Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Nyie mmejaa Majin kuliko dini yeyote maana mwenye mapepomnayapooza na kusema kitu kasema hvi na Hiv kama lin shetani akabembelezwa badala stole, pia Kwa mwamposa waliojaa huko ni waislam na wanaanguka mapepo vibaya mnoo
🤣🤣
Eti kiti anataka maji, dhahabu
Sie hatuna muda, tunayafukuza Ili kae Roho Mtakatifu ndani ya mtu sio majini
 
ISOMEKE Eliya mtishbi Siyo Elizabeth Kama ulivyoandika
 
Kuna majina mengi Sana lakini kuna jina moja tu, lenye mamlaka NAME ABOVE EVERY OTHER NAME

Amenitendea mengi hayahesabiki
 
Yesu
Yesu hakuwahi kuua adui zake, ulipaswa kumuhubiri huyo mganga fundisho kuu la Yesu

"Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri injili....
 
Mathayo 13:41
Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi.

Andiko hili vichwa ngumu kama
FaizaFoxy, kamwe hawawezi kulielewa.
Mwana wa Adamu na Malaika wapi na wapi?

Mathayo 13:10
Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.

Hapa yeyote mwenye ushirika na Majini anatoka Kapa.
 
Yesu alihubiri upendo, ndiyo tofauti yake na Eliya, Eliya aliua manabii wa Baali lakini Yesu akiwa msalabani alisema "Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalolitenda... "

Usimdhihaki FaizaFoxy mfundishe kwa upendo. Hata Paulo kaandika muwaonye wazee kwa heshima
 
Umeniita? Tatizo nini?

Ukitaka kumjuwa Yesu kamsome kwenye Qur'an.
 
Jina lake lilinipatia kazi, amani ya moyo na yote kwa yote roho ya kusamehe na kunijifariji baada ya kuondokewa na mpendwa wangu.

Hivi vitu nina hakika navyo maana baada ya kujitahidi kwa njia nyingine zote na kushindwa kabisa na nikakiri nimeshindwa, nilisikia mahubiri kutoka kwa Mchungaji mmoja hivi, ambae alisema watu wengi wanakosea kuomba unapoomba weka nia ya dhati na mueleze Yesu ombi lako.

Ni kweli baadae, jibu lilipatikana.
 
Jina hili lina nguvu sana , Aidha nakumbuka nilikuwa katika nchi ya vita burundi . Siku moja nilipita maporini , tulikuwa na gari tunatafuta kufika mji mkuu Bujumbura . Askari walisimamisha gari letu na kutaka uhalali wa sisi kuwepo yaani passport na nyaraka zote , wakati huo mimi nilikuwa na kawaida ya kuingia burundi kwa ujirani mwema . Aidha siku hiyo nilipuuzia kwani nilikuwa siendi bujumbura lakini mwenzangu alinishawishi tufike huko na kesho turudi ila tupite njia nyingine .Ghafla tulikutana na wajeda full vyuma . NILIITA JINA LA YESU NIKASEMA BWANA YESU MIMI SISHUKI NIFUNIKE KWA DAMU YAKO !. Hakika ndivyo ilivyokuwa , yaani askari anaangalia ndani ya gari lakini hanioni , anawaambia hamna kitu na nipo kiti cha mbele cha gari aina mchomoko . hakika jina hili lilishangaza watu wengi na wote tuliokuwa nao waliokoka na kumkubali yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yao . wenzangu walipata madhila ya kunyanganywa pesa na viboko vingi sana
 
Ndugu yangu, duniani hapa kuna kundi fulani hata uwapigie ngoma hawawezi kuelewa.

Luka 7:32
Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
...................

Hilo kundi liliongelewa na Manabii wa
Agano la Kale.

Isaya 6:9
Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione.
..............................

Likaja kukumbushwa katika Agano Jipya.

Mathayo 13:14
Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Paulo akaja kuwakumbusha akashindwa.

Tito 1:12
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.
.................

Hao watu, kwa Neema ya Kristo wachache wao wameijua Kweli.

Matendo ya Mitume 2:11
Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
...............

Sio mimi Brother sio mimi.
"mioyo ya watu hawa imekuwa mizito"
Tokea zama za Kale, zama za Manabii.
 
Utofauti uliopo wa kiimani uliweka gap kubwa kati ya Muumba na uumbaji wake japo Muumba wa wote ni mmoja.

Ndo maana sauti (nuru) ikawa inatokea gizani wengi hawakujua ilo giza limetoka wapi kutoka 20:21 na 2korintho 4:6 wasijue ni gap lililokuwapo.

Wengi hawajui kwanini Muumba alisema katika 1korintho 13:1-13 kwamba hata uwe na imani ya kuhamisha milima kama huna upendo hakuna kitu hapo ndo maana akasema yeye ni upendo katika mstari wa 13 ya upendo ndo unaondoa izi tofauti za kiimani.

Muumba wetu sio mwislam wala mkristo wala mbudha na mhindu au rastafarian izo zote zimeletwa na wanadam.
 
Sawa, unaamini kwamba jina la YESU lina nguvu? limekutendea makubwa gani? wasilisha ushuhuda wako ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, unaamini kwamba jina la YESU lina nguvu? limekutendea makubwa gani? wasilisha ushuhuda wako ...

Sent using Jamii Forums mobile app

Yesu alisema mwenywe katika Yohana 17:3 uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli yaani Muumba.

Na katika yohana 4:23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

Na katika 1korintho 15:28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe (Yesu) naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Sasa tumefika kwa Muumba ambaye ni mmoja na wakuabudiwa ni mmoja yaani Muumba.

Waefeso 4:6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

Majira ya Yesu imeshapita.
 
Wewe bado hujamjua Yesu Kristo.

Ngoja nikupe Homework.

Mama wa Nabii Musa alimtupa mtoto wake Musa mtoni kwa kuogopa atachinjwa na Herode.
Binti Farao akamwokota mtoto Musa na kuamua kumlea.

Mama wa Musa alifuatilia tukio lote la mtoto wake Musa kuchukuliwa na Binti Farao.

Kwa mapenzi makubwa ya Mama ya Musa kwa mtoto wake Musa ilibidi Mama wa Musa aende kwa Farao kuomba kazi ya Kijakazi au Housegirl ili amlee mtoto wake Musa.

Naomba unijibu hapa.

1.Familia ya Farao ilimjua Housegirl wao kuwa ni mama yake Musa?

2. Kwanini Mama wa Musa hakujitambulisha kama Mama wa Musa kwa Farao?

3. Je huyo Housegirl wa Farao alipo ongea kwenye familia ya Farao aliongea kama Mama wa Musa au kama Housegirl wa Farao?

4. Tufanye siku ya kwanza ya mama wa Musa kufika kwa Farao na kuomba kazi ya ujakazi, hivi angesema yeye ndiye mama mzazi wa Musa unafikiri nini kingetokea?

5. Kuna mtu kwenye familia ya Farao aligundua kuwa huyo hakuwa mjakazi bali ni mama mzazi wa Musa na hakumwambia mtu yeyote, unafikiri ni kwanini alinyamaza?

6. Ungekuwa wewe kwenye familia ya Farao. Ungeweza kumtambua yule mjakazi kuwa ni mama mzazi wa Musa?

7. Kama wewe ulivyo, ungehitaji nini ili umtambue mama mzazi wa Musa kuwa amejifanya tu kuwa ni Housegirl ili awe karibu na mtoto wake?

Tafakari haya maswali kwa muda kadhaa.
Halafu unijibu kadiri ya uelewa wako.

Nakusikiliza.
 

Kuna kitabu kimeelezea historia ya Yesu kristo zaidi ya vitabu vya injili? Kati ya Kurani na vitabu vya injili vipi ni vitabu vikongwe kwa mujibu wa historia katika uandishi wake?
 
Mnatapeliwa na Wachungaji eti jina la Yesu , yaani hilo sio changa la uso ni mawe ya uso , Yesu mwenyewe kakataza jina lake lisitumiwe nyinyi mnampinga Yesu, ni haki yenu kutapeliwa, Wajinga ndiwo waliwao

Leta kifungu ni kupe vifungu vya Yesu kuwaambia wanafunzi wake watumie Jina lake kupata wokovu.
 

Kutoa tahadhari ni longorongo,ajuza acha unafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…