Je, Jeshi la Polisi Tanzania linaruhusiwa kumchunguza Waziri au Naibu Waziri akitenda jinai? Au hadi wapewe ruhusa yakufanya hivyo?

Acha uongo, hakuna polisi wa hivyo tanzania, Gekul atachukuliwa hatua kwa sababu moja tu hili suala limefika kwa rais.
Rais naye kuna amri ngapi amezitoa zikaenda kuathiri raia wasiokuwa na hatia?
 
unampa pole mama chupa au mtu mwingine ?
 
Unaulizia kwa maana ya sheria kuwaruhusu ama mazoea na tabia za upimbi?
 
Labda kwa kuwa ameshatenguliwa !
Vinginevyo mbona walishindwa kumhoji hapo kabla akiwa bado ni naibu Waziri ??!!
 
Toa mfano wa polisi mwenye independent mind.
 
Toa mfano wa polisi mwenye independent mind.
Wapo mkuu,ndomaana unaona wengine hadi wanafikia hatua ya kuacha kazi kwa kuandika barua ndani ya masaa 24,siyo polisi wote wanaendeshwa nje ya viapo vyao.
 
Mkuu swala la sumu kalitaja huyo kijana mwenyewe kwenye clip, usichanganye habari.
 
Mkuu Pole sana kama ulikuwa hujui Vyombo vyetu vya Usalama hasa Polisi hufanya kazi kwa Maagizo/Maelekezo.

Hujasikiliza hata hiyo Clip ya yule Mwandishi wa habari kuwa alizuiliwa kuondoka Nyumbani kwa Mhe. Naibu Waziri hadi aruhusiwe na Naibu mwenyewe.

Hao wanakazi ya kupokea maagizo tu
 
"Mfumo wetu wa siasa unakataza indirectly Kiongoz wa kisiasa au chama tawala kuhojiwa anapotenda jinai . Vinginevyo lazima wapokee maelekezo kutoka kwa viongozi wa kisiasa wasipofanya hivyo". Haya ni maelezo au ni swali? Andika kwa usahihi.
 
Inasikitisha sana.
 
Sasa hao polisi ni sehemu ya watesaji, je wanaweza kujichunguza? Rejea kesi ya kina Zombe. Kweli hili la huyu Waziri na polisi pia wameshiriki kutesa na kunyanyasa.
 
Inasikitisha sana.
Katiba yetu ina mapungufu mengi mno hasa hii loopholes ya Viongozi wa kisiasa kuwa na amri kwa hao Mapolisi.

Unakuta jambo lipo kwenye mamlaka ya upelelezi ama vinginevyo lakini Waziri/RC/DC/PM/VP ama namba moja mwenyewe anatoa agizo linaloingilia utendaji kazi wao.
 
Na ubunge huyu asirudi tena
Wamtoe nje ya mstari kabisa
Awe benchi

Ova
Wamepiga hela sana hawa
Ingekuwa Rais mtu wa bifu
Hapo angechunguzwa mpaka mali zake na kutaifishwa, lazima amepiga hela sana
Ubunge atapigwa chini hataupata tena, tusubiri mda utasema
 
Ni utawala uliojaa sura ya kinafiki kuhusu haki. Double standards, chukua mfano Naibu waziri fulani aliyepata ajali na akatuhumiwa ushiriki wak kifo cha mwanafunzi UDOM alikingiwa kifua na kila mweny mamlaka ya kufanya hivyo.

Huyu wa sasa, it seems she was working independently without the influence of the bigwigs

Lakini la pili kwa sababu alitokea CDM kwa hiyo nyoka ya kijani inahisi akawa double agent ndio maana wamemtosa kabla ya uchunguzi kufanyika. Mamlaka yake ya kinidhamu imkaa kimya badala yake kaondoshwa kwnye nafasi usiku!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…