Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?

Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?

Kuna kitu kimoja kingekuwepo kama kusingekuwa na Israel yenye waisrael.

# Mungu angeprove kwamba ni muongo.Maana aliweka agano na Ibrahim.
Kwamba ahadi alizomwahidi Ibrahim hakuweza kuzisimamia.

# Kwa hio hii nchi ingekaliwa na watu wengine hata hio Habari ya hakuna Mungu ingeanza kuwa na mashiko,,maana kama Mungu angekuwa kafeli kwa wayahudi hata sisi tungekuwa na mashaka ya kumuamini.

Lakini sivyo ilivyo maana yote aliosema Mungu yapo vile vile na ameprove kwamba sio muongo na kila alichosema kiko vile vile.Sio Mungu wa kusadikika.Yupo..
 
Yehova sio concept,,kabla ya wayahudi kulikuwa na watu waliomjua na kumuabudu Jehovah,,fuatilia Habari ya balaam na balack ufikiri wao walikuwa wanamuabudu Mungu gani.Pia hao wakwe wa musa walikuwa wanamjua pia huyo Mungu waliemuabudu wayahudi na sio kwamba kaanza kuabudiwa baada ya kuwepo taifa la Israel.

Zaidi sana jiulize kwamba huyu Mungu kaanza kuabudiwa lini? Kwa vizazi vyote tokea Adam?
Concept ya taifa teule,ilianza wakati wa moses(kama aliwahi kuishi),ni wakati wa moses ndipo jina la mungu jehova lilipojitokeza,
wakati huyu mungu akijitambulisha kwa moses,alisema kuwa kina Abraham,isaka na yakobo hawakumtambua huyo mungu kwa jina la jehova,

hapa unapata kujua wazi kuwa abraham,isaaka na yakobo waliabudu mungu yuleyule alieabudiwa na watu wa caanan,mungu huyo ni El,
na hata abraham kipindi akiwa mgeni pale kaanan,alimtambua Melkizedeki kama kuhani mkuu wa mungu El,

huyo el alikuwa mungu mkuu wa jamii zote za caanan,

sasa unajiuliza kwani jehova aendelea kukubali taifa lake teule litumie jina la mungu wa kipagani?

Jehova anajitetea kwa moses kuwa ,hapo mwanzo kina abraham,isaac na yakobo walinjua kwa jina jingine lakini jina lake halisi ni jehova,

lakini tena ukirudi kuchimba story ya jehova,inaonekana jehova alikuwa ni miongoni wa miungu iliyoabudiwa na kabila la wamedian,Yahwew ama jehova kwa kiswahili alikuwa ni mungu wa vita wa median,kwahiyo inshort alikuwa mungu wakipagani pia,

baada ya moses kumuua mtumishi wa farao alikimbilia nchi ya midian,akakaa kwa miaka mingi,na huko ndiko alipomuoa mkewe zilipa,
baba mkwe wa moses alikuwa ni kuhani wa mungu yahwew ama jehova kwa kiswahili,

so huko median ndiko hasa concept ya mungu jehova alipoitoa moses,

na ni hapo ndipo concept ya taifa la mungu ilipoanza
 
Nje ya kujadili na kukosoa imani za watu wengine huwa huna kazi ya kufanya?Au ndivyo mnafundishwa pale kwenye chuo cha Ahsante Nkapa pale Morogoro?Why don't you invest more of your time trying to solve the problems facing your religious community in which ignorance and poverty are persistent?Ukiyafanya hayo hakika utapata thawabu kwa Mnyazi Mungu na jamii yako itapunguza chuki kwa jamii zilizo busy kujishughulisha na maendeleo yao kiuchumi,kiroho na kijamii.
Ni ushauri tu ndugu yangu!
Shukrani mkuu wa ushauri mzuri....
 
Kuna kitu kimoja kingekuwepo kama kusingekuwa na Israel yenye waisrael.

# Mungu angeprove kwamba ni muongo.Maana aliweka agano na Ibrahim.
Kwamba ahadi alizomwahidi Ibrahim hakuweza kuzisimamia.

# Kwa hio hii nchi ingekaliwa na watu wengine hata hio Habari ya hakuna Mungu ingeanza kuwa na mashiko,,maana kama Mungu angekuwa kafeli kwa wayahudi hata sisi tungekuwa na mashaka ya kumuamini.

Lakini sivyo ilivyo maana yote aliosema Mungu yapo vile vile na ameprove kwamba sio muongo na kila alichosema kiko vile vile.Sio Mungu wa kusadikika.Yupo..
Mkuu labda sijaeleweka hakuna mahali nimesema Mungu kavunja AGANO na Abraham na Israel

Pia nimekubali Israel ni nchi ya ahadi

Pia nimekubali Israel ilichaguliwa na Mungu

Pia nimekubali Israel inahusika na unabii wa siku za mwisho

LAKINI nachohoji Israel ni nani kwa muktadha wa agano jipya.... Je ni lile taifa la kina Netanyahu lililopo pale mashariki ya kati au ni wakristo yaani waliomfuata Yesu.

Na nimeweka hapo mistari juu hivyo jikite hapo je Israel ni nani??

Natanguliza shukrani
 
AFTERMATH
Hivyo basi kwa kuwa Mungu alikwisha dhamiria kurudisha uhusiano na mwanadamu ikabidi ageukie mataifa mengine ambayo ndio yangeendeleza agano lile na hapo ndipo likapatikana agano jipya ambapo neema ya wokovu haukuwa wa Wayahudi pekee sababu walimkataa bali ukawa wa mataifa yote as long as watamfuata Yesu (Yohana 1:11-12) pia Mathayo 21:42-43 ambapo tunaona ufalme wa Mungu umehamishwa kutola Israel kwenda kwa mataifa mengine.

42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.

View attachment 929907

Swali linaibuka je Israel inabakia taifa la Mungu??

NDIO ni kweli Mungu aliendelea na agano na taifa la Israel ila tafsiri ya taifa la israel ni lipi limebadilika kupitia agano jipya.

Warumi 9
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.

Na pia hapa ndipo tunaona kunazaliwa waisraeli wa kimwili (mashariki ya kati) na Israel ya Kiroho (wakristo)

Warumi 2:28-29
28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Hivyo kufikia hapa tunaona kuna wayahudi/waisrael aina mbili sasa je ahadi za ISRAEL ya agano la kale anarithi nani za kuwa taifa teule,chaguo la Mungu n.k

Galatia 3
6 Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu
.
.......................................
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.Ahadi kwa Abrahamu
..............................
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Kupitia mistari hii tunaona sasa ahadi zote walizopewa Abraham na Israel zinarithiwa rasmi na wale wote wamfuatao Yesu yaani wakristo ambao ndio wale paulo kawaita waisrael wa Kiroho sio kimwili. Hivyo ningependa nichukue fursa hii kutoa msimamo wangu kwamba Israel hii ya kimwili sio taifa la Mungu na halitokaa liwe unless na wao wamfuate Yesu hapo ndipo watakuwa NCHI YA AHADI na taifa la Mungu. Kwa kuhitimisha kupitia agano jipya ambapo sasa wanaomfuata wote Yesu bila kujali ni muisrael au lah ndio wanakuwa TAIFA TEULE ama ISRAEL hivyo baraka zote ahadi zote na unabii wote wa TAIFA LA ISRAEL sio tena wa hii Israel ya yakobo bali ni wote wamfuatao Yesu kristo na hii ni kwa mujibu wa Biblia.

However upande kinzani unasema Israel ya mashariki ya kati bado ni taifa teule kama zamani na hakuna kilichobadilika na wanatumia mstari huu.

Warumi 3:3-4
3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.

Nakubaliana na Mstari huu unaosema Mungu hajawaacha wayahudi licha ya kumkataa lakini bado msimamo uko pale pale kwamba ni lazima wamkiri massiah ndio wawe teule till then hawana tena hadhi ya kuitwa taifa teule kulingana na vifungu nilivyoweka.
View attachment 929908

ANGALIZO
Kumekuwa na interpretation nyingi sana za unabii kuhusu Israel ya kimwili yaani hii ya mashariki ya kati na nina hofu kuwa na wakristo pia wameingia mkenge kama wa wayahudi wa kale kwa kutoelewa unabii na wakatafsiri kwa akili zao kiasi kwamba Yesu alipokuja hawakujua na wakamkataa. kuna wakristo wengi leo wanaamini vita na matetemeko yaliyotabiriwa kwenye ufunuo ni ya kimwili au hekalu litajengwa kimwili hivyo watashituka Yesu amekuja kivingine wao bado wanasubiri vita ya amragedon sijui kujengwa hekalu ilihali hizo mambo zina maana tofauti kabisa ingawa hii ni mada ya siku ingine ila nachoweza hitimisha ni kwamba Biblia imeandikwa kwa codes nyingi hivyo kuitafsiri inahitaji umakini na utulivu sana sio kwenda kichwakichwa mfano inapotabiri kuwepo kwa njaa na kiu haimaanishi njaa ya kimwili ila ukisoma Amos 8:11 utajua njaa inaongelewa ni ya kusikiliza neno la Mungu such phrases mtu akisoma kwenye ufunuo ana conclude kuwa kutakuwa na njaa,vita matetemeko,ukame huu wa kimwili kumbe zina maana nyingine kabisa hivyo nilitaka kuliweka hilo sawa. Kwa kusema hayo naomba kuwasilisha mada kwa ajili ya michango na maoni ya wanajukwaa letu pendwa.

Cc cc Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Mkuu umeiva, kifupi tu waisrael wa mashariki ya kati Mugu kawalaani.
 
Asante sana mkuu zitto junior kwa mada hii pia pole kwa kejeli ya mdau mmoja hapo juu.

Umeelezea vizuri sana kwa kile kilichoitwa taifa teule hakipo tena kijiografia bali kiroho. Lakini kule kuwepo kiroho kwa siku hizi hakutaondoa ile ahadi alioahidi Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim.
Yametokea mambo mengi sana tokea kipindi kile mpaka ujio wa Kristo,na tokea Kristo mpaka leo hadi kiyama.
Unaweza kua zile kabila 12 za yakobo zilizo zaa Israeli hazipo tena katika umoja ambao ungezaa taifa lakini katika ufalme ule wa Mungu israel hatakosa kiti chake iwe ameamini Kristo ama laa.

Kule kuamini kwetu kristo sisi wa mataifa mengine ndio kumetupa nafasi ya kuwa taifa teule la Mungu hata kama kimwili hatukutahiriwa .

Lakini tujue toba ya israel inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi kuliko mwingine kwa sababu Mungu yeye alisema ni Mungu anaetimiza makubaliano.
Alisema pia mwingine anaweza kumwadhibu kwa gango iwapo akipotea lakini Israeli anamudhibu kwa fimbo nyembamba kumrejesha.

Nafasi ya israeli kwa Mungu sio ndogo kwa sababu ya ahadi/agano.
Nafasi kwa Mkristo kwa Mungu sio ndogo kwa sababu ya kuamini.

Wale wote (YESU) waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyaka wana ambao si kwa nguvu ya mwanadamu bali kwa nguvu ya Mungu mwenyewe.
 
Mkuu nashukuru kwa mchango wako ila labda tuwekane sawa....
1. Majibu yangu yote ni kwa mujibu wa AGANO JIPYA hiyo bold ya kwanza ningeomba tusaidiane umeisoma wapi kwenye Bible kuwa muisrael ataenda mbinguni hata kama hajamkubali Yesu??

Yohana 14:6
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Sasa naomba tusaidiane mstari ambao unasema mtu anaweza kwenda mbinguni bila kumkubali Yesu???

2. Pia umesema toba ya israel husikilizwa haraka sababu Mungu anatimiza agano..... Sijakataa toba ya Israel au agano la israel kuwa halitimizwi bali hoja yangu najikita ISRAEL ni nani.... Je warithi wa agano la Abraham ni nani??

Galatia 3
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

Sasa tunafahamu wenye imani kwa Mungu agano jipya ni wakristo sababu walimuamini Yesu sasa hao wayahudi ni lini walimuamini Yesu?? Kama hawana imani huoni automatically sio watoto wa Abraham

Galatia 3
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Hivyo ningeomba unionyeshe wapi kwenye agano jipya ambapo Israel ya netanyahu iliwahi kuwa ya wakristo ili wawe watoto wa Ibrahimu

Kwa kuhitimisha ningeomba pia unipe maana ya mstari huu

Mathayo 21:43
42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake

Je biblia ina maana gani kusema ufalme wa Mungu umeondolewa kwa Israel kwenda mataifa mengine.....

Karibu kwa mjadala
 
Pongezi Sana kwako mkuu Zittor Jr kwa mada nzuri kwani umeitendea haki wakati naisoma hi mada mchango wangu naona mkuu mpalasinge kashauchangia...maana ukisoma Vizuri warumi 11 yote utazidi kupata majibu mengine ambayo yanafanya uone kwanini waisrael wamekua hivi walivyo leo
 
Nafikiri shida ilianzia kwa Esau alipokubali kuuza haki yake ya uzao wa kwanza ndio ikampa confidence Yakobo kuwa yeye ndio anastahili baraka za ''first born'' ikapelekea atumie ujanja mwingi ili aweze kutumia hiyo fursa aliyoachiwa na Esau.

Pili kwenye Biblia Mungu alikuwa anaheshimu sana maamuzi ya watu wake mfano Nuhu alimlaani Canaan kisa dhambi ya baba yake yaani Ham na Mungu aliitimiza laana hiyo kwa kuangamiza kizazi chote cha canaan kupitia Israel.....

So Mungu habariki wizi bali ametuachia free will ya kuamua hatma yetu yeye anasimamia tu.... Sasa Isaka ndio kambariki Yakobo hapo Mungu azuie tena ilihali ni maamuzi ya Isaka mwenyewe!!! Ila kama wamgemshirikisha Mungu kabla ya kutoa hizo baraka huenda ndio Mungu angeingilia na kumpa haki yake Esau!!

Muhimu hapa ni kumshirikisha Mungu mapema ndio hatoruhusu walaghai kama Yakobo kujipenyeza.
Shida ilianzia toka tumboni mkuu Na Mama yao Rebeka alikua anajua kwani alijulishwa na BWANA baada ya kuuliza Soma mwanzo 25:21-23 angalau ni nje ya mada
 
Mkuu nashukuru kwa mchango wako ila labda tuwekane sawa....
1. Majibu yangu yote ni kwa mujibu wa AGANO JIPYA hiyo bold ya kwanza ningeomba tusaidiane umeisoma wapi kwenye Bible kuwa muisrael ataenda mbinguni hata kama hajamkubali Yesu??

Yohana 14:6
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Sasa naomba tusaidiane mstari ambao unasema mtu anaweza kwenda mbinguni bila kumkubali Yesu???

2. Pia umesema toba ya israel husikilizwa haraka sababu Mungu anatimiza agano..... Sijakataa toba ya Israel au agano la israel kuwa halitimizwi bali hoja yangu najikita ISRAEL ni nani.... Je warithi wa agano la Abraham ni nani??

Galatia 3
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

Sasa tunafahamu wenye imani kwa Mungu agano jipya ni wakristo sababu walimuamini Yesu sasa hao wayahudi ni lini walimuamini Yesu?? Kama hawana imani huoni automatically sio watoto wa Abraham

Galatia 3
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Hivyo ningeomba unionyeshe wapi kwenye agano jipya ambapo Israel ya netanyahu iliwahi kuwa ya wakristo ili wawe watoto wa Ibrahimu

Kwa kuhitimisha ningeomba pia unipe maana ya mstari huu

Mathayo 21:43
42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake

Je biblia ina maana gani kusema ufalme wa Mungu umeondolewa kwa Israel kwenda mataifa mengine.....

Karibu kwa mjadala
Nashukuru kwa hoja na ukaribisho wako.

Naomba ukumbuke agano la jipya ni marejeo ya agano la la kale kwa wale walioandika agano jipya.

Wakichofanya ni ku compare yale yaliosemwa zamani yawe katika wakati uliopo.

Paulo Alikua anawaambia warumi si kwamba Neno la Mungu limetenguka kwa sababu si wote waisraeli walio uzao wa israel (naiongeza mimi si wote walio wakristo watokanao na kristo)

Alichokua akiangalia Mungu ni Ahadi rejea sura 9-9 warumi.

Naomba niegemee agano la kale zaidi sura ya 31- 3 Yeremia Mungu anasena hivi "naam nimekupenda kwa upendo wa milele"

Mkuu nadhani unaelewa maana ya neno milele.
Na aliekua akiambiwa amependwa kwa upendo wa milele ni israeli alie mzao wa ibrahim kulingana na warumi 9:9 "maana ahadi ni yenyewe ni hii, wakati maalam nitarudi nae sara atapata mtoto".

Sura ya 31:20 yeremia anaandika "je efrahim si mwanangu mpendwa? Maana kila nisemapo neno ninamkumbuka sana, kwa sababu hio moyo wangu unataabika kwaajili yake BILA SHAKA NITAMREHEMU. Asema Bwana.

Mpaka hapo mkuu unaona nafasi ya Rehema ilivyo kubwa mpaka moyo wa Mungu unataabika kwaajili ya mzao wa israel.

Mungu alitoa ahadi ya Upendo wa milele kwa israeli na ujajua wazi kabisa Mungu hasemi kitu asicho kitekeleza.kwa hali kama hiyo mkuu atashindwaje kumsamehe israeli kwa kosa lolite?

Sura ya 31:27-28 Yeremia anaandika "Mwenyezi Mungu asema hivi, tazama siku zinakuja nitakapoijaza nchi ya israeli na yuda watu na wanyama. 28"kadiri nilivyokua mwangalifu kuwang'oa kuwaboma kuwaangsha kuwaharibu na kuwatesa ndivyo nitakavyokua mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.

Sura ya 31:36 Yer. Mwenyezi Mungu asema hivi "mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku. Pia mimi huitikisa bahari nayo hutoa mawimbi: jina langu mimi ni Mwenyezi Mungu wa majeshi. Basi nami nasema KADIRI NINAVYOTEGEMEZA MIPANGO HIO YOTE YANGU, KADIRI HIO HIO ISRAEL WATAKAVYOBAKI KUWA WATU WANGU.

31:37 Yer kama mbingu zinawezekana kupimwa na misingi ya dunia kuchunguzwa basi nitawatupilia mbali wazawa wa israel kwa sababa ya mambo yote walionitenda. Mimi mwenyezi Mungu nimesema.

Ndugu yangu zitto junior na wadau wengine, kwenye Biblia inapotaja dunia ujue ina maana ya ulimwengu.
Mimi nawe tumeshuhudia zama zetu ukuwaji wa tecnologia lakini hijaweza kuupima au kuuchnguza msingi wa ulimwengu na wala anga halijajulikana kwao.
Mungu aliahidi kama utakujawezekana kuupima msingi wa mbingu ndipo atakapowatupa wana wa usrael.
Mstari ule wa 36 ametaja nmna anavyofanya kazi mf kuitisa bahari kuamrisha jua na mwezi na nyota kuwa sehemu yake kwa mpangilio ameahidi kwa namna hio hio anavyotenda ndivyo atakavyowahifadhi wana wa israel.

Mpaka hapo hakuna shaka juu ya israeli kwamba nafasi yake kwa Mungu sio ndogo.

Swali ambalo halina majibu ni kwa sasa hao wana wa israeli waliotajwa ndio hawa tulio nao sasa?

Rejea rumi 9:9 kwamba ahadi ilikua mahsiusi kwa mwana wa sara never otherwise.

Karibu mkuu.
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo maana inagusa moja ya topic zenye utata katika ulimwengu wa imani ila ningependa tusome kwa utulivu uzi wote alafu tujadiliane kwa hoja ili tuweze kusolve hili swali la karne nyingi sasa.
View attachment 929882
UTANGULIZI
Mwanzoni kulikuwa na agano kati ya wanadamu na Mungu kupitia Adam ila tunaona Adam analivunja agano hili

(Hosea 6:7)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu;

Hivyo Mungu alitaka kurudisha uhusiano tena na mwanadamu tunaona akapatikana Nuhu ambaye alimcha Mungu sana na akachaguliwa kuianza dunia upya baada ya gharika. Sasa baada ya gharika dhambi ilirudi tena kupitia Ham ambaye alipelekea Nuhu kumlaani mwana wake Ham yaani canaan kuwa atakuwa mtumwa wa kaka zake Ham yaani Shem na Yapheth (Hili la muhimu sana huko mbeleni) hivyo uzao wa Ham ukawa na watu waovu sana mfano Nimrod wa Babylon aliyeleta ibada za sanamu na dini za kipagani hadi kuleta machafuko kwenye ukoo wa Nuhu na kusababisha dunia nzima kumuacha Mungu wa Nuhu.

Katika sintofahamu hii aliyesimama imara alikuwa Shem/Melchizedek ndie aliendelea kushika wokovu na hata Abraham alipozaliwa aliendelea kumsimamia kiimani na hivyo hata alipokufa Abraham kati ya wanadamu wengi ndio aliendeleza imani ya kumuabudu Mungu wa babu zake (YAHWEH) hivyo baada ya Mungu kuona Abraham ana msimamo thabiti kwake akampa ahadi ya kuwa na uzao wa watu wengi kama nyota za angani lakini pia alimpa ahadi ya kumpa nchi hii ya canaan.

Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Hivyo ni kupitia ahadi hii ndipo taifa la Israel lilipotabiriwa rasmi kuwepo. Na ahadi hiyo itakuja kutekelezwa na mjukuu wake yaani Yakobo ambaye aliiba urithi wa mtoto wa kwanza hivyo hii baraka ya Abraham akairithi yeye na tunaona uzao wake kupitia Joshua na Caleb ndio wanaingia kwenye nchi hii ya canaan rasmi na kuasisi taifa la Israel.

Je Mungu aliichagua Israel??

Kumb. La torati 7:6
6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.

Kupitia mstari huu tunaona Israel ilichaguliwa na Mungu lakini je kwanini aliichagua??

Kumb. Torati 7:7-8
7 BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu.

Hivyo Mungu aliwachagua Israel sababu hiyo ya kutimiza uapo kwa mababu ikiwemo Nuhu + Abraham. Na hili ndio lilisababisha Israel wapewe nchi ya Canaan sababu ilikuwa inahitimisha unabii wa Nuhu kuwa Canaan atakuwa mtumwa wa shem (Babu wa Abraham) na sio kwa sababu nyingine yeyote.

Mwanzo 9
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake

View attachment 929883
Ramani ya canaan

Hivyo baada ya Agano hili na Israel ambalo kupitia wao ndio Mungu alipanga kuwaletea Messiah yaani Yesu ili aweze kurejesha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu kama wa kipindi cha Adamu lakini wayahudi walimkataa Yesu kwa sababu hawakujua kutafsiri unabii ulioandikwa kuhusu maisha ya Yesu kwenye agano la kale. Kwa kifupi maisha yote ya Yesu kuanzia kuzaliwa mpaka kufa yalikuwa yanaendana na unabii wa agano la kale 1 korinto 15:1-4 Mfano wa nabii zilizotimizwa kupitia maisha ya Yesu ni hizi. Kuanza mahubiri yake galilaya ulitabiriwa na Isaya 9:1-2 na ukatimia Mathayo 4:13, Pia Yesu kupanda Punda kuingia jerusalem ulitabiriwa na Zakaria 9:9 na kutimia Mathayo 21:1-9 n.k yaani kuna mistari zaidi ya 100 iliyotabiriwa kuonyesha Huyo Messiah ataishije.

Lakini wao wayahudi hawakuliona hili sababu walidhani Yesu atakuwa handsome boy, Damu ya kifalme,Mwanajeshi kama alexander the great n.k hivyo kwa jinsi alivyokuja "kimasikini" wakaona kama anakufuru mwisho wa siku wakamuua na yote ni kutokana na kushindwa kutafsiri maandiko ya unabii.

Matendo 13:26-27
27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.

Mkuu Hongera sana kwa Kusumbua Bongo na Kufiri sana juu ya Mada hizi ngumu na tata Ubarikiwe tu!
Ningependa kwa kweli kusema machache tu kwa mtazamo wa kidunia na kibiblia na nisingependa kunukuu maandiko mengi moja kwa moja lakini nitakachokisema kinatokana na maandiko machache na historia!

Taifa la Israel! Yaani taifa la Yakobo - Aliyeshindana na Malaika mpaka kukaanza kupambazuka.
Maisha,Tabia za hawa wajamaa yaani hazijabadilika sana.
Nilikuwa nafuatilia historia ya Mawaziri Wakuu wa Israel takribani robo tatu yao sio Wakristo wala Wayudai(Judaism), Ni wapagani typical.Nikajiuliza hivi hili si Taifa la Mungu,wanaongozwa na katiba gani hawa? Inasemaje kuhusu Imani ya Kiongozi wa nchi?
Sifa ni Kuwa Myahudi tu! mengine wala hawajali.
Mwenendo wake tangu watanyike 70 AD,mateso na manyanyaso waliyopitia na hata hatari ya Kutoweshwa katika mgongo wa ardhi inalifanya libaki kuwa Taifa pekee la Mungu ambalo sasa mataifa megine yamebarikiwa kupitia taifa hili Adhimu.
Makanisa yote ya Kipentekoste hapa nchini wameiga ile tabia ya Kupeperusha bendera ya Israel ndani ya makanisa yao wakizingatia maandiko na kuheshimu asili ya Imani ya Ukristo iliko asisiwa.
Hii imeonekana kama kampeni flani hivi inayoitwa Pro - Jews and Jewish state.Kuunga Mkono Uzayuni.
Na kila mtu anayeipinga Israel anaonekana kama Anti - semitic au Mnazi.
Mambo mengi yameendelea juu ya taifa hili;Wameshambuliwa sana;wanahusishwa na Njama kuu za Kuwa ndio Wapotoshaji wa Kubwa wa Ukweli ulimwenguni na Watu wa Njama ya kuja kuitawala dunia katika nyanja zote za maisha -
The Protocols of the Elders of Zion - Ni kati ya kijitabu kinachodhaniwa kuwa kina kanuni na miongozo ya jinsi ya taifa hili litakavyokuja kuutawala Ulimwengu wote kwa hila na Njama kubwa.

Mwandishi Kijana mwenye Upeo kama wa kwako Zitto Jr - Andrew Carrington Hitchcock ameingia kwenye shida kubwa baada tu ya kuandika kinyume na Wayahudi akiwatuhumu kuwa si chochote na wao sio tena Sinagogi la Mungu bali la shetani - Ufunuo 2:9 Naijua dhiki yako na Umasikini wako,(Lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi,nao sio,bali ni sinagogi la Shetani.

Akinukuu tarehe na matukio ya Kihistoria toka mwaka 740 AD hadi mwaka 1897. amechambua njama na hila za Wayahudi kwa jinsi ambavyo ukisoma huwezi tena kuwathamini wayahudi katika uso wa dunia.

Lakini Msingi mkuu wa Hoja yako ni kuwa Iwapo Israel ya Sasa bado inakibari na kicho mbele za Mungu kuendelea kuwa taifa Teule la Mungu au Hisani hiyo imewaangukia waisraeli wa Kiroho ambalo ndio Kanisa la leo! na kinachoendela ni propaganda tu Kanisa?
Jibu langu ni Hapana;Naomba kutofautiana na wewe.Mungu hawezi kuliacha agano lake hata iweje!
Ameahidi kuwa hatawaacha na bado mambo mengi hayajatimia juu ya unabii wa taifa la Israel katika Mwili;Ingawaje kwa matendo yao na Mtindo wa maisha yao mara nyingi haukisi Ukristo wala uchamungu lakini kwa Ahadi ya Mungu mwenyewe hata wakatilia mbali katika mwili la.

Hata tu suala la kuikataa habari njema ilifanyika neema kwa mataifa yote Ulimwenguni - Kwa sababu Yesu mwenyewe anajitanabaisha mwanzoni kuwa hakutumwa isipokuw kwa kondoo wa Israel waliopotea.
Swali la kujiuliza ni Mara ngapi Israel wameshindwa kutekeleza Amri na Maagizo halali ya Mungu kupitia manabii na Mitume ? Je ilikuwa ni sababu ya Mungu kuachana nao na kutafuta taifa lingine tiifu zaidi?

Warumi 11:1-6
Basi, nauliza: je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mimi binafsi ni Mwisraeli mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini. 2Mungu hakuwakataa watu wake aliowateua tangu mwanzo. Mnakumbuka yasemavyo Maandiko Matakatifu juu ya Eliya wakati alipomnung'unikia Mungu kuhusu Israeli: 3Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua? 4Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: "Nimejiwekea elfu saba ambao hawakumwabudu Baali." 5Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake. 6Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.

Warumi 11:28 -29
28 Basi Waisraeli ni maadui wa Mungu kwa sababu ya Injili. Hii ni kwa faida yenu. Lakini kuhusu uchaguzi, Waisraeli bado ni wapendwa wa Mungu kwa sababu ya ahadi yake kwa Abrahmu, Isaki na Yakobo. 29 Kwa maana karama za Mungu na wito wake hazifutiki.

Kanisa ni matokeo ya kazi ya Mungu ya Kipekee kabisa na wala sio Israel mpya!
Kanisa halijaitwa Israel popote katika agano jipya! -1 Wakorintho 10:32.

Ni kweli Taifa la Israeli halijaishi wala kuchangia kazi ya kueneza Injili Duniani kwa kiasi ambacho ilitegemewa;isipokuwa leo linaingiza fedha za kigeni nyingi kutokana na kumiliki sehemu nyingi za kihistoria kuhusu imani hii ya kikristo.

Mauaji yanayolioendelea na kuendelea Ukanda wa Gaza,Katika Makazi ya wapalestina na kwingineko mashariki ya kati hayaondoi ile hiba ya kuwa hawa mabwana ni Wateule.
Waisreli wakristo ni wachache sana! wengi wa wayahudi hawa ni Wapagani na Judaisimu.
Jinsi Vile wanavyoishi na kuenenda isiwe hoja ya kuwahukumu Moja kwa moja;Tumuachie manani atakuja kuwahukumu mwenyewe-tena watahukumiwa hukumu ya kipekee.
Asante Sana.
 
In Exodus 6:2-3- Yahwew the god of israel state that..
"i revelled myself to Abraham,to isaac and to Jacob as El shaddai(God almight)-Mungu mkubwa.

Or El elyon(God the most high)-mungu alie juu.

But was not known to them by my name Yahwew.

As we can see,Abraham,isaac and jacob didnt know Yahwew.

But Genesis indicate that not only the hebrew patriarch,but also,their neighbour in caanan and other throughtout Mesopotamia WORSHIPED EL as the highest God,

for example the king of the town of Salem(the future Jerusalem) greeted and blessed Abraham in the name of the God most high-El Elyon.

==genesis14:19--Melchizedek king of salem brought a bread and wine,He was priest of God most high El Elyon and he blessed Abraham,

it turn out El is not Yahwew

psalm 89:6-7(world english bible version)

-who is like YAHWEW among the SONS of El.?,im the council of the holy ones,El is greatly feared ,he is more awesome than all who surround him,

it turn out kumbe jehova ni mtoto wa mungu el,
 
Yhwew is not the most high God but a son of God in the divine court according to bible,
yahwew is assigned to be Lord god of israel not the most high God elohim.

Deutronomy32;8-9

--when the most high El elyon gave nations their inheritance,when he separated the son of man,He set boundaries of the peoples according to the NUMBER OF THE SONS OF GOD in his devine court,
for the lord(Yahwew) portion was to his people israel,

i have always been explaining we are still worshipping pagan gods,

if you do some search it will led you to claim that,Yahwew in factor was the impostor who claiming to be the almight God,

yahwew was the one who was thrown out of heaven after he wanted to ovethrow God almighty,
some say,yahwew is that snake in eden who tricked Eva and adam into eating from the tree of good and evil.

Remmember when yahwew was killing his people on the desert after the refuse to obey him?,

he told moses to elect a copper snake idol,so whoever looked at the snake was saved from death,

that is a symbolic to worshipping the snake a satan,

remmember when Jesus told the jews that,They belonged to SATAN,that their father was always a deceiver,a Lier,

it is true,we so how jacobo deceiver his father isaac into blessing him instead of Essau,

we saw how jacob deceive his uncle Laban an managed to steal more than half of his livestock etc,

actually i dont beliave all these bullsh*t,
what am sure is all these stories are finction
 
Salamu wana jamvi,
Naomba nianze kuchangia mada hii nikionyesha msimamo wangu na imani yangu kuwa 'Israel hii ya leo bado ni taifa teule la Mungu. Pamoja na michango ya wanajamvi humuna mleta mada kujaribu kushawishi kwa maandiko kuwa Israel hii ya akina Netanyahu si lolote si chochote,na kuwa kanisa la leo ndio Israel mpya.Pamoja na dhumuni la YESU KRISTO kuja duniani kumkomboa mwanadamu hiyo bado haitoshi kulifanya kanisa kuwa Israel kamili hoja za kuunga mkono msimamo wangu ni nyingi na mojawapo ni hizi mbili.
1.Yako mambo yaliyotabiriwa tangu agano la kale hayajatimia na utimilifu wake utafanyika katika Israel hii hii ya akina Netanyahu na tena pale YESU atakaporudi mara ya pili.Hebu tutafakari hii kitu inyoitwa the GOLDEN GATE/EASTERN GATE OF JERUSALEM ambayo imendikwa ndani ya Biblia kwenye EZEKIEL 44.1-2 Nabii Ezekiel alioneshwa kwenye maono kuwa huo mlango/gate la mashariki halitafunguliwa mpaka atakaporudi YESU na sababu zake zikatolewa(Soma Ezekiel 44:1-2) na maandiko mengine nitawaletea na waarabu walishajaribu sana kubomoa huo mlango wa mashariki imeshindikana(Google ujisomee mwemyewe). Hivyo hoja yangu ni kuwa yapo maagano ambayo Mungu aliyaweka tangu enzi za akina Ibrahimu ambayo mpaka sasa yadumu kusubiri kutimia,wapi kama sio ISRAEL ya leo,na mengine mengi.

2.Dunia nzima inafahamu kuwa Israel ya leo ndio yenye wanasayansi bora kabisa waliotapakaa Ulaya na Amerika wakifanya mambo makubwa,kwa mfano inasemekana(sina uhakika) lakini haya yalitamkwa na Waziri mkuu wa Israel kuwa siku za karibuni kuwa katika makampuni makubwa 10 bora duniani ya IT,Telecom,Energy etc,yaliyoko Marekani matano yakiwemo(Yahoo,Whatsapp,Microsoft etc) yana research centres Tel Aviv hii ya leo,Kwa nini? Wazungu wa ulaya na Amerika wanaijua Israel hii ya leo mnayoipinga kuwa inazo zile baraka za Mungu kupitia Ibrahimu na uzao wake.Nani asiyejua kuwa modern agricultuere iko Israel,Jeshi lenye nguvu ni huko.Jamani habari za hili taifa la Isarel wanazijua waarabu wanaoizunguka Israel kama kweli hii Israel ya leo ndio ile ya ahadi ya Mungu?

Nimalize kwa kusema ahadi ya Mungu ni ya milele kanisa la leo kama Israel mpya limeandaliwa kwa ajili ya uzima wa milele baada ya maisha ya hapa duniani,

Nawasilisha, nitarudi
 
Wakuu,
Mimi niseme tu kuwa pamoja na madhaifu yao yote ujeuri walionao,na hata kumkataa YESU KRISTO wakidai bado wanamsubiri mesiah wao,hiyo haiondoi kuwa wao ni taifa teule na baraka alizowatamkia Mungu na maagano aliyoyaweka toka enzi za agano la kale hayajaondoka wala kutenguliwa,ukitaka kuamini kuwa Israel hii ya sasa ndio ile ya kwenye agano la kale nenda kaanzishe vita na wao, au panga njama yeyote ya kulidhuru taifa lao hapo ndio utajua kama Mungu wa baba zao akina Ibrahimu ndio huyu wa akina Netanyahu.

Mungu ni yeye yule jana leo na hata milele,chokoza Israel kama hautauona mkono wa Mungu ukiwatetea, haya mataifa mengine Mungu alituhurumia tu akasema hawa nao ngoja tu warithi baraka za Ibrahimu ingawa hizo baraka mpaka leo huku Africa na kwingineko tunazisoma na pengine hatuziishi ipasavyo
 
DAH: ELIMU MNAYOTOA NYIE WATU WAWILI NI YA PEKEE SANA, napenda mnavojadiri kwa kutumia hoja na mistari kutoka kitabuni!!! Ni ajabu sana, MUNGU awatunze aisee

Back
Top Bottom