Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?


Nakumbuka enzi hizo moja ya washairi washawasha alikuwepo, kweli wewe mwana wa washawasha ulimlipa baba yako kwa ushairi
 
Jina langu nimelichukua kama lilivyo kwa pioneer wa hydrogren bomb-so i have self efficacy of producing new ideas ambazo in one way or another ztaleta mafaniko kwa wale wote ambao watafanyia kaz kile ninachosema,japokuwa kutakuwa na wanaonipnga-but I will keep saying for anything that seems to be right for me to say just as Edward Teller alivokuwa anafanya-SO THIS NAME GIVE ME POWER TO FEEL MYSELF KAMA NINA POTENTIAL NYINGI AMBAZO ITAKUWA ZAMBI KAMA SITAZISHARE NA WENZANGU HAPA JAMVINI NA KWINGINEKO-thats all
 
nilijiunga mwaka 2006 nikitumia ID ya kingereza, baadaye mwaka jana niliamua kubadili na kujiita IHOLOMELA, jina hili ni la mtu maarufu sana kwetu Igunga..alikuwa manju wa ngoma za kienyeji. Namkubali sana jamaa.
 
RURAL SWAGGA,,,,. Mtoto wa mkulima niliyesoma primary school na kulipa ada ya jengo Tsh 800,Upe1000,nyingine nimesahau!!! Nilibeba mzigo wa kuni na Galoni yangu ya maji ya Lita 3 kwenda shule,Niliyekuwa nawahi kuamka na kwenda kushika namba shule na kurudi nyumbani kukamua maziwa ya ngombe na kufagia uwanja.Niliyeshika namba 1 darasani na sikuwahi kuvaa kiatu mpaka siku ya mtihani wa Darasa la 7.Niliondokana na Mateso yote ya kijijini pale nilipochaguliwa shule ya Vipaji Maalum [ELBORU] na mpaka leo ninaendelea vizuri na Maisha Yangu,Nakula Bata Ndefu sanaaaaaaaaa,,,,
 
Habari yako ndugu tanmo
 
Mimi niliwahi kufanya kazi na wale wanaotoka kuleeee mbaliiiiii, e-mail address ya kampuni password yake ilikuwa ZARATUSTRA! Hivyo kwa kumbukumbu ya wale jamaa na kampuni yetu iliyosambaratishwa, ndo nikaamua niwe natumia jina hili, ingawa hadi leo sijui maana ya neno hilo!!
 
The Farmer, Kama jina linavyo jieleza...Ni mkulima wa kawaida...Ila kutokana na hizi sera za kilimo kwanza nanyemelea fingu fulani ili ni upgrade shughuli zangu.

The Farmer=Mkulima...
 
Tatu bila, wamebana wameachia. Nimeupenda sana huo wimbo a bongo fleva. Nikiukumbuka hua unanipa hali sana ktk kazi zangu,hasa ninapokua natumia kitarakishi.

Mambo ya Juma Nature POA
 

Basi miye nilifikiri una mdogo wako anaitwa Lende, kumbe ni sehemu! Ahsante sana Mkuu.

 
TzPride==kuna mizungu ilikuwa ikipenda kunipachika hilo jina kiutani tukiwa ofisini, hasa kama nikiwasemea mbovu wakati wanaikandia nchi yangu....utawasikia ..mmh Tz pride! Nina matatizo ya kutomvumilia foreigner akiisaga nchi yangu kwa dharau.

nimependa.
 

ha ha ha!
Hiyo technique yenu ya wizi ni noma.
 
Brandon ni jina la first born wangu, i have special feelings for him maana thru him nimepata experience nyingi sana hapa duniani nzuri sana na mbaya sanaaa.
 
Quimby_joey ni majina yangu halisi ukiyageuza. hili jina quimby ni jina la ukoo wetu huko kaskazini ingawa katika kiswahili halitamkwi hivyo, ni jina kubwa kwenye ukoo wetu na halipatikani kwenye koo yoyote au kabila lolote lingine tz. Nilipigwa na butwaa wakati naangalia katuni za TOM & JERRY baada ya kuona Director/ Producer wake anaitwa Joe Quimby (kwa wapenzi wa katuni za TOM & JERRY bila shaka wanalifahamu jina hili), yaani tunafanana majina yote mawili na huyu jamaa.

Wakati najiunga JF last year karibu majina matatu hivi ya mwanzo niliyochagua kujisajili nikaambiwa tayari kuna watu wanatumia, hivyo nikaona nitumie jina langu halisi kama ID yangu humu, ndio nikachagua kuliweka katika namna hiyo.
 
Hakuna njia ya kubadili jina hapa JF.

hakuna njia nyingine ispokuwa kuwaomba idhini Mods wao ndio wenye mamlaka ya ama kukukubalia la kukukatalia. Inatakiwa uwe na sababu za msingi kuweza kuwashawishi
 
Mpui Lyazumbi, Ni majina ya maeneo wanakotoka wazazi wangu- Baba anatoka Mpui, Mama anatoka Lyazumbi. Maeneo haya ni maarufu sana katika barabara kuu itokayo Tunduma kwenda Mpanda via Sumbawanga, kwa sasa barabara hiyo inaboreshwa katika kiwango cha lami-uhuru kwa watu wa Rukwa. Rukwa - RUKA.(Mwashipusa kalesaaa)
 
Womtindo was a name given to my daughter by her cousin. she was very young by then, the cousin liked her and called her Womtindo meaning Pretty and Trendy. She is still young, I hope she will live her name. I like the name.
 
Hii thread nimewahi kuisoma siku za nyuma sana, lakini bado naifurahia kuisoma. Majina mengine huku asili na maana yake ni burudani tosha.
 
Njowepo = nami niseme/niseme/naweza sema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…