Kwa mtazamo wangu ni kwamba kulikuwa na mafarisayo na wanasheria na kwa leo ungewaita elites,,,hawa Yesu hakuwataka kabisa maana walikuwa wanafki.ila sio watu wote wa Israel walikuwa mafarisayo na wanasheria,,ilikuwa ni sehemu ya watu wachache.Na kufa kwa Yesu pia sio wayahudi wote walifurahia,,kuna wengi tu walimuona ana haki,,,ila wale elites wengi wao ndio walitaka afe tena na baadhi yao walimuona ana haki pia ila kwa kuwa lilikuwa jambo lenye msukumo wa rohoni hawakuweza kulipinga.Kanisa halijachukua haki yote ya wana wa Israel..Na hata wayahudi kumuua Yesu walikuwa wanatimiza kusudio lililokuwa la zamani kabla ya kuwepo taifa la Israel.Kumbuka hapa duniani hata hao wayahudi wanatumikia makusudio yanayotakiwa yatekelezwe.Hawapo kama wamiliki ila wenye kumilikiwa,,na kwao ni njia ya kupitia Mambo mengi ya dunia.