Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Jina hili nilipewa na watu wangu wa karibu kutokana na magari ninayoingiza mara kwa mara yakiwa saba au zaidi.

Ndio likaanzia hapo
 
KWEZISHO - Kitongoji katika kijiji chetu na ndipo kulipo na chemchem ya maji mengi inayotegemewa na watu wengi kipindi cha kiangazi, ila kando tu ya hilo eneo kuna shamba langu.
-Kwa kisambaa ina maana kwenye jicho.
Onga umbuje.
 
Hili ni jina langu kweli.
Kipindi hicho nazunguka kwenye gyms na sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujiweka fit nikaingia kwenye ubondia.

Kila bondia anataka jina la kutisha wenzake, nikatumia langu la ukweli ili kudhihirisha kua hata katika uhalisia wangu bado nina uwezo wa kukutisha (ingawa nafikiri sura yangu ndiyo iliwaogopesha[emoji23] [emoji23] [emoji12] [emoji23] [emoji12] [emoji23] [emoji23] [emoji12] )
 
the boss...............ni kwa sabbu kweli i amm the bossi.
Hili jina ni jina langu nje ya jf.

Na nilishangaa nilipojiunga kukuta mtu mwenye jina kama langu.


Sasa wengi hua wanachanganya wanafananisha jina lako na langu.


Hua nakazi ya ziada kusema huyo wa jf sie Mie.
 
Ukikua utaacha kuulizia kwa lengo la kufahamu ID za Watu hapa JF!
 
Nasemanao - nimekamatwa na polisi wamenizunguka, wamenidhulumu haki yangu ya msingi kwa kutumia mabavu lakini sijakata tamaa naendelelea kusemanao mpaka nipate haki yangu, haki yangu ya kulindwa na polisi na sio kupigwa kuchezea virungu na uonevu wa kila aina, haki yangu na uhuru wangu na sio kununua haki kwa rushwa wakati sina kosa lolote mtanzania mimi.
 
Fanya upeleleze kituo cha mawasiliano hapa hupati kitu. Potea rudi kwenye desk waambie mission impossible
 
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukubi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Mi langu hata halina maana yeyote nimejisikia kuliweka tuu,
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana Mkuu endelea kupigania haki yako mpaka kieleweke.

Nasemanao - nimekamatwa na polisi wamenizunguka, wamenidhulumu haki yangu ya msingi kwa kutumia mabavu lakini sijakata tamaa naendelelea kusemanao mpaka nipate haki yangu, haki yangu ya kulindwa na polisi na sio kupigwa kuchezea virungu na uonevu wa kila aina, haki yangu na uhuru wangu na sio kununua haki kwa rushwa wakati sina kosa lolote mtanzania mimi.
 
Back
Top Bottom