Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
Vyakula vingi vilivyopo huku kule pia vipo...kinachotufautiana sana ni mapishi..Na wali nao upo!?
Ndizi je!?
Nako kuna migomba!??.
Hivi huko nako Kuna daladala halafu makondakta wanakuwa rafurafu km huku kwetu!?
Halafu nasikia masaa yamepishana, huko muda huu Ni mchana au asbh.. hivi si naeza shida nmelala mchana usiku kwangu ndio mchana.maana kasheshe ya kubadili Muda Sio ndogo
Mchele upo unauzwa,viazi, nyanya, hoho..n.k..
Ndizi nilikuwa napata mbichi na mbivu ila zina utofauti kidoogo na huku kwetu..
Daladala no...[emoji16][emoji16].Wana mabasi kama haya ya mwendokasi ambayo hayana conductor..unatumia kadi au cash....ukifika kituoni kwako unabonyeza tu swich, dereva anasimama..[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
Wenzetu wameendelea zaidi..
Hatufanani muda...Kwa mfano ukiwa majimbo ya mid west kama Chicago, Indiana na Iowa ambapo ndipo nilikuwa naishi, tunapishana almost masaa 8...Tanzania ipo mbele kwa masaa 8...kwa mfano huku ikiwa ni saa 4 usiku, kule ni saa 8 mchana siku hiyo hiyo...
Huku pakiwa saa 8 mchana kule ni saa 12 asubuhi...ndiyo panakucha..
Kwa majimbo yaliyopo Mashariki zaidi mfano Washington DC napo nilikaa tunapishana masaa kama 7..
Majimbo yaliyopo Magharibi zaidi tunapishana nayo masaa mengi 8 na zaidi....ile nchi ni kubwa sana..
.[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji39] kwa hiyo kule ikifika kati ya saa 6 mpaka 8 mchana (majimbo niliyoyataja coz ndipo nilipoishi) ndiyo unampigia cm mtu wa TZ kumtakia usiku mwema...ambapo huku huwa ni kati ya saa 2 mpaka 4 usiku...
Kupata maruweruwe ya usingizi siku za mwanzo ni kawaida...tofauti ya masaa 8 si ndogo....na isitoshe miezi hii ya Summer, Kule jua linazama saa mbili usiku[emoji83][emoji83][emoji83]....This is crazy