Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

tam- initials ya majina yangu rasmi.
sana- niliweka baada ya kuonekana jina 'tam' lilikuwa limesasajiliwa humu. Ili kijitofautisha nikajiita tamsana.
Thomas
Timoth
Timotheo
Theophil
Titus
Tito

T 😎
 
Farolito(Little star)

Huu ni wimbo wenye ladha ya Latin/Salsa ninaoupenda umeimbwa na Gloria Estefan,kwa mara ya kwanza niliusikia miaka mingi iliyopita nilikuwa kwenye basi natoka chuo kwenda mjini,nikaupenda,niliposhuka nikaongea na dereva nikamwambia nimeupenda huu wimbo,kaimba nani nikautafute?hata yeye akasema hajui ila akanionyesha kumbe aliweka kaseti,basi nikamsihi sana aniuzie,nashukuru alikubali nikampa sh 2,000 akaniachia.

Nilipoangalia ndio nikajua ilikuwa Gloria Estefan album ya Abriendo Puertas,na nikagundua pia kulikuwa na nyimbo nzuri zingine humo,hio Cassette nimeitunza hadi Leo.

Maana halisi ya neno Farolito ni taa Fulani za karatasi zinamwanga wa mdogo,zinatumiwa zaidi kuonyesha upendo,au kumbukumbu nzuri kwa mtu au tukio.Huko Latin America hupangwa barabarani au pembeni ya kuta za nyumba kusherehekea Christmas au Santa Fei.

Kwahio nilijiita Farolito kwa kuwa naupenda wimbo huu na maana yake halisi na kumbukumbu yake iliyobeba na jinsi taa hii ilivyosifiwa ndani ya wimbo huu.
]
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    50.3 KB · Views: 5
DIY do it yourself... Yes fanya kila kitu mwenyewe, mie ni mmoja wapo wa watu wanapenda fanya kila kitu, naamini hakuna binadamu hawezi fanya kile kitu ambacho mwenzie anaweza fanya ni determination tu, ukiwa mwanaume fanya kila kitu mwenyewe!
 
(Lucky) (line)
Lucky= nilipewa na doctor, mama anasema wakati wa kuzaliwa nilitanguliza miguu, it was complicated kujifungua na hakukuwepo mambo ya operation. Maness wa kawaida wote walitoka ikalazimika kuja ma dr kama 5 hivi, (hiyo sehemu huduma za afya zipogo kitambo sio kama huku) hii ishu ya kutanguliza miguu mikono inabaki nyuma mara uje mmoja mwingine ubaki ilikuwa nadra sana. Dr moja alitoka kwenda kufata kifaa wakati wengine wanaendelea anarudi ndo akakuta nishatoka hapo hapo akatoa hilo jina.
Aisee,na kwenye avatar ukaamua kutanguliza miguu kwanza[emoji3]
 
Nilikula hela ya ada kama laki 2 na ikafika tarehe za end of semester uongozi wa chuo ukatukatalia kuwa asielipa ada hafanyi paper zimebaki siku kama tatu tufanye nilikuwa sins raha laki 2 naipata wapi nikasema ngoja niombe mungu kwa siku 1 moja anisaidie nipate hela pindi nikiomba watu wanipe weee siku ya kwanza kila nikiomba kwa mtu hana siku ya pili hola daa nikasema ngoja niombe kwa shetani nikasema shetani nisaidie nibet nile nikabet mkeka nikala laki 5 daaa toka siku hiyo nikaamini shetani ukimuomba anakupa nikajitiita Iblis bin Shetan maana aliniokoa kweli
Kwahio umechagua upande wake?bado unamtegemea?
 
Yna12...nimelipenda tu hilo jina..mimi ni mpenzi sana wa philipino drama..na namkubali sana hyu dada alieigiza kama yna kwenye tamthilia moja hivi...ndio maana nikaamua kujipachika ilo jina..na hyo 12 ni idadi ya watoto niliopanga kua nao...[emoji137]
Aisee,mipango ya watoto 12 inaendelea?umefikisha wangapi mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom