Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

ACDs ni kipimo cha kiroho kinapima imani ya mtu dhidi ya imani yake.
Ni SAwa na tester ya umeme.
Mfano huyu ni Mkristo nguvu yake ya imani ni asilimia 3,4,10,50,70,nk.
Au huyu ni mchawi nguvu yake ya uchawi ni asilimia 1,2,4,10,30.
Hizi ni elimu za mambo ya kiroho yaani ulimwengu usioonekana.
Mfano ajent/mchawi akitaka kumuangusha mtumishi wa Mungu utumia kifaa kiitwacho ACDs ana pima imani yake then analinganisha na nguvu ya uchawi alionao kama unaweza mdhuru mtumishi wa Mungu akipima akaona yule mtumishi nguvu yake ya imani ni ndogo anamtumia madhaifu wanatumia zaidi wanawake warembo,au wanaingizia tamaa ya ngono au tamaa ya pesa kisha mchungaji anaswa kwenye eneo hilo anakuwa ameangushwa.
So ACDs ni SAwa na tester,ya kumtest mtu kabla ya kumpiga kombora. Hata wachawi nao uogopa kifo au madhara dhidi ya wapinzani wao. So ni lzm wafanye vipimo kwanza kabla awajashambulia, so ukiwa dhaifu huna Yesu wanakuchezea watakavyo.

Kipimo hicho kilianza kutumiwa wapi ? Kwenye biblia ipi utakikuta?
 
Kama yupo kila mahali, kwanini asiungane na hao wanadamu yeye mwenyewe pasipo kutumia mawakala?
Kitambo tu mbona ameungana nao kwa kuwatumia malaika zake waovu Ili kuwaingia wanadamu watende matendo maovu Ili kumuabudu.
 
Yesu wa Nazareti, the same guy Mimi nikiamua kumuita Juma Bakari au Potu Pato, atapungukiwa nini? Je, kwa MTU huyo ACDs ingetoa majibu sawa?
Mwanadamu hana msaada wowote kiroho kama ukimtumainia na hawezi leta matokeo yeyeto.
 
Ye
Mwanadamu hana msaada wowote kiroho kama ukimtumainia na hawezi leta matokeo yeyeto.
Yesu akiitwa Dimoso, anabadikika nini?

Kama binadamu hawezi kutumainiwa, unawezaje kuitumaini NOMINO/Sauti dhania na kutaraji matokeo chanya.

Roho haina mipaka ya majina wala nafasi, wala muda. Roho ni Ukamilifu wakati wore. Amkeni.
 
Kitambo tu mbona ameungana nao kwa kuwatumia malaika zake waovu Ili kuwaingia wanadamu watende matendo maovu Ili kumuabudu.
Kwanini atume malaika, kwanini asiwaingie yeye mwenyewe?
 
Ye

Yesu akiitwa Dimoso, anabadikika nini?

Kama binadamu hawezi kutumainiwa, unawezaje kuitumaini NOMINO/Sauti dhania na kutaraji matokeo chanya.

Roho haina mipaka ya majina wala nafasi, wala muda. Roho ni Ukamilifu wakati wore. Amkeni.
Sababu ipo nguvu kuu ya utendaji ndani ya jina la Yesu. Hayo majina mengine hayana nguvu ya kutenda chochote.
 
Uchawi ni nini? Ulishushwa kutoka wapi? Nani aliushusha na kwanini?
Uchawi ni hasi kutenda uhalibifu.Ulishushwa na majini toka kwa shetani malaika hao waovu wanaoitwa maharuta wa maruti,lengo kuu Ili kupunguza uwezo wa kufikiri wa mwanadamu aache kutumia akili aliyopewa na Mwenyezi Mungu amtegemee shetani,fanya tafiti mchawi au mshirikina huwa na uwezo Mdogo Sana wa kufikiri.Thus wazungu baada ya kuwaua wachawi wakapata Jamii inayofikiri vizuri na wakawa na maendeleo makubwa Sana.
 
Tangu uliposhushwa uchawi duniani na majini.
Biblia haijaandika kila kitu visingetosha

Kwa hivyo hivyo vipimo walivianzisha wazee wa kanisa lako ?
Unaongelea biblia ipi? KJV, QJV, NIV au biblia zaidi ya 1000 tofauti ?
 
Kwa hivyo hivyo vipimo walivianzisha wazee wa kanisa lako ?
Unaongelea biblia ipi? KJV, QJV, NIV au biblia zaidi ya 1000 tofauti ?
Sio vipimo vya kanisa,hivi vipo hata kabla ya uwepo wa kanisa.Ungekuwa na elimu ya falaki ungeelewa
 
Ni muhimu watu mjue tofauti ya Mkristo na mtu mwenye jina la kikristo au mtu anayeenda kanisani.Siyo watu wote wanaoenda kanisani ni Wakristo mbele za Mungu ,wanaweza wakawa wote ni Wakristo mbele ya wanadamu lakini mbele za Mungu ikawa tofauti.Wakristo wanapatikana katika kusanyiko linalokutana kanisani na ninaposema kanisa siyo kila kanisa ,ninaongelea kanisa linalofundisha mafundisho sahihi kwa mujibu wa Biblia takatifu.Kwa hiyo kama kuna mtu anamiliki Bar,au ni Changudoa huyo ni wale wenye majina ya Kikristo lakini siyo wakristo.Hapa napo kuna somo na kuna kutofautiana kwani kuna mtu moja "anajiita" mtumishi wa mungu alilewa,na video zikasambaa,baadaye akahojiwa redioni kama Kunywa pombe ni dhambi akajibu " inategemeana na kanisa".Kwa hiyo inawezekana kuna makanisa kumiliki Bar siyo shida that is why tunasisitiza watu wasome Biblia waijue kweli nayo kweli itawaweka huru.
Kwa sababu kuna machangudoa wana majina ya Kikristo hii haimanishi ukristo unaruhusu uchangu doa,ukija hivyo nitakuuliza dini yako inaruhusu Bongo fleva?Mbona tunawaimbaji wengi na wakubwa wa dini yako?Mbona mnamijadala kama ni sahihi au siyo sahihi kupokea nyumba ya ibada iliyojengwa na msanii wa Bongo fleva?(concern kubwa hapa ni njia ambayo pesa zimepatikana ,je ni halal au halamu?).Kwa hiyo kuna maswali mengine mnauliza ,mnatusaidia kuwajua ni watu wa aina gani na uelewa wenu juu ya haya mambo ukoje.
Unaleta hoja ya kuna ombaomba wengi wakristo,hatuwasaidii watu kwa sababu ni wakristo tunamsaidia mtu yeyote ambaye ni muhitaji,Ukristo haufundishi ubaguzi,kama kuna mkristo unamsaidia mtu kwa sababu ni mkristo una shida.Huyo ambaye leo siyo mkristo ni mkristo wa mwaka kesho au miaka kumi ijayo.

Kuna vituko vingi sana vinaendelea mtumishi mmoja baada ya watu kukanyagana na kufa alihojiwa akaulizwa atoe maoni yake "mtumishi huyu akasema hata kipindi cha Yesu watu walikanyagana" alichosahau ni kwamba ni kweli kwa Yesu watu walikanyagana lakini hakuna aliyekufa.Lakini huku walikanyagana na kufa,siyo wote mtanielewa kuna kitu chakujifunza na sitaki mniulize.
Ukiisoma Biblia na kujua jinsi Mungu anavyotenda kazi utaelewa,ukiisoma Biblia ili upate kuikosoa au na wewe upate kamstari kakuja hapa kupoteza watu haitakusaidia.Mleta mada alileta mada nzuri watu washuhudia nini jina la Yesu limewasaidia lakini watu wametoka kwenye lengo la mleta mada.Huu pia tunaweza ita ni uchanga,"failure to pay attention to details".
Sasa naomba kwa wakati wako fuatilia Mkristo ni mtu wa aina gani? Labda kwa ufupi tu nigusie ya Kwamba Mkristo ni mtu yeyote anayeamaini katika mafundisho ya Yesu Kristo na mitume wake.Anatakiwa kuamini katika Agano la kale na Agano jipya,anatakiwa kuamini ya kwamba Yesu ndiyo njia pekee ya kweli na uzima.Huwezi kuingia mbingunii la kupitia kwa Yesu Kristo.Kwa kadri atakavyojifunza atajua ya kwamba anatakiwa kuepuka dhambi na kuishi maisha matakatifu na kufuata mafundisho kwa mujibu wa Biblia takatifu.
Siyo kila kanisa linalotamka au kufanya miujiza kwa jina la Yesu ni kanisa la kweli la Kristo,kwa kuwa jina la Yesu ndilo jina pekee tulilopewa,jina lenye uwezo kama likitumiwa na mtu sahihi?(siyo kila mtu) lakini pia shetani amepandikiza watu wanatumia jina hilo na miujiza inatokea(tuelewane hapa hata kama ni Jina la Yesu limetamkwa ila siyo Yesu anayetenda hiyo miujiza) .The Devil is mighty,but God is almighty,kama unadhani shetani hana uwezo wa kufanya miujiza kasome biblia yako vizuri.Watoto wachanga wanadhani kila muujiza unatoka kwa Mungu kwa kuwa hawayasomi maandiko hawajui hata Farao aliita wachawi na wenye akili wakageuza fimbo kuwa nyoka?Je huu haukuwa muujiza?Hawajui katika kitabu cha Matendo ya mitume kulikuwa na mchawi ila watu walimwita "mtumishi wa mungu"?
Kuna vitu hata ukiandika haviwezi kumsaidia mtu kwani kutokana na jinsi mtu huyo alivyokamatwa huwezi mbadilisha kwa ushawishi wako wa kuandia hapa JF,Neema ya Mungu inahitajika.
Niwape pole ndugu zangu manaoleta maandiko na kujaribu kuuchallenge ukristo,siwazuuii kwani ni haki yenu ila nawahurumia kwani najua waliowapoteza ni akina nani?Nanyi makakubali kupotezwa kwa hoja za kibinadamu na wingi wa maneno .Hata mimi walitaka kunipoteza miaka ya 90 lakini namshukuru Mungu alinifunulia technique zao kwa hiyo huwa nawasikiliza tu na kuwahurumia.
"Mambo ya imani kwa wasio amini ni upuuzi",hapa hata ulete ushuhuda gani kwa asiye amini unatwanga maji kwenye kinu,kuna hatua za kuanza na mtu huyu.Haiwezekani leo wewe mtoto mchanga tukupe chakula kigumu tutasababisha matatizo.Shida ya mitandao watu wako beginner level lakini wanauliza maswali ya Advanced level,majibu yakitolewa wanazidi kuchanganyikiwa.Kwanini?Kuna mafundisho yalitakiwa kutangulia kabla ya hili.
Nimalize tu kwa kusema Jina la Yesu lina nguvu na uwezo,yapo majina mengi lakini unapotaja jina la Yesu mijadala huwa mikuwa?Yesu siyo Mungu,Yesu ni nabii Issa,Yesu na Nabii Issa ni kitu kimoja?
Siyo kila mtu anaweza litaja jina la Yesu na kikatokea kitu labda iwe neema ya Mungu tu kwa sababu ya kutokujua kwako anakusaidia ila ukikomaa utaelewa.
Kuna majina mengi yapo lakini jina hili truly ni la tofauti,hata nikielezea kuna watu hamuwezi kunielewa mpaka tuanzie na masomo ya mwanzo(elementary lessons).Unaweza ukawa na umri wa 40+,unaweza ukawa umesoma mpaka phd lakini usiwe na elimu ya haya mambo ya dini.Kuwa na elimu ya dunia haikufanyi uwe unaufahamu na elimu ya mambo ya Mungu.Mungu anahitaji sana mtu mtii,ndiyo sababu huweza kumtumia mtu yeyote ambaye anamtii.

Nisisitiza tena Mungu anavyotutazama sisi wanadamu si sawa na mwanadamu anavyomtazama mwanadamu mwenzake.Mungu anachunguza moyo/mawazo ya mtu,wanadamu wanaaangalia muonekano wa nje na tabia zinazo onekana.Kwa hiyo Yesu aliposema ondokeni kwangu siwajui,hakuwa anawaambia Wakristo wote bali alikuwa anaongea na watu ambao walipokuwa duniani waliingia makanisani,wakajiita Wakristo lakini maisha yao hayakuwa matakatifu mbele za Mungu.Sasa kwa bahati mbaya sana wapotoshaji wamewapotosha nanyi mmekubali.
Mambo mengine ni mazito hatuwezi sema hapa hazarani ili hali isiharibike,ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia ucheze.Usitake kuyajua mambo ya Wakristo na Mungu wao anavyowatendea wakati uko nje,ingia ndania yeye ni Mungu wa wote wenye mwili hana ubaguzi.Angalizo: Siyo kila kanisa linapotajwa Jina la Yesu au injili kuhubiliwa ni kanisa sahihi,hizi ni nyakati za mwisho kuwa makini na sehemu ya kwenda.
Ushauri wangu hata kama siyo Mkristo soma Biblia utashangaa kwa mambo utakayoweza kujifunza,Biblia imeongelea mambo mengi sana ya maisha yetu ya kila siku,uongozi,familia,vita,upelelezi,n.k.Una swali?Kuna kitu unataka kujua njoo PM.
Regards
Aqua
 
Shetani yupo KILA mahali, pia kupitia mawakala wake duniani unaweza mpata.
Makao ya shetani ni kuzimu
Kama yupo kwanini mpaka wakala wake? Tupe anakopatikana tukajue ukweli. Kila jambo anasingiziwa shetani kwakua haonekani!!
 
Back
Top Bottom