Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Kwa

Kwani yesu ndio mungu?
 
Huyu anatamka Jesus na mwengine anatamka Yesu, inakuaje tunasema jina lenye miujiza na hali kuna utamkaji tofauti tofauti? Mimi nafikiri kama kuna hiyo miujiza basi haipo kwenye hayo majina bali ni matokeo ya imani za watu wahusika.

Sidhani kama ukitumia neno Mungu kufanya miujiza ndio haitofanyika miujza hadi utamke Yesu au Jesus.
 
Imani ni tokeo la Hisia za MTU, vile anavyoguswa. Ni zao la HISIA. Hisia za mtu hata ziwe nzito kiasi gani, haziwezi kubadilisha chochote ila tu Hesabu sahihi zinapofikiwa.

Utuambie sasa, hiyo ACDs ni nini hasa na inapimwaje? Ikiwezekana kwa mifano.

Kiswahili ni Yesu, English ni Jesus, wengine wanamuita Ruva, nk... Sasa utuambie ni lipi hapo lenye hizo ACDs 100%?
 
Ubishani wa kipuuzi huwa haipendezi..mnaharibu..tuwe wastaarab..

Elezeni miujiza.. na upekee wa Jina la Yesu na wengine wachangie..
 
Yesu kama jina wapo wengi, hata wazungu wapo wanaoitwa Jesus. Mimi namsema Yesu Kristo wa Nazareth, Jesus Christ of Nazareth ndie source ya positive power ana ACDs 💯%.ACDs zako zitapanda zaidi toka 1% kuelekea 100 kwa kadri jinsi unavyojitoa kutumika na Yesu Kristo.

ACD s ni nini, ACDs ni kifaa kitumikacho kupima nguvu ya imani uliyonayo. Inapima vitu vinne.
1.Nguvu ya imani uliyonayo
2.Udhaifu wa kiimani ulionao
3.Inapima saporter company, saporter company ni nani wapo nyuma yako wanaokusaidia kukuza imani yako
4.mamlaka ya imani

Mfano mchawi anapotaka kukuroga upima nguvu ya imani uliyonayo,kabla ajafanya maamuzi kama akupige kombora au aachane na wewe kama nguvu yako ni kubwa ataamua yeye aachane na wewe akijua atapigwa au aongeze nguvu toka kwa mkuu wa wachawi wa mtaa, wilaya, mkoa, nchi, au akuandikie hati ya mashtaka kisha aitume kuzimu kwa majemedari sita wa lusifa. Unaweza ukapigwa au ukawapiga hapa sasa ni nguvu ya imani, Ndo maana ya vita vya kiroho yaani unapambana na nguvu za giza. So kifaa kinachotumika kupima nguvu ya imani either ya Mungu au ya shetani uliyonayo dhidi ya mashindano wako kinaitwa ACDs.
Kama una nguvu ya Mungu hata ukifa kaburi lako mchawi, jini, shetani achezei wala kusogea linakuwa na moto zaidi ya gas masaa 24.
 
Nikuulize moja kwa moja labda, je hicho kifaa ni cha kufikirika au kinashikika physically? Kama kinashikika, tuambie kimetengenezwa wapi na nani?

Accuracy yake ipoje?

 
Hizo ACD ni vipimo vya Kanisa lenu au biblia yenu ?
ACDs ni kipimo cha kiroho kinapima imani ya mtu dhidi ya imani yake.
Ni SAwa na tester ya umeme.
Mfano huyu ni Mkristo nguvu yake ya imani ni asilimia 3,4,10,50,70,nk.
Au huyu ni mchawi nguvu yake ya uchawi ni asilimia 1,2,4,10,30.
Hizi ni elimu za mambo ya kiroho yaani ulimwengu usioonekana.
Mfano ajent/mchawi akitaka kumuangusha mtumishi wa Mungu utumia kifaa kiitwacho ACDs ana pima imani yake then analinganisha na nguvu ya uchawi alionao kama unaweza mdhuru mtumishi wa Mungu akipima akaona yule mtumishi nguvu yake ya imani ni ndogo anamtumia madhaifu wanatumia zaidi wanawake warembo,au wanaingizia tamaa ya ngono au tamaa ya pesa kisha mchungaji anaswa kwenye eneo hilo anakuwa ameangushwa.
So ACDs ni SAwa na tester,ya kumtest mtu kabla ya kumpiga kombora. Hata wachawi nao uogopa kifo au madhara dhidi ya wapinzani wao. So ni lzm wafanye vipimo kwanza kabla awajashambulia, so ukiwa dhaifu huna Yesu wanakuchezea watakavyo.
 
Nikuulize moja kwa moja labda, je hicho kifaa ni cha kufikirika au kinashikika physically? Kama kinashikika, tuambie kimetengenezwa wapi na nani?

Accuracy yake ipoje?
Mambo ya kiroho huwezi yashika kwenye ulimwengu wa mwili.Ni hadi uingie kwenye ulimwengu wa kiroho, ulimwengu usioonekana.
Wachawi, waganga wanavyo, watu wa Mungu wao Wana macho ya kiroho.
 

[emoji22][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1430][emoji1430][emoji1430] wacha nicheke Mbona tunapata manufaa kwa shetani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yesu wa Nazareti, the same guy Mimi nikiamua kumuita Juma Bakari au Potu Pato, atapungukiwa nini? Je, kwa MTU huyo ACDs ingetoa majibu sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…