Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kumbe unayajua mambo...nlifikiri unabahatisha.

Najua bana, Ayubu ni yule aliyevumilia mateso mengi kwa ajili ya kutetea imani yake ya kutokumkufuru Mungu.....Nakumbuka alipata majipu mwili mzima, damn na majipu yanavyouma OMG!

na hapa usiponigongea senksi ntakususia wiki nzima!

Haya babu, pata hii hapa bana:
The Following User Says Thank You to Asprin For This Useful Post:

Keren_Happuch (Today)

 
...................................nikupe hongera sana mkuu kwa hii thread,zaidi mno kwa wana jf wote waliochangia na wengine watakaoendelea kuchangia. Si tuu kwamba imefanya tufahamiane ila pia imetukumbusha tulikotoka,inaelekeza tunako kwenda na kutuonyesha hapa tulipo. Mimi ni Mwenzetu kama jina langu lilivyo.
 
Mimi ni mtu wa furaha muda wote, napenda kusifu, napenda kushangaa na kushangalia. Ninahakikisha kabla ya kulala ninaingia kitandani nikiwa na furaha, nikiamka ninatafuta sababu ya kuwa na furaha. Siku inapita, maisha yanakewnda. MAMMAMIA is an Italian expression!

Nikiona zuri, Mammamia!; baya, Mammamia!; mchangiaji ameweka vitu safi, Mammamia!; hata anayeboa, Mammamia!; msichana aliyeumbika, oooooh, Mammamia!

Otherwise ningeweka OMG (Oh My God), lakini hii nimeipenda zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

[SIZE=4[FONT=Book Antiqua]Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Hii ni post nzuri sana, asante sana Babu. Ni moja kati ya posts nilizozipitia mwanzo hadi mwisho. Ni vizuri kufahamiana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mipango mji dalali maarufu huku kwetu, naish kwa mipango kila kitu kwangu ni mpango
 
hahahah..!! unaniangusha sasa babu! Vitu kama hivi unatakiwa uvijue ili uwafundishe wajukuu!

Ayubu hakulewa, na hakulala na mabinti zake! Aliyefanya hivyo ni Lutu.

Yaani unanifikiri ingekuwa Keren_Happuch amefanya hayo, ningechukua jina lake, aakha!!!! Tabia nyingine zinatembea na majina ati![/QUOTE]


KH hapo kwenye nyekundu ni kweli kabisa kama yale majina ya havinitishitishi
 
Mzee BAK.
Thanks for the thread.Ila kuna mtu humu ndani alishauri tuangalie pia avatar anayotumia mtu na kana ina uhusiano au maingiliano na jina lake!Nadhani ingeleta ladha zaidi.
Jina langu linamaananisha mtizamo wangu wa kutokubali kudanganywa tena hasa na wanasiasa uchwara wa sasa.Lakini pia linaashiria mabadiliko katika mtizamo wangu kisiasa.Mwaka 2005 mimi nilikuwa shabiki mkubwa sana wa JK na nilimpigia kura nikiwa na imani naye sana.Mwaka 2010 baada ya kuona madudu aliyoyafanya hapa kati ndo nikaamua kujiita hivyo.Kwamba mwaka 2010 sidanganyiki!
Avatar yangu inaonyesha panya anayeuangalia kwa makini mtego uliowekewa chambo!Ingawa anashawishika na hicho chambo lakini anadhamiria kutoshawishika!
Kwa maana nyingine huyu panya yuko wary!(marked by keen caution, cunning, and watchfulness especially in detecting and escaping danger!)
 
susy ni kifupisho cha jina langu halisi.
 
tzjamani --- Jamani Tanzania

Naishangaa and kuililia Tanzania yangu kwa kuwa maskini wakati utajiri wa rasimali Mungu katujalia.
 
hahahah..!! unaniangusha sasa babu! Vitu kama hivi unatakiwa uvijue ili uwafundishe wajukuu!

Ayubu hakulewa, na hakulala na mabinti zake! Aliyefanya hivyo ni Lutu.

Yaani unanifikiri ingekuwa Keren_Happuch amefanya hayo, ningechukua jina lake, aakha!!!! Tabia nyingine zinatembea na majina ati![/QUOTE]


KH hapo kwenye nyekundu ni kweli kabisa kama yale majina ya havinitishitishi

Ni kweli kabisa BAK, mimi niko makini sana na maana ya jina! Kuna watu wanawapa watoto wao taabu, shida, matatizo....! Kwa kweli unaweza ukashangaa hao watu wakawa na maisha ya taabu siku zote, na hata wasione connection ya majina yao!

Otherwize thanks BAK for very this useful thread!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukubi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.

Copyright ina sehemu ya moral right yaani mwandishi ana uhuru wa ku-disclose jina lake au la!
 
Miaka ya 50 babu yangu aligundua gundi akaiita nyamgluu. Wakoloni wakamchakachulia idea yake. Kwaio namwonyesha babu kuwa mimi bado namkubali na innovation yake. Kaka wa babu ndie aliyegundua Tanzanite nae wakamchakachua. Alilipwa sh 20! Dah if only....
 
Regam lina maana ya members wa familia yangu. Re- ni herufi mbili za kwanza za jina la mke wangu(rehema), ga- ni herufi za kwanza za jina langu(gabriel)na jina la mwanangu wa kwanza (gabriel jnr.), m- ni herufi ya kwanza ya jina la mwanangu Mwile.
 
Mimi ni mmoja wa tuliopinga kwa nguvu kufutwa kwa azimio la arusha..na kuirithiwa na azimio la zanzibar

... Nilipendekeza serekalini na kwa vyombo mbalimbali kuanzishwa kwa Azimio Jipya..

...bado natumaini linakuja.
 
Nyandaigobeko.

Hili jina limetokana na majina mawili,Nyanda na Igobeko. Ninatumia hili jina kwani lina historia tamu sana.

Kule usukumani kulikua na utawala wa kichifu(kunaitwa Sima,maeneo ya Sengerema),sasa huyo chifu alikua na watoto kadhaa afu na mfanyakazi 1 ivi wa kiume. Wakati wa Muingereza,ikaja oda kua watoto wa machifu wakasome,sasa chifu akakataa kuruhusu watoto wake wakasome (aliogopa pengine wasingerudi hai),ivyo chifu akamwambia yule kijana mfanyakazi ndo akasome! Kijana akaenda kupata elimu na akaelimika,kisha akarudi Sima. Chifu alipofariki kasheshe likaanza kwny nani amrithi,watoto wake walikua hawajasoma ivyo wakazidiwa ujanja na yule kijana mfanyakazi aliesoma(alijua kusoma na kuandika,ivyo akatumia ujanja ujanja na kwenda kwa Muingereza na maandishi kua yeye ndo kateuliwa kua chifu). Ivyo alivyorudi akajitangaza kua chifu(ingawa hakustahili kua kwavile yeye alikua mfanyakazi tu). Sasa baada ya kua chifu,akaamua kujipa jina la Igobeko yaani mtu aliejipachika au kujichomeka au kujitosa mahala na kuwazidi ujanja waliokuwepo.

Hivyo ndivyo filosofia yangu ilivyo. Nyanda maana yake ni kijana kwa kisukuma. Ivyo unganisha na maana ya Igobeko,utaelewa mimi nikoje.
 
"Mbaha" ni neno la lugha ya kipare (ingawa mimi si mpare) maana yake kwa kiswahili ni "Mkubwa" neno ninalopenda sana kuwaita wenzangu kila ninapowasiliana nao bila kujali umri wao.
 
"Mbaha" ni neno la lugha ya kipare (ingawa mimi si mpare) maana yake kwa kiswahili ni "Mkubwa" neno ninalopenda sana kuwaita wenzangu kila ninapowasiliana nao bila kujali umri wao.

Mbaha, kwa nini kipare na siyo kutumia jina la kabila yako lenye maana kama hiyo?

 
Back
Top Bottom