PreGE2025 Je, Jimbo la Kisesa watakubali kumtosa Mbunge wao kipenzi ndugu Mpina kirahisi?

PreGE2025 Je, Jimbo la Kisesa watakubali kumtosa Mbunge wao kipenzi ndugu Mpina kirahisi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Atapitishwa kikaragosi ili tu mpina atoswe. Kisesa wana mbunge mzuri sana ila ndio hivyo atatoswa
Mpina toka aondolewe uwaziri akili imemruka sio yule tena

Anahitaji tiba ya akili na roho hayuko vizuri kabisa Kajaa Hallucinations nyingi kichwani
Nyingi mno
 
Mpina agombee kupitia jukwaa lingine, chamachake kwautawala huu washamuonesha chuki kubwa kisa mawazo yake fikirishi wao wanataka nyimbo za kusifu tuu
 
Kwa mazingira ya sasa Mpina hawezi kuwa mbunge tena, akibaki CCM hata akipita kura za maoni atakatwa kwa amri ya Samia, na hata akienda chama kingine hata wapiga kura wakimchagua kwa 90% hatatangazwa kuwa ameshinda kwa amri ya Samia.Bila mabadiliko Tanzania hakuna uchaguzi kura hazina thamani tena. No Reforms No Election.
 
Mpina toka aondolewe uwaziri akili imemruka sio yule tena

Anahitaji tiba ya akili na roho hayuko vizuri kabisa Kajaa Hallucinations nyingi kichwani
Nyingi mno
basi, kama shida ni kukosa uwaziri msimtotese ubunge
 
Hellow!

Nimesikia kiongozi mmoja akielekeza wapiga kura kuwa, Mbunge aliyepo Ndugu Mpina hafai kuwa Mbunge wa jjimbo Hilo. Kwamba anatafuta umaarufu jukwaani,

Kwamba hatoshi kwenye Nafasi hiyo na kwa dharau kubwa anawaambia wana Kisesa kuwa labda aletwe bungeni kwa Nafasi zile kumi za upendeleo. Kelele za shangwe alizopigiwa Mbunge wa Kisesa ndugu Mpina zinaonyesha kwa kiasi gani anakubalika na wananchi.

Swali LANGU ni kuwa, ikiwa ndugu yetu Mpina jina lake litafanyiwa fitna na kutorudi, umma wa Wananchi uliomshangilia muda wote pale mkutano, utaelewa kirahisi kumtosa Mbunge wao kipenzi?

NB: Uchaguzi ni baada ya kufanyika reforms kwenye katiba kupata tume huru ya uchaguzi,

NO Reforms NO Election 💪 🔥

Abarikiwe sana ndugu Mpina,

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿
Mpina ni mbunge pekee ambaye ametekeleza majukumu yake kikamilifu.
Wanachotaka kumfanyia ni kumuondoa kijanja.Mwenyekiti wake angesema asiwe mbunge kabisa ameogopa angesababisha taharuki.

Lakini kusema kweli baada ya uchaguzi Mpina hatakuwa mbunge na hata huo wa kuteuliwa hatapata.
 
Mimi sio chama chao lkn nakwenda na Luhaga Mpina mwenye ujasiri wa kukosoa, Macha wote , nasema machawa wote ndio wanamuona mpina hafai, la hasha, MPINA AMENYOOKA
NA BUNGE LIJALO MPINA ANARUDI MJENGONI KWA KISHINDO.
 
Kiongozi anatakiwa atokane na wananchi. Kama bado wanampenda, CCM wamrudishe tu sababu mbunge ni muwakilishi wa wananchi, sio muwakilishi wa chama chake.​
 
Kwa huu mfumo mbovu wa kila kiongozi wa siasa lazima ateuliwe na chama ni kwamba chama hakitampitisha .
Hoja ya Marehemu Mtikila ya Mgombea binafsi hadi leo serikali inashindwa kuijibu kwani ni takwa la kikatiba na lina kubalika kimantiki
Kama kila raia aliyefikisha miaka zaidi ya 18 anaruhusiwa kuchagua kiongozi bila kupitishwa na chama cha siasa inakuaje sasa raia huyo akatazwe kugombea pasipo kupitishwa na chama.
Nchi inahitaji kuruhusu mgombea binafsi
 
Hakuna mbunge au kiongozi yeyote anachaguliwa na wananchi hii nchi. Kisesa itawakilishwa na chawa ambaye mfumo umemchagua.
Unataka kusema hata akina Mbowe na Lissu walipokuwa wabunge hawakuchaguliwa na wananchi?
 
hachaguliki wewe ni raia wa kisesa? kachague mdebwedo huko kwenu zanzibar unakoishi, ya kisesa waachie wanakisesa.
watamnyorosha vizuri sana akithubutu kupeleka kiburi chake kwenye debe gentleman
 
kubomoa jina la mtu ni sekunde ila kulijenga ni miaka, na unaweza bomoa tofali moja nyumba nzima ikaanguka
 
Back
Top Bottom