Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Anne jina langu lingine ila Sio official.
Nilizaliwa kipindi wazazi wanasali uwata.
Yalipendekezwa majina 3 baada ya maombi na hili lilikuwapo.
Likapita moja la kutumia officially.

Saint ,hakuna aliye mkamilifu ila najitahidi kuutafuta utakatifu ili niwe Bora na nimpendeze Mungu sawa na zaburi 16:3
Bwana asifiwe Mpendwa, pole na kuniombea, karibu faraga ya emau!
 
Mimi navuta sana bangi na ndio starehe na kitulizo pekee cha akili na mwili, nikaamua kujiita kayaman
 
The notorious conor mcgregor fearless young talented ucl fighter of all time(kwangu). Huyu jamaa kapitia life gumu sana mpaka akaja kutoboa kupitia ucl fights sio mchezo aisee.
I was so dissapointed alivyopigwa na mayweather aisee
Hahaha...umemsahau Khabib Nurmagomedov.
 
'Ngareroo'natokea Ngarenaro A-Town Arusha,,Ngareroo ni swaggz tu ya Jina Ngarenaro,pia napenda sana kuongea Slangs ya Chuga ambayo tunaiitaga 'Ngareroo slangs'...Ni ivo tu Laigwanani.
Lol nilijua umeitoa kwenye ule wimbo wa Joh Makini ft AKA wa Don't Bother kwenye chorus kuna mstari anasema "daraja mbili ngarero daraja hili hawadandii masoro"
 
KAYEMBA

Kayemba ni jina/title ambalo mzazi wangu analomuita mzazi wa mke wangu kwa kule kwetu nyanda za juu kusini. Sasa mimi nimefanana sana na babu yangu mzaa mama hivyo babu na bibi upande baba wakawa wananiita KAYEMBA
 
KAYEMBA

Kayemba ni jina/title ambalo mzazi wangu analomuita mzazi wa mke wangu kwa kule kwetu nyanda za juu kusini. Sasa mimi nimefanana sana na babu yangu mzaa mama hivyo babu na bibi upande baba wakawa wananiita KAYEMBA
Kingozi! Akili yangu ni nzito sana.

Unaweza ukaenda taratibu hapo kwenye Bibi na Babu nakadhalika? Hizo mimi huwa zinanichanganya sana. Zikitumika sentensi huwa nashindwa kuielewa.

Samahani lakini.
 
Back
Top Bottom