Diehard
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 470
- 356
Jina la Funzadume nilijipa mwenyewe baada ya mzee wangu kutunga shairi na kuniomba nimpelekee radio Tanzania kipindi hicho ili lisomwe kipindi cha mashairi, ktk jina lake kule chini aliweka aka Washawasha sasa baada ya hapo na mimi nikatunga shairi na chini ya jina langu nikaweka aka funzadume kama kumlipa mzee wangu ile aka ya washawasha nilipomwonyesha lile shairi mzee alicheka sana ilo jina la funzadume kwa hiyo nilipojifunza kufungua e-mail miaka ya nyuma sana wakati mtandao ndio unapata umaarufu Bongo nilijaribu kwa kutumia e-mail funzadume@yahoo.com
Toka hapo kila mtandao naoingia natumia jina la funzadume, inachekesha na wengine wanaliponda ila kwangu lina historia sana na nyumbani uwa wananiita kifupi funza
kwa hiyo jina ni Funzadume mwana wa Washawasha
Nakumbuka enzi hizo moja ya washairi washawasha alikuwepo, kweli wewe mwana wa washawasha ulimlipa baba yako kwa ushairi