Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?


Haya babu, pata hii hapa bana:
The Following User Says Thank You to Asprin For This Useful Post:

Keren_Happuch (Today)

 
...................................nikupe hongera sana mkuu kwa hii thread,zaidi mno kwa wana jf wote waliochangia na wengine watakaoendelea kuchangia. Si tuu kwamba imefanya tufahamiane ila pia imetukumbusha tulikotoka,inaelekeza tunako kwenda na kutuonyesha hapa tulipo. Mimi ni Mwenzetu kama jina langu lilivyo.
 
Mimi ni mtu wa furaha muda wote, napenda kusifu, napenda kushangaa na kushangalia. Ninahakikisha kabla ya kulala ninaingia kitandani nikiwa na furaha, nikiamka ninatafuta sababu ya kuwa na furaha. Siku inapita, maisha yanakewnda. MAMMAMIA is an Italian expression!

Nikiona zuri, Mammamia!; baya, Mammamia!; mchangiaji ameweka vitu safi, Mammamia!; hata anayeboa, Mammamia!; msichana aliyeumbika, oooooh, Mammamia!

Otherwise ningeweka OMG (Oh My God), lakini hii nimeipenda zaidi.
 
Reactions: BAK
Hii ni post nzuri sana, asante sana Babu. Ni moja kati ya posts nilizozipitia mwanzo hadi mwisho. Ni vizuri kufahamiana.
 
Reactions: BAK
mipango mji dalali maarufu huku kwetu, naish kwa mipango kila kitu kwangu ni mpango
 
 
Mzee BAK.
Thanks for the thread.Ila kuna mtu humu ndani alishauri tuangalie pia avatar anayotumia mtu na kana ina uhusiano au maingiliano na jina lake!Nadhani ingeleta ladha zaidi.
Jina langu linamaananisha mtizamo wangu wa kutokubali kudanganywa tena hasa na wanasiasa uchwara wa sasa.Lakini pia linaashiria mabadiliko katika mtizamo wangu kisiasa.Mwaka 2005 mimi nilikuwa shabiki mkubwa sana wa JK na nilimpigia kura nikiwa na imani naye sana.Mwaka 2010 baada ya kuona madudu aliyoyafanya hapa kati ndo nikaamua kujiita hivyo.Kwamba mwaka 2010 sidanganyiki!
Avatar yangu inaonyesha panya anayeuangalia kwa makini mtego uliowekewa chambo!Ingawa anashawishika na hicho chambo lakini anadhamiria kutoshawishika!
Kwa maana nyingine huyu panya yuko wary!(marked by keen caution, cunning, and watchfulness especially in detecting and escaping danger!)
 
susy ni kifupisho cha jina langu halisi.
 
tzjamani --- Jamani Tanzania

Naishangaa and kuililia Tanzania yangu kwa kuwa maskini wakati utajiri wa rasimali Mungu katujalia.
 
 
Reactions: BAK

Copyright ina sehemu ya moral right yaani mwandishi ana uhuru wa ku-disclose jina lake au la!
 
Miaka ya 50 babu yangu aligundua gundi akaiita nyamgluu. Wakoloni wakamchakachulia idea yake. Kwaio namwonyesha babu kuwa mimi bado namkubali na innovation yake. Kaka wa babu ndie aliyegundua Tanzanite nae wakamchakachua. Alilipwa sh 20! Dah if only....
 
Regam lina maana ya members wa familia yangu. Re- ni herufi mbili za kwanza za jina la mke wangu(rehema), ga- ni herufi za kwanza za jina langu(gabriel)na jina la mwanangu wa kwanza (gabriel jnr.), m- ni herufi ya kwanza ya jina la mwanangu Mwile.
 
Mimi ni mmoja wa tuliopinga kwa nguvu kufutwa kwa azimio la arusha..na kuirithiwa na azimio la zanzibar

... Nilipendekeza serekalini na kwa vyombo mbalimbali kuanzishwa kwa Azimio Jipya..

...bado natumaini linakuja.
 
Nyandaigobeko.

Hili jina limetokana na majina mawili,Nyanda na Igobeko. Ninatumia hili jina kwani lina historia tamu sana.

Kule usukumani kulikua na utawala wa kichifu(kunaitwa Sima,maeneo ya Sengerema),sasa huyo chifu alikua na watoto kadhaa afu na mfanyakazi 1 ivi wa kiume. Wakati wa Muingereza,ikaja oda kua watoto wa machifu wakasome,sasa chifu akakataa kuruhusu watoto wake wakasome (aliogopa pengine wasingerudi hai),ivyo chifu akamwambia yule kijana mfanyakazi ndo akasome! Kijana akaenda kupata elimu na akaelimika,kisha akarudi Sima. Chifu alipofariki kasheshe likaanza kwny nani amrithi,watoto wake walikua hawajasoma ivyo wakazidiwa ujanja na yule kijana mfanyakazi aliesoma(alijua kusoma na kuandika,ivyo akatumia ujanja ujanja na kwenda kwa Muingereza na maandishi kua yeye ndo kateuliwa kua chifu). Ivyo alivyorudi akajitangaza kua chifu(ingawa hakustahili kua kwavile yeye alikua mfanyakazi tu). Sasa baada ya kua chifu,akaamua kujipa jina la Igobeko yaani mtu aliejipachika au kujichomeka au kujitosa mahala na kuwazidi ujanja waliokuwepo.

Hivyo ndivyo filosofia yangu ilivyo. Nyanda maana yake ni kijana kwa kisukuma. Ivyo unganisha na maana ya Igobeko,utaelewa mimi nikoje.
 
"Mbaha" ni neno la lugha ya kipare (ingawa mimi si mpare) maana yake kwa kiswahili ni "Mkubwa" neno ninalopenda sana kuwaita wenzangu kila ninapowasiliana nao bila kujali umri wao.
 
"Mbaha" ni neno la lugha ya kipare (ingawa mimi si mpare) maana yake kwa kiswahili ni "Mkubwa" neno ninalopenda sana kuwaita wenzangu kila ninapowasiliana nao bila kujali umri wao.

Mbaha, kwa nini kipare na siyo kutumia jina la kabila yako lenye maana kama hiyo?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…