Je JWTZ wako tayari kumlinda aliyevunja Katiba?

baro

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,423
Reaction score
4,986
Ndugu Wana ukumbi,

Nina swali kwenu, Je JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi vinaweza kula kiapo cha kumtumikia na kumlinda Rais aliyeingia madarakani kwa kuvunja Katiba ya nchi?

Wakati wao huapa kuilinda Katiba ya nchi?
 
Chadema kweli nyie ni vichwa bange, mkutano mkuu ndiyo wenye maamuzi ya mwisho ndani ya chama na maamuzi yake ni ya mwisho! Kwa nini mnajisumbua bure kutaka kuchonganisha Watanzania? CCM ni chama cha kisiasa, kina taratibu zake, kinaweza kupindisha katiba yake kikiona kuna ulazima na tija endapo suala husika litasadia kuokoa muda. Hata Chadema mmewaweza kuamua lolote endapo wajumbe wenu watatimiza katika kufanya lile au badiliko mnalokusudia.
 
Acha taratibu za CCM Kila mtu anazifahamu usijitoe akili, kiufupi utaratibu ulivurugwa na Katiba haikufuatwa ,Je JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi, watamtumikia Rais aliyevunja Katiba ? Au ndio mwanzo wa mapinduzi?
 
nakushauri bure achana na siasa kama akili ndio hizi
 
Mkutano mkuu ndio upo na maamuzi katika chama ila sio maamuzi yanayopitiliza kuvunja katiba ya nchi ,unasikia we chawa mzoefu, chama chochote kinaweza kufa ila sio nchi .

Ikumbukwe vyama vinaundwa chini ya katiba ya nchi , msajiri anatakiwa kukifuta chama cha ccm mara moja vinginevyo atajua Mungu yupo, hatuwezi endesha mambo ya msingi katika nchi kihuni.

Tz vyama vya siasa ndo vinaweza kutoa kiongozi mkuu wa nchi maana hatuna sheria ya mgombea binfsi , sasa kama tunaweza kuwa na vyama ambavyo vinajiendesha kihuni ,ofisi ya msajili kazi yake nini sasa, futa ccm mara moja
 
Acha ulofa we mfuasi wa maudenda..
Kwani JWTZ huwa wanaapa kulinda katiba ya chama au katiba ya JMT?
acha kuropoka kama bosi wako maudenda, tuambie ni ibara gani imevunjwa..hapo ulipo una katiba ya ccm au unaropoka?

kaa ukijua rais na jwtz huapa kwa kutumia katiba ya nchi na si katiba ya vyama..
umesikia we ropo ropo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…