwa israeli na ujajua wazi kabisa Mungu hasemi kitu asicho kitekeleza.kwa hali kama hiyo mkuu atashindwaje kumsamehe israeli kwa kosa lolite?
Sura ya 31:27-28 Yeremia anaandika "Mwenyezi Mungu asema hivi, tazama siku zinakuja nitakapoijaza nchi ya israeli na yuda watu na wanyama. 28"kadiri nilivyokua mwangalifu kuwang'oa kuwaboma kuwaangsha kuwaharibu na kuwatesa ndivyo nitakavyokua mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.
Sura ya 31:36 Yer. Mwenyezi Mungu asema hivi "mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku. Pia mimi huitikisa bahari nayo hutoa mawimbi: jina langu mimi ni Mwenyezi Mungu wa majeshi. Basi nami nasema KADIRI NINAVYOTEGEMEZA MIPANGO HIO YOTE YANGU, KADIRI HIO HIO ISRAEL WATAKAVYOBAKI KUWA WATU WANGU.
31:37 Yer kama mbingu zinawezekana kupimwa na misingi ya dunia kuchunguzwa basi nitawatupilia mbali wazawa wa israel kwa sababa ya mambo yote walionitenda. Mimi mwenyezi Mungu nimesema.
Ndugu yangu
zitto junior na wadau wengine, kwenye Biblia inapotaja dunia ujue ina maana ya ulimwengu.
Mimi nawe tumeshuhudia zama zetu ukuwaji wa tecnologia lakini hijaweza kuupima au kuuchnguza msingi wa ulimwengu na wala anga halijajulikana kwao.
Mungu aliahidi kama utakujawezekana kuupima msingi wa mbingu ndipo atakapowatupa wana wa usrael.
Mstari ule wa 36 ametaja nmna anavyofanya kazi mf kuitisa bahari kuamrisha jua na mwezi na nyota kuwa sehemu yake kwa mpangilio ameahidi kwa namna hio hio anavyotenda ndivyo atakavyowahifadhi wana wa israel.
Mpaka hapo hakuna shaka juu ya israeli kwamba nafasi yake kwa Mungu sio ndogo.
Swali ambalo halina majibu ni kwa sasa hao wana wa israeli waliotajwa ndio hawa tulio nao sasa?
Rejea rumi 9:9 kwamba ahadi ilikua mahsiusi kwa mwana wa sara never otherwise.
Karibu mkuu.