Je, Japan ndiyo nchi inayoongoza kwa kuthamini Utu na Ubinadamu?

Je, Japan ndiyo nchi inayoongoza kwa kuthamini Utu na Ubinadamu?

Nahisi kuna tofauti kati ya utu na ustaarabu!

Kwa mfano, mashabiki kuokota makopo uwanjani=ustaarabu

Vilema kupewa kazi viwandani=utu

Wafanyakazi wa ndege kuomba radhi=ustaarabu


Hakuna mifano mingine ya utu huko Japan?

Mfano, mtu akiwa mgonjwa yumo ndani anapewa kampani + chakula na jirani yake au mpaka aite mamlaka za serikali zije zimsadie bila hivyo anajifia ndani?

Mayatima wanapewa sapoti na wanajamii?

Wazee wanathaminiwa?

Mtu akiwa hana hela yaani ana maisha magumu anapewa msaada na ndugu, jamaa na marafiki?

Wajapani wanasaidiana kifedha mtu na mtu?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Kivyovyote vile lakini wana Utu na Utulivu
 
Hawa jamaa wamebarkiwa Sana , hata hivyo wamefika hapo Kwa Gharama kubwa , waafrica viongozi wetu ni mamluki wa nchi za Magharibi, tunaogopa Gharama ya kujinasua , Africa isahau kufikia level za Asia ambayo pia nchi nyingi zilipitia adha ya kutawaliwa Ila wakajinasua , mara moja moja nchi za Africa hubahatisha kupata viongozi mashuhuri na wenye maono Ila huishia kusalitiwa na kuuliwa ..kila mmoja apambane na Hali yake tuu
 
Zile movie nyingi ni za wachina..Ni kama zile za North na South Korea...Ila kuwa jirani na Mchina lazima mchapane tu siku moja..
Huyo Japan aliua wachina kikatili sana na kubaka wanawake wengi wa kichina hivyo kuna chuki baina yao
 
Hawa jamaa wamebarkiwa Sana , hata hivyo wamefika hapo Kwa Gharama kubwa , waafrica viongozi wetu ni mamluki wa nchi za Magharibi, tunaogopa Gharama ya kujinasua , Africa isahau kufikia level za Asia ambayo pia nchi nyingi zilipitia adha ya kutawaliwa Ila wakajinasua , mara moja moja nchi za Africa hubahatisha kupata viongozi mashuhuri na wenye maono Ila huishia kusalitiwa na kuuliwa ..kila mmoja apambane na Hali yake tuu
DPW
 
Anaandika KENGE,

Katika ulimwengu wa sasa upendo umeingia doa,Upendo hakuna tena,Visa vya ukatili haviishi.Dharau,Majungu na najigambo kuanzia kwa mtu mmoja kwa mwingine(Individually) mpaka mataifa kwa mataifa(internationally).Mataifa yamekosa utu na kuviziana,kupigana na kuuana imekuwa kama tabia sasa

Lakini Nchini JAPAN mambo ni tofauti kidogo.Hawa watu wamekua wakishika vichwa vya habari kwa nyakati tofauti tofauti kwa matendo yao ya UTU na Ubinadamu

Moja ya habari iliovutia wengi mtandaoni ni picha inayowaonesha wafanya kazi(Staff) wa Japan Airline wakiwaomba abiria wao msamaha baada ya ndege kuchelewa kufika uwanjani kutokana na mvua na hali ya hewa kuwa mbaya.

Sio hivyo tu,Kwa wapenzi wa Soka mtakumbuka kombe la dunia lililopigwa nchini Qatar.kuna tukio moja lilifanywa na mashabiki wa japan.Tukio ambalo liliibua hisia za watu wengi na kupelekea Japan kupewa TUZO ya timu yenye nidhamu.

Ilikua ni baada ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Germany,baada ya mchezo mashabiki wa Japan walianza kusafisha uwanja kwa kuokota uchafu wa makopo na makaratasi waliotupa wakati wa kuangalia mpira.Huku kauli mbiu yao ikiwa ni 'Triple C' yani Cheer,Chant,Clean wakiwa wanamaanisha tunashangilia,tunafanya lolote lakini mwisho tutaacha tumesafisha

Tofauti na nchi zetu,Africa mchezaji akifunga atatupiwa chupa,mawe na kumulikwa tochi.Na kama ni derby Mfano Simba na Yanga zinacheza pale taifa timu moja ikifungwa shabiki wanang'oa viti yaani ni vurugu mwanzo mwisho.

Matukio ni mengi ya kuelezea UTU wa watu hawa.Miaka ya nyuma walipitisha sheria wafanyakazi wa kucontrol marobot wanatakiwa wawe ni vilema.Ili kusaidia walemavu kwahiyo ukienda viwandani waendesha robot utakuta ni wengi ni walemavu.

Yapo mengi ya kuelezea UTU wa waJAPAN lakini licha ya kuwa nchi zenye acient ya Asia yaani wachina,Wakorea wamekuwa wakitafuta chokochoko na mataifa mengine.Yani kuvimbiana lakini ni tofauti kwa wenzao JAPAN sio watu wa skendo kabisa

JE kwa karne hii JAPANESE ndio watu wanaothamini UTU na UBINADAMU

Nawasilisha
Wako mtiifu
Fuatilia historia ya Japan... fuatilia vita ya pili ya dunia. Afu ujue wajapan halisi. Hawa wa Japan wa siku hizi wapole baada ya kupigwa bomu. Wajapan Wana historia ya ukatili hujawahi ona
 
Niliwahi kuambiwa huko kuwa suoermarkets zinapata hasara sana kutokana na items nyingi kuonekana kama reject ilhali kwingine duniani zingeweza kuuzwa kama kawaida.
Mfano plastic bottle ya maji ikibonyea kutokana na adha ya usafirishaji Japan huwezi ukaipanga kwenye shelf . ni ya kutupa kwenye dustbin
 
Niliwahinkuambiwa huko kuwa suoermarkets zinapata hasara sana kutokana na items nyingi kuonekana kama reject ilhali kwingine duniani zingeweza kuuzwa kama kawaida.
Mfano plastic bottle ya maji ikibonyea kutokana na adha ya usafirishaji Japan huwezi ukaipanga kwenye shelf . ni ya kutupa kwenye dustbin
Duuh hii balaa sasa
 
Japan mtu watu wakigundulika wamekula rushwa wanajinyonga Kwa aibu...

Huku MLA rushwa ndo tunampa na ubunge....🤣
Yule waziri anaendesha gari la serikali na hawara kumkimbia mke wake anapata ajali na kumuua hawara ndio kwanza second in command anaenda kumtembelea hospital kumfariji na kumpa pole.
 
Fatilia documentaries za kuhusu jela zao ndo utajua kama wana utu na ubinadamu au la!
 
Japani ndio taifa lenye Kujali na Kuthami utu na viumbe wengine.
Japan hakuna kabisa watoto waishio mitaani.
 
Back
Top Bottom