Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Asalam wanajamvi?

Niende moja kwa moja kwenye mada! nini kilichopo nyuma ya hilo jina. Nini unakikumbuka ukajiita hilo jina! yapo majina mengi yanatoa tafakari na burudani!

Nikianza na mimi kindikinyer leborosier

Ni muunganiko wa vijiji vinne vilivyoandkwa kwa kifupi:

Kindi ni kijiji kimoja kipo kibosho kilimanjaro ambapo niliwahi kukaa kwa miaka minne nilijifunza uchaga na tamaduni zao zilinivutia na hua napakumbuka sana!

Kinyer (lendikinya) ni mtaa mmoja upo monduli umasaini niliwahi kwenda kusanya data nikajifunza mambo mengi ya kimasai.
Na tamaduni zao pia!

Leboro ni kijiji kingine kipo Manyara wilaya ya mbulu kata ya mama isara, ni chimbuko la wambulu (wairaki) niliwahi kwenda kukaa na kufanya shughuli zangu pale kwa muda pia, ni mahali pako vizur sana milima ile hali ya hewa ya ubaridi.. napakumbuka sana!

Na mwisho sier (esere) ni kijiji kipo wilaya ya ngorongoro mkoa wa Arusha kata ya enduleni, hapa kuna mambo mengi sana yalinifanya niishangae sana Tanzania, madini, mapango ya kale, na nyayo za mtu wa kale ambae zipo pembeni kidogo panaitwa laitolye, wanaishi wamasai nilijifunza mengi pia!!

Nini kinakukumbusha ukitazama jina lako la JamiiForums!!

Uzi tayari
https://www.jamiiforums.com/threads/je-jina-lako-id-unalotumia-jamiiforums-lina-maana-yoyote.40266/
 
Sawa mpenzi...

Na mimi naitwa brather... nimezaliwa peke yangu...

Naona huu ni mpango wa maulana kutukutanisha hapa. Labda uwe mbishi tu
Hapana wewe utakuwa san[emoji16][emoji16]
 
Asante, haha the other one is my famous nickname wengi wanaonijua nje ya JF wanalijua lile jina na ukizingatia ninayoandika humu sivyo nilivyo basi kuna watu wakaanza kunifuata wakisema hawaamini kama ni mimi ndiyo naandika haya ninayoandika humu

Wakati kiuhalisia mimi ni mpole ila humu naonekana nina mdomo nikasema mimi ndiyo napenda nionekane hivi humu ila nikaona isiwe taabu acha nibadilishe tu nitafute id ambayo hamna mtu yeyote anayenijua anaijua then nikaona hii ndiyo inafaa.

...and why did yo change from the other one
....btw hii ya sasa iko poa zaidi
 
Baada ya kuwa nafanya project ya kuongeza nguvu za kiume kupitia wi-fi na jina la project yangu ya kisayansi ni mbo technology nikaunga nikapata mbotech
 
Hivi hawa watu wenye id zaidi ya moja mnawajuaje mbona mimi simjui hata mmoja?
Sijajua km Ni ya kwake.
Avatar zinafanana halafu huyo Humble amepotea kitambo Sana.
Unaweza kuangalia miandiko km inalingana.
 
Majibu yako
.Zitaenda orphanage kuchangia
.Rafiki yangu ni pombe sio watu sipendi watu
.haha unaogopa kifo kila mtu atakufa
.yes anaonekana kujali ila Kama amenipenda au wapo wanaotamani uwepo wangu imekula kwao wapambane na Hali zao waniache na mm nipambane na Hali yangu
.mwisho nikiandika nitakutag
Na mimi naomba unitag
 
Safi mkuu hata mimi namkubali sana Kylian Mbappe na nilikuwa sipendi kabisa mpira ila baada ya France kuchukua kombe la dunia mwaka jana ndiyo nikaanza rasmi kuwa shabiki wa mpira kwa sababu ya maajabu aliyoyaonesha huyo dogo na nimemuweka kwenye top four katika list yangu ya wachezaji bora duniani
What is your EPL team??
 
Back
Top Bottom