Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Nilikula hela ya ada kama laki 2 na ikafika tarehe za end of semester uongozi wa chuo ukatukatalia kuwa asielipa ada hafanyi paper zimebaki siku kama tatu tufanye nilikuwa sins raha laki 2 naipata wapi nikasema ngoja niombe mungu kwa siku 1 moja anisaidie nipate hela pindi nikiomba watu wanipe weee siku ya kwanza kila nikiomba kwa mtu hana siku ya pili hola daa nikasema ngoja niombe kwa shetani nikasema shetani nisaidie nibet nile nikabet mkeka nikala laki 5 daaa toka siku hiyo nikaamini shetani ukimuomba anakupa nikajitiita Iblis bin Shetan maana aliniokoa kweli
 
Mlongoooo nimechekaaaaaaa sanaaaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
🤣🤣🤣 dah mkuu nimeona tu jina nimecheka mno na kufungua ndani ndo hadi machozi yametoka. shukrani sana kwa kushare.
 
Es = S - comes from initial name of mine
Mari - last spellings kutoka kwa jina la ukoo

All those make Esmari
 
Daah sio poa aseeh
 
(Lucky) (line)
Lucky= nilipewa na doctor, mama anasema wakati wa kuzaliwa nilitanguliza miguu, it was complicated kujifungua na hakukuwepo mambo ya operation. Maness wa kawaida wote walitoka ikalazimika kuja ma dr kama 5 hivi, (hiyo sehemu huduma za afya zipogo kitambo sio kama huku) hii ishu ya kutanguliza miguu mikono inabaki nyuma mara uje mmoja mwingine ubaki ilikuwa nadra sana. Dr moja alitoka kwenda kufata kifaa wakati wengine wanaendelea anarudi ndo akakuta nishatoka hapo hapo akatoa hilo jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…