Yesu alihubiri upendo, ndiyo tofauti yake na Eliya, Eliya aliua manabii wa Baali lakini Yesu akiwa msalabani alisema "Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalolitenda... "
Usimdhihaki
FaizaFoxy mfundishe kwa upendo. Hata Paulo kaandika muwaonye wazee kwa heshima
Ndugu yangu, duniani hapa kuna kundi fulani hata uwapigie ngoma hawawezi kuelewa.
Luka 7:32
Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
...................
Hilo kundi liliongelewa na Manabii wa
Agano la Kale.
Isaya 6:9
Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione.
..............................
Likaja kukumbushwa katika Agano Jipya.
Mathayo 13:14
Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Paulo akaja kuwakumbusha akashindwa.
Tito 1:12
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.
.................
Hao watu, kwa Neema ya Kristo wachache wao wameijua Kweli.
Matendo ya Mitume 2:11
Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
...............
Sio mimi Brother sio mimi.
"mioyo ya watu hawa imekuwa mizito"
Tokea zama za Kale, zama za Manabii.