Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Asalam wanajamvi?

Niende moja kwa moja kwenye mada! nini kilichopo nyuma ya hilo jina. Nini unakikumbuka ukajiita hilo jina! yapo majina mengi yanatoa tafakari na burudani!

Nikianza na mimi kindikinyer leborosier

Ni muunganiko wa vijiji vinne vilivyoandkwa kwa kifupi:

Kindi ni kijiji kimoja kipo kibosho kilimanjaro ambapo niliwahi kukaa kwa miaka minne nilijifunza uchaga na tamaduni zao zilinivutia na hua napakumbuka sana!

Kinyer (lendikinya) ni mtaa mmoja upo monduli umasaini niliwahi kwenda kusanya data nikajifunza mambo mengi ya kimasai.
Na tamaduni zao pia!

Leboro ni kijiji kingine kipo Manyara wilaya ya mbulu kata ya mama isara, ni chimbuko la wambulu (wairaki) niliwahi kwenda kukaa na kufanya shughuli zangu pale kwa muda pia, ni mahali pako vizur sana milima ile hali ya hewa ya ubaridi.. napakumbuka sana!

Na mwisho sier (esere) ni kijiji kipo wilaya ya ngorongoro mkoa wa Arusha kata ya enduleni, hapa kuna mambo mengi sana yalinifanya niishangae sana Tanzania, madini, mapango ya kale, na nyayo za mtu wa kale ambae zipo pembeni kidogo panaitwa laitolye, wanaishi wamasai nilijifunza mengi pia!!

Nini kinakukumbusha ukitazama jina lako la JamiiForums!!

Uzi tayari
Jina Ebenezer halina historia sana japo ni jina fulani hivi la kiebrania ambalo lipo katika vitabu vya dini na pia lina maana yake kibiblia
 
Lisu ni ngumu kuwa Rais. Nyie wachaga hamtakubali agombee kupitia Chadema. Lazima Mbowe ambanie tu. Victoire ni jeshi la mtu mmoja. Nadhani Victoire timing ilimponza tu. Alitakiwa baada ya awamu hii ndo aende Rwanda akampinge Kagame. Angeendelea kuweka nguvu zake kwenye mitandao huku akiwa Uholanzi.
Khaaaa! Umeanza ubaguzi wallah... Huyo Mbowe kagombea urais mara ngapi??

Afu nani alikuambia mi mchagga? Shika adabu yako nakwambia
 
Typing error, ahsante ila ndo maana nasema somo la bt au botany sijawahi kulipenda maishani mwangu, corse work za hili somo zilikuwa vichekesho...... Kwa waliosoma kwa dokta manoko udsm nadhani wanaelewa
Ahahahah mimi somo la biolojia kiujumla nilimalizana nalo nilipomaliza form four japo siyo kwamba nililichukia hapana
 
In short focus on your goals.

Dagagekyeulalwe : wawindaji porini hata simba akiwa anawinda uwa ana deal na ile target yake tu. Mathalani kwenye kundi la nyumbu ama pundamilia akishamtarget mmoja ni anakomaa nae huyo huyo hata kama atajichanganya Kwa wengine atakamatwa yeye tu. Hii dagagekyeulalwe (fukuzia ulichokianzisha) means we should not deviate from the main goal Kwa namna yoyote ile....
 
Kuna siku nilikuwa naangalia mpira zaman kidogo (sijui ilikuwa ligi gani) kuna mchezaji akawa na hilo jina... Na kwa kuwa linaendana na jina langu halisi nikalipenda kulitumia kama nickname
 
  • Thanks
Reactions: BAK
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahah niko huku kwa mabingwa wa kombe la dunia babu!!

Halafu unajua mimi naweza nisiwe mjukuu wako kabisa kwani una umri gani??
 
Mmhh wewe siyo kwamba umeenda huko kwa sababu ndiyo wamechukua ubingwa wa uefa msimu huu? Maana kuna watu wengine wanashabikia mpira ila ukiwauliza timu gani hawana timu wao timu yoyote itakayoshinda ndiyo ya kwao ikishindwa wanahamia kwingine

Shabiki wa kweli huvumilia yote by the way mimi nachagua timu kutokana na wachezaji ninaowapenda kwa Europe niko Barcelona na kwa Africa niko Simba vipi wewe wachezaji wako bora duniani ni wepi tukianza na Mohammed Salah? Najua tu yeye ndiyo wa kwanza
Hapana[emoji23][emoji23][emoji23].
Nipo Liverpool tangu enzi zile za kina Gerald na Torres.

Huyu Mo salah kijana wa juzi tu huyu.
 
BOEING 747....nadhani siyo jina geni kwa watu..
Ni ndege kubwa ya pili duniani ya kubeba abiria..k
Achana na Antonovo ndiyo ndege kubwa kabisa lakini ni ya mizigo..
Kwa nini nikajiita Boeing..?
Mwaka 2013 na 2014 nilikuwa ninaishi USA...nilipaa kwa KLM from Dar to Amsterdam...hii ilikuwa Boeing 777
Nilifika Amsterdam saa moja Asubuhi saa za Netherlands...nikawa natakiwa nifanye connection ya ndege nyingine kwenda USA..na ndege hiyo ilikuwa inapaa saa Sita mchana saa za Netherlands..so nilikuwa na muda mrefu wa kukaa pale Schiphol airport...
Siku hiyo ndiyo kwa mara ya kwanza naiona BOEING 747 double deck ikiwa ardhini...ndiyo niliyoipanda kwenda Marekani...
Wazee lile dude ni kubwa...nililipenda na mara kwa mara naliota usingizini..wakati wanapakia mizigo mule lilifunguliwa ile pua ya mbele. kukawa kuna Fork lift zinatembea huko ndani kama zipo kwenye godown..[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] ...wazee ile ndege inabeba...kilichonivutia zaidi tulivyofika pale O'Hare international airport Chicago, yule rubani alikuwa analiteremsha lile lidege kwa mbwembe mpaka nikawa nasikia maini yanapanda juu[emoji16][emoji16]..

Katika maisha nimebeba vitu vingi vya kihistoria wakiwemo watu ambao nimewabeba...basi nikajifananisha na ile ndege iliyonipeleka kwa Obama by then....USA the land of Opportunity..[emoji39][emoji39][emoji39]

Kwa sasa nipo nchini naunga mkono juhudi za awamu ya tano...[emoji106][emoji106]

Im proud to be Boeing 747, The Jumbo of the sky..
Hahahaha..
Opportunities gani uliziona huko.?
 
Yeah nimeshasema kule juu sababu ni kuwa nilitaka tu jina lolote zuri lenye herufi nane, yaani konsonanti nne na irabu nne zilizojipangilia vizuri ndiyo likaja hili.
Ngoja nikubali kishingo upande..
 
Back
Top Bottom