BOEING 747....nadhani siyo jina geni kwa watu..
Ni ndege kubwa ya pili duniani ya kubeba abiria..k
Achana na Antonovo ndiyo ndege kubwa kabisa lakini ni ya mizigo..
Kwa nini nikajiita Boeing..?
Mwaka 2013 na 2014 nilikuwa ninaishi USA...nilipaa kwa KLM from Dar to Amsterdam...hii ilikuwa Boeing 777
Nilifika Amsterdam saa moja Asubuhi saa za Netherlands...nikawa natakiwa nifanye connection ya ndege nyingine kwenda USA..na ndege hiyo ilikuwa inapaa saa Sita mchana saa za Netherlands..so nilikuwa na muda mrefu wa kukaa pale Schiphol airport...
Siku hiyo ndiyo kwa mara ya kwanza naiona BOEING 747 double deck ikiwa ardhini...ndiyo niliyoipanda kwenda Marekani...
Wazee lile dude ni kubwa...nililipenda na mara kwa mara naliota usingizini..wakati wanapakia mizigo mule lilifunguliwa ile pua ya mbele. kukawa kuna Fork lift zinatembea huko ndani kama zipo kwenye godown..[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] ...wazee ile ndege inabeba...kilichonivutia zaidi tulivyofika pale O'Hare international airport Chicago, yule rubani alikuwa analiteremsha lile lidege kwa mbwembe mpaka nikawa nasikia maini yanapanda juu[emoji16][emoji16]..
Katika maisha nimebeba vitu vingi vya kihistoria wakiwemo watu ambao nimewabeba...basi nikajifananisha na ile ndege iliyonipeleka kwa Obama by then....USA the land of Opportunity..[emoji39][emoji39][emoji39]
Kwa sasa nipo nchini naunga mkono juhudi za awamu ya tano...[emoji106][emoji106]
Im proud to be Boeing 747, The Jumbo of the sky..