Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Leo tunalewa wapi
 
Ah! Bella ciao Bella ciao Bella ciao.
Kama umeangalia Lacasa de Papel... Kuna nyimbo anapenda kuuimba Berlin na Professor....

Bella ciao maana yake ni kwaheri mrembo, original ya huu wimbo ni wimbo wa mapinduzi katika nchi ya ITALIA
 
Mimi ni Mwandishi wa kujitegemea,naandika nakala mbalimbali....
 
Maisha nikamari, I lose some & I win some.
I can keep the poker face so well even when the stakes are high
 
wakati nikiwa advance katika shule moja iliyopo kandokando ya ziwa kubw hapa nchini sasa siku tukiwa zetu beach tunafua na washkaji zangu basi nilikuwa na taulo moja hv la kizamani kwa rangi na michoro ake asa nilikuwa nmelivaa huku nikiwa kifua wazi basi kutokana na muonekano fulani wa mwili wangu basi jamaa angu akasema naonekana kama yule muigizaji wa movie ya spartacus ..basi mpk leo wamenizoeza hv mpk leo naitwa hv basi nikaona sio ishu nikilitumia humu jf
 
Oh nimekuelewa vizuri.
Akhsante kwa maelekezo,nimejifunza mengi.
Siku bongo kukiwa halueleweki Sana tutajilipua kwenda huko hata kazi ya usafi tu inatosha.
 
Oh nimekuelewa vizuri.
Akhsante kwa maelekezo,nimejifunza mengi.
Siku bongo kukiwa halueleweki Sana tutajilipua kwenda huko hata kazi ya usafi tu inatosha.
Hahaa...usiniache plzzzz...tukaanzishe maisha yetu mapya..[emoji4][emoji4]
 
Leo nalewa nyumban kwa kuibia wamenipa vidonge wameniambia nisinywe na huyu mdada hapa yupo hapa ananisaidia saidia mambo ya home ni jirani yangu

anapiga patrol kuchek Kama nina mzgo ila nimetia konyag zangu kweny kidumu cha Kilimanjaro bado hajagundua anajua nakunywa maji

Haya mambo ya kufatiliana haya ngoja nimkaushie tu maana ananiambia akiniona nalewa atamwambia baba mwenye nyumba mi mgonjwa nalewa ntamletea murder case
Leo tunalewa wapi
 
Sawasawa mzee, mdogomdogo
 
Hivi kaka yangu unadhani pombe zitabadilisha uhalisia wa Mambo yaliyotokea!???
Ukweli Ni kwamba pombe zitakuchakaza tu, sometimes ukilewa Sana unakuwa Kama mjinga km jinsi ulivyosema kwamba unaweza lala bar,utatapika,,unahatarisha afya yako...
Huoni Kama Ni hatari kunywa wakati mgonjwa!??. huoni km inaweza kukusababishia madhara au kifo kabisa?.
-Vipi baada ya kunywa mawazo yameisha!.?
-Uhalisia wa Mambo umebadilika!?
Kuna faida gani katika pombe!??
Ukifikiria haya utajua ukweli kwamba uhalisia wa Mambo uko pale pale...
There is no way you can change your past my brother.. you have to accept it without any regret..
Now you have to handle your present with all your confidence.. don't allow your past to destruct your present and your future.

Kwanini usiachane na hayo maisha ya ulevi ambayo hayana faida yoyote, nadhani hata wewe umeona hayana faida,, Zaidi vitu vimebaki Kama vilivyotokea....
Natamani Sana ubadilike., nitafurahi Sana endapo utabadilika,,je upo tayari??
Tafakari tena,, maisha yako kiujumla..kweli kote ulikotoka,ndoto zako, Jinsi ulivyo fight huko nyuma,elimu yako..unataka vipite bure!??
Hukuzaliwa uishi hivi unavyoishi.
Hukuzaliwa uumie.
Tafakari tena
Yupo rafiki mmoja,mwaminifu,amejaa kweli.
MLEVi Mmoja
 
Leave him alone!
 
Nilipokuwa sumbawanga nikiishi kwa dada yangu wakati huo.
Alikuwa na watoto watatu wote wakiume walikuwa wananipenda sana nami niliwapenda haswa huyu wa mwisho alinipenda hadi asiponiona chakula hawezi kula.Nliwalea hivo kwasababu michezo na taaluma vyote nilivyopenda mimi toka udogoni hawa madogo nilitaka wapite humohumo maana walinijua mimi ni mjomba wao ambae kama baba na mama wakiwa hawapo wanajua mi nitawafanyia kila wanachotakiwa kupatiwa.Huyu mtoto wa mwsho akiwa na miaka minne alikuwa akiona namwandalia msosi ananisifia sa asa kuna siku wakati natembeatembea nae huku naongea nae akaanza kusema kwa kuimba ilihali sijawahi msikia wala kusikia sehemu yoyote wakisema hli neno "FOCAL MANDUNDA"akawa anaimba nikamsikiliza nikalipenda nikaanza mfatisha kuimba..focal mandundaa... ooh!yeah!!kumbe focal mandundaaa..bas tukifurahi tukawa tunaimba huo wimbo hata nilipoondoka kwa kutoroka lakini yule mtoto nilipata taarifa zake kwamba usiku alikuwa halali kwasababu mimi hanioni.Kwahyo hilo jina ninamuenzi mtoto wa dada yangu aliyeanzisha kupitia wimbo aliotunga.Namkumbuka sana.Mashabiki wa soka tuelewane kwamba hilo jina sijapunguza au kuongeza herufi kupitia kwa kipa wa simba aitwaye said mohamed maarufu kama "ndunda".
 
Kwa sababu .nilikuwa naona kila mtu na avatar yake vinanivhanganya.nikaamua Mimi niwe mtu flani tu .yani mi mwenyewe hadi sasa sielewi mtu flani yupi sasa na yupo wapi ila mtu flani naipenda sana Jf ndo ilinifanya nijiite mtu flani
Bro Maxence Appreciate you Blood
#Mtu_Flani
 
Ule wimbo wa 'Nini dhambi kwa mwenye dhiki' ndio wimbo wangu bora wa rap wa wakati wote mwimbaji akiwa Faza Nelly na crew nzima ya Xplastaz.
Baada ya kifo chake nikaamua kumuenzi kwa kutumia jina lake na picha yake humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…