Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kipindi cha miaka ya 1994, lilikuwepo kundi maarufu sana la waigizaji nchini Kenya. ambao walikuwa wanarusha vipindi vyao kupitia KBC. Baadhi ya waliokuwepo kwenye kundi hilo ni Mzee Ojwang, Mama Kayayiii (mke wa mzee Ojwang), Masaku, Otorong'ong'o, Maliwasa, Makanyaga........
 
NIkiwa kwetu, kuna mzee tulikuwa tunaishia naye jirani, mjini. Sasa mijini kuna haya makundi ya ngoma za kienyeji yanayotoa burudani, kwa wakati huu kwenye masherehe. Kule kwetu kulikuwa na kundi la ngoma ya mganda, ambalo kila Jumapili kulikuwa na eneo fulani makundi haya yanatoa burudani bure. Unahama tu toka kwenye ngoma hii kwenda nyingine. Sasa huyo mzee (RIP Ngalikihinja) alikuwa ananilazimisha mimi nijiunge na kundi la ngoma ya mganda, maana ni ya kijiji kwetu. Nikajiunga na kuwa napiga ngoma ndogo (perekete - cocastic anaweza akawa anaijua). Kumuenzi nikaamua kutumia jina lake huku JF
 
Back
Top Bottom