Kakumamoto
JF-Expert Member
- May 6, 2015
- 1,237
- 1,696
Mkuu biblia imeandikwa figurative sio lateral... Yaani 80% ya maneno yana maana ya kiroho sio kimwili wanatheolojia watanielewa kwa mfano hio njaa Biblia imeeleza vzuri kabisa njaa ni ipi
Amos 8:11
11 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.
Kwenye Biblia ARDHI sio hii ya kimwili bali Ardhi kiroho ina maana Kanisa au wakristo soma wakorintho 3:9 hata vita inayoongelewa sio ya kimwili bali vita za kiroho kati ya wakristo dhidi ya shetani kama
Waefeso 6:10-20
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama
And a lot nikipata wasaa ntaleta mada humu maana naona watu wengi sana mnafikiri Biblia inaongelea vita za kimwili mnapotoka mtashangaa Yesu wenu anarudi huku nyie mnasubiri eti vita sijui matetemeko..... World war 1 ma 2 zimeua watu zaidi ya million 50 je Yesu alirudi?? Matetemeko makubwa yamekuwepo toka karne ya 1 je Yesu alirudi??
Waisrael ndio walipotoka pia walidhani Yesu atakuja kama mfalme fulani wa kimwili ndio maana alipokuja kama mchonga mbao wakamdharau wakamuua
Amkeni wakuu
Hii tafsiri ya kiroho wengi hatuielewi. Hata tukiambiwa ufalme wa mbinguni uko ndani yetu hatuelewi tunasubiri tuuone physically, matokeo yake hatuuishi kama ilivyokusudiwa.