Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?

Kwa tambuemi kuna Israel ya sas na Israel ya kale,ni tofauti.
Israel ya kale lilikuwa taifa la Mungu sababu alikua amelichagua kwa ajili ya mtumishi wake Ibrahim Mwanzo 12:7. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ilitimizwa na wazal wa Yakobo/Israel pale walipotolewa Misri chini ya uongozi wa Musa na kuimiliki nchi ya Kanaani, baada ya kumiliki ikawa ya waisraeli. Taifa teule sababu Mungu alikua amelichagua na kulipa sheria na miongozo yake wazifuate. Lakini walianza kuasi agano la Mungu na kuanza kuabudu mabaali,wakaua manabii, mwishowe Yehova Mungu akawakataa Luka 13:34. Mwaka 70 ndio ulikua mwisho wa Israel ya kale pale jeshi la Roma lilipovamia na kuharibu kabisa hekalu,na wayahudi wote wakasambaa kama Yesu alivyosema Mathayo 24:2
Israel ya sasa ni kaa Tanzania tu haina uteule wowote wala uhusiano na Mungu kwani imeanza mwka 1948 ndani ya Palestina.
 
First thing first wahayudi hawapendi wakristo wala waislamu.
 
Wewe ndio wa hovyo kweli, ndani ya Palestina kuna Wayahudi Wakristo na Waislam.
Judaism sio dini tengua kauli yako, wanatumia biblia kuabudu.
.
Alafu huko Palestine kati ya wakristo na waislam dini ipi inazaidi ya 80% ya washirika? Jibu kama ni waislam nyamaza na kama ni wakristo mjadala uendelee
 
Judaism sio dini tengua kauli yako, wanatumia biblia kuabudu.
.
Alafu huko Palestine kati ya wakristo na waislam dini ipi inazaidi ya 80% ya washirika? Jibu kama ni waislam nyamaza na kama ni wakristo mjadala uendelee
1 JUDAISM NI NINI KAMA SIO DINI?
2.MAJORITY RULE MINORITY RIGHT UNAELEWA MAANA YAKE?
Judaism - Wikipedia
 
1 JUDAISM NI NINI KAMA SIO DINI?
2.MAJORITY RULE MINORITY RIGHT UNAELEWA MAANA YAKE?
Judaism - Wikipedia
Haya endelea kuwa na misimamo yako isiyo natija wala uhalisia.
.
Nimebahatika kufika kfar saba ni mji waki_Hebrew ni kazi sana kumpata mzungumzaji wa kiingereza kule kila baada ya hatua tatu unakutana na muyahudi (ambayo wewe unaiita dini) wao wanamisingi yao ambayo pia inatumiwa na kufuatwa na wa_Orthodox wa ukraine 100%.
.
Wanatumia biblia kama tunayoitumia sisi biblia yao ya Early Christianity yenye torati za mussa haitumiki tena kwa wayahudi walio wengi ila misingi yao haijafa.
.
Ni kama wakristo wasasa hutumia zaidi agano jipya na kuachana na lakale kwa mafundisho yaliyomengi (lakini misingi ya ukristo iko palepale.)
.
NB;JUDAISM IS AN EARLY CHRISTIANITY sasa wewe fuata unachokiamini.
.
Kwa kumalizia nenda mkoani dodoma kuna wayahudi wakitanzania na wayahudi wa israel wanafundisha vyema kabisa bila propanganda unazozisikia au kadhuru israel kama unahela.
 
Hivyo umehitimisha uyahudi nini?
 
Uko sahihi, ila kwenye kipengele cha *Angalizo* naona kama hauko sawa.
Njaa, matetemeko, vita n.k vimetabiriwa kuwa vitatokea physically na kuna baadhi yalishatokea.

Mfano WWI, WWII n.k
Sidhani kama waandishi wa Biblia walilenga kuyatabiri haya matukio kwa code!
 
Mkuu biblia imeandikwa figurative sio lateral... Yaani 80% ya maneno yana maana ya kiroho sio kimwili wanatheolojia watanielewa kwa mfano hio njaa Biblia imeeleza vzuri kabisa njaa ni ipi

Amos 8:11
11 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.

Kwenye Biblia ARDHI sio hii ya kimwili bali Ardhi kiroho ina maana Kanisa au wakristo soma wakorintho 3:9 hata vita inayoongelewa sio ya kimwili bali vita za kiroho kati ya wakristo dhidi ya shetani kama

Waefeso 6:10-20
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama


And a lot nikipata wasaa ntaleta mada humu maana naona watu wengi sana mnafikiri Biblia inaongelea vita za kimwili mnapotoka mtashangaa Yesu wenu anarudi huku nyie mnasubiri eti vita sijui matetemeko..... World war 1 ma 2 zimeua watu zaidi ya million 50 je Yesu alirudi?? Matetemeko makubwa yamekuwepo toka karne ya 1 je Yesu alirudi??

Waisrael ndio walipotoka pia walidhani Yesu atakuja kama mfalme fulani wa kimwili ndio maana alipokuja kama mchonga mbao wakamdharau wakamuua

Amkeni wakuu
 
Uyahudi ni nini?
 
Suala la Esau na Yakobo ni tata tangu tumboni. Kimsingi mpango wa Mungu ulikuwa kwa Yakobo ambae ndio Israeli. Esau ni gugu lililopandwa kuuvuruga mpango huo. Ndio maana tunaona mapigano kati yao tangu tumboni mwa nama yao. Yaani yule mpinzani alijaribu kuzuia kusudi la Mungu kwa kuingiza roho ya utasa kwa Rebeka. Ile roho ilipong'olewa akapanda gugu.
Hongera sana mleta mada. Umejitahidi sana kuielezea kwa mapana. Uko sahihi ila usitake kulifuta taifa LA Israeli la kimwili kwani bado lina nafasi take katika mpango mzima wa Mungu. Katika Kitabu cha ufunuo wametajwa kwa kutenganishwa na watu wa mataifa na mabila na lugha mbalimbali. Pia usisahau mambo yote yaliyo katika join went I was roho hudhihirishwa katika ulimwengu wa mwili hadi pale mbingu mpya na nchi mpya zitakapochukua nafasi ya mbingu na nchi ya sasa. Hiyo ni baada ya shetani na walio wake kutupwa jehanamu. Nikipata muda nitachangia baadhi ya vipengele ili tupate kuelimishana kwa mapana zaidi. Ubarikiwe sana.
 
Sio Wayahudi hawa , hawa ni Ma ashkenazi Watu wanitoka KHAZAR KARIBU NA URUDI HAWANA DAMU YA KIYAHUDI KABISA ila walijiigiza kujifanya wayahudi wakati wa vita vya kwanza ili wasiwe chini ya utawala wa KIKRISTO WALA KIISLAM WAKACHAGUA UYAHUDI BUT ki ukweli sio uzao wa YAKOBO na wanafahamu hivyo ASHKANAZI JEWS SIO TAIFA TEULE LA MUNGU
 
Huu ni ukweli mchungu ambao wafia dini hawataki kuusikia..... Kitabu cha 13th tribe kimechambua vizuri sana hii hoja yako.

Shukrani
 
Je,Wayahudi wa UKWELI Ni Wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Haijulikani walipo maana walipotea utumwani zaidi ya makabila 10 na walichanganyika na mataifa mengine hivyo bado hawajulikani wako wapi leo labda iko siku watapatikana ila hawa waliopo Tel Aviv ni wahuni tu waliojivika uyahudi wakati walitokea kwenye milima ya Khazaria na sio Judeah.
 
Mkuu Isaka alikuwa specific alimuita ESSAU kwa jina wala sio kwa TITLE(mzaliwa wa kwanza) , hivyo Yakobo anabaki kuwa mdanganyifu kwa gharama ya mama yake, swali vip Mungu aruhusu aliedanganya apate baraka ?
 
Nimekuelewa vizuri mkuu ila ujue Yacob siyo mwizi, but kulikuwa na utapeli fulani wa kishetani wa kutaka ku-Divert urithi wa Mungu kwa taifa lake pendwa Israel kupeleka upande wa shetani. kila mpango wa Mungu unapofanyika shetani ana plan b, ndo maana alitamka wazi kuwa alimchukia Esau japo yacob babae alimpenda, hata hivo Esau alioa kwa wa- edomites, ambao walikuwa hawa-comply na Mungu na hao hao wa-edom ndiyo walimuua Yesu wakishirikiana na utawala wa Warumi mfano mzuri ni Herode the Great Caipha nk. watu kama, Er na ndugu yake Onan wana wa Judah, na wengine wengi Mungu hakuwapenda sababu hawakufuata misingi ya imani ya Mungu,na pia walikuwa ni plan b ya shetani.always shetani alikuwa ana plant his own seeds katika uzao wa israel kupitia Mwanamke huyu huyu mama wa viumbe vyote [yaani vinavyoonekana na visivyoonekana).


Kwa akili ya kawaida ya kibinadamu tunaoana wizi mwingi na uasherati vilifanyika pale, lakini ilikuwa ni mipango ya Mungu kutunza pure generation of Israel. mfano Judah alimtia mkwewe Tamar na akazaa mapacha Perez na Meziah. kupitia Perez ikawa ni blood line ya King solomon son of David na kuendelea.
 
Mkuu unatuthibitishia kuwa Mungu anaweza kucheza rafu ili mradi tu Mipango yake itimie ?
 
Najaribu kwenda nawe kidogo kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mun
Hahaa...Taifa Teule, sasa iweje Mungu ambaye hana upendeleo awe na taifa teule tena? Ina maana kuna watu wengine wanakuwa na maana zaidi kwake kisa wamezaliwa sehemu fulani ya Dunia tu na sio matendo yao?
Mungu hana ubaguzi, yeyote anayekubalika nae ni wake.... (nimesahau andiko)
Kwa sasa Mungu Israeli haina agano lolote na Mungu, mana waliwakataa manabii wote waliotumwa kwake. Ukitaka uhusiano wako na Mungu ww mkaribiee tu nae atakukaribia (Yak 4:8)
 

Bro yani sina shida kabisa na mtizamo wako, hongera kwako. Ninapopapenda mimi ni mafunuo ya kifikra na sio kimwili kama wengi wanyoamini au kuelewa. Kwamba hata hadithi ya kuanguka kwa kuta za Yeriko kwa kupuliza tu tarumbeta na sauti ni swala la kifikra na sio kimwili.Kila mtu anatakiwa aifikie kanaani yake na kuna kuta za kifikra zinatuzuia bila kujua. Yani ufalme wa mbinguni utanyakuliwa na wenye nguvu, sio nguvu za gym bali za kifikra/kiroho. Kuna namna ya kufikiri sawa sawa. Ukianzisha Uzi juu ya mada hii nitag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…