Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Anayesema maneno hayo anaendelea kusema

Warumi 7

14. Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi.

15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya.
Hoja yako ni ipi ?
Wewe unasema nini ?
 
God is real, and his powers is all around us. Utaamini the day uta experience mwenyewe
 
MIZANI YA IMANI YA WAKRISTO

Bwana Yesu Kristo alieleza mizani na alama za imani kama ifuatavyo:

1. Mkiwa na imani ya punje ya haridali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa nenda kule, nao utaondoka; wala halitakuwapo neno lisilowezekana kwenu. (Mathayo17:20; 21:21; Marko 11:22-23, 9:23, Luka 17:6, 12, 13).

2. Bwana akasema: “Kama mngekua na imani kiasi cha chembe ya haridali mngeuambia mkuyu huu, ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” (Luka 17:7).

3. Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na imani , msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, ngo'ka ukatupwe baharini, litatendeka. na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Mathayo 21:21-22)

4. Amin, Amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwani mimi naenda kwa Baba. (Yohana 14:12-13).

5. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa. (Yohana 15:7).

6. Tena nawaambia, wawili wenu mtakapopatana duniani katika jambo lolote watakalo liomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. (Mathayo 7:3-12).

7. Ombeni nanyi mtapewa.... (Mathayo 7:3-12).


Katika mizani hii ya imani ya Wakristo, tumejua kwamba Mkristo atatambulika kwa alama zilizotajwa hapo juu.

Tena hizi ni alama za imani ndogo sana ya chembe ya haridali. Lakini kama Mkristo atakuwa na imani kubwa ataweza kuonesha miujiza mikubwa zaidi.

Vilevile Mkristo mwenye imani ni yule ambaye ataweza kuonesha miujiza na hasa sawa na ya Bwana Yesu bali mikubwa zaidi kuliko yake.

Sasa kwanza tutafute miujiza ya Bwana Yesu katika Biblia, tumeona baadhi yao kama ifuatavyo:

1. Kuponya wagonjwa (Mathayo 8:16, 9:22, na 15:21).

2. Kuponya walemavu (Mathayo 8:1-3).

3. Kuponya mabubu. (Mathayo 9:3-7; 12-22).

4. Kuponya mwenye kupooza upande mmoja (kiarusi) (Mathayo 8:5-13. 9:1-7, 12:22).

5. Kumponya mwenye kifafa. (Mathayo 17:14-19).

6. Kuponya mkono wenye ukoma. (Mathayo 12:15).

7. Kuponya mgongo uliopinda (Kibyongo) (Luka 13:10).

8. Kuwafufua wafu. (Mathayo 9:24).

9. Kugeuza maji kuwa pombe. (Yohana 2:1-9).

10. Chakula kidogo kitoshe watu elfu tano.(Mathayo 14:13-21).

11. Kutembea juu ya maji. (Mathayo 14:22-23).

12. Kuzuia tufani . ( Mathayo 8:23-33).

Hapa nimetoa baadhi ya mifano tu ya miujiza ya Bwana Yesu.

Kama Wakristo hamuwezi kuonesha miujiza ya aina hii au alama ya imani yao sawa na Biblia, basi
mambo mawili yanathibitika.

A. Bwana Yesu pia hakuonesha mujiza wowote bali ni hadithi za kutungwa tu zisizo na ukweli ndani yake.

B. Siku hizi Mkristo yeyote hana imani sawa na chembe ya haridali, bali wote mumeshapotea tayari na hamna alama au dalili yoyote ya imani.

Hali hizi zote mbili ni mbaya sana na za kutisha.

Na dawa yake ni moja tu kwamba muingie katika dini ya Mwenyezi Mungu, ISLAM, baada ya kutambua umoja wa Mungu na Mtume Muhammad s.a.w. bila hivyo mtaendelea kufedheheka siku hadi siku.


TAMBIO:

Ninawapa Wakristo tambio (challenge) kwamba kama wanayo imani sawa na chembe ya haridali, watuoneshe miujiza iliyotajwa hapo juu. Mkristo mmoja au wawili au wajumuike wote, tunataka kuona miujiza tu ya imani yao, hata Pope au wachungaji wenu wajitokeze.
Yesu hakufanya muujiza wa kugeuza maji kuwa pombe. Aligeuza maji kuwa divai. Divai ni maji ya zabibu ambayo bado hayajachachushwa kutengenza pombe (alcohol). Ni sawa sawa na wewe ukamue maji ya zabibu (juice ya zabibu) halafu uite hayo maji kuwa ni pombe. Kuna tofauti kati ya Mvinyo (wine or grape alcohol) na divai(grape juice).
 
Nilikuwa na interview kwenye taasisi moja kubwa ya umma, hapa nchini; mara ghafla mida ya saa 9 usiku nikiwa usingizini nikasikia sauti ikiniamsha amka uombe maana Kristo amekusudia kukupa hii kazi, hitaji lako la kazi Mungu amelisikia na anakwenda kukutendea muujiza, amka uombe, usiache kuomba

Kweli nikaamka, nikakuta kwenye radio kuna maombi yanaendelea ya kuombea watu wanaokwenda kwenye interview siku inayofuata

Nikafuatilia hayo maombi hadi alfajiri yalipokwisha

Nilikwenda kwenye hiyo interview najiamini sana; nilishinda hiyo interview bila rabsha yoyote, kwenye Oral interview niliulizwa maswali mawili tu...nieleze nitafanya nini kipya nikipewa hiyo kazi na swali la pili ningependa nilipwe mshahara kiasi gani..

Mwaka wa 4 huu sasa niko kazini, maisha yamebadilika; JINA LA KRISTO YESU NA LIHIMIDIWE!
Ameeen!
 
Hayo majina mengine hayana nguvu ACDs zake zipo chini.ACDs ni kipimo kipimacho nguvu ya imani.
*Jesus anayo ACDs 100%
*Shetani anayo ACDs 40%
*Majemedari sita wa shetani wanayo 3 hawa ni wasaidizi wakuu wa shetani.
*Jini anayo 2.5
*Mwanadamu yeyeto anayo ACDs 1
*Wanyama wanayo 0.5.
Mwanadamu ACDs yake inapanda kadri ya upande anaoutumikia. S

So attack yeyeto ya kiroho itategemea na nguvu uliyojiunganisha nayo.
Kwann tuna believe in Jesus sababu anayo ACDs 100 so ukijiconnect nae Hakuna cha jini, shetani, mzimu, mchawi sijui takataka gani itakuweza sababu unapokea nguvu direct toka kwa Jesus Power.
Kirefu cha ACD ni nini? Na umepata wapi hayo?
 
Yesu hakufanya muujiza wa kugeuza maji kuwa pombe. Aligeuza maji kuwa divai. Divai ni maji ya zabibu ambayo bado hayajachachushwa kutengenza pombe (alcohol). Ni sawa sawa na wewe ukamue maji ya zabibu (juice ya zabibu) halafu uite hayo maji kuwa ni pombe. Kuna tofauti kati ya Mvinyo (wine or grape alcohol) na divai(grape juice).

Sawa kama wewe kweli ni mwenye imani ya ukristo wenye uzito wa chembe ya hardali , tugeuzie maji kuwa soda 😛 😛
 
Back
Top Bottom