Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwanza kabisa hoja yako ni potofu, natural selection haina hoja ya kwamba yenyewe haina upendeleo, haina ubaya, it is just a natural process. Natural process haijali kuhusu ubaya na uzuri.This natural selection is a fraud. Kwann ipendelee baadhi ya watu kwa vitu mbali mbali. Kwann iweke ubaya kati ya watu na watu kati ya wanyama na watu. Uthibitisho wenyew ni wa mwili tu jibu la kiroho inayotenda zaidi halina hili. Ieleezee kwann watu anaamua kusafiri kutoka sehem mbali mbali kutafuta namna ya kuishi na pia ielezee kwann mtu awe na utashi kuliko wanyama.
Mto ukijaza bwawa la maji lililo mlimani, bwawa likafurika, maji yatashuka kilima tu, maji hayatasema "haaa, hapa chini ya mlima kuna kijiji kina watu, ngoja nikwepe kijiji nisiue watu". Maji yanafuata gravity tu, hayajali habari zenu za uzuri na ubaya.
Natural processes do not have consciousness to care about good and bad, you are just projecting your human bias into natural processes. This is anthropic bias.
Lakini, ngoja nikupige "immanent critique". Nikuoneshe udhaifu wa hoja yako, kwa kuanza kama nataka kukukubalia hoja yako. Naanza kukukubalia hoja yako, halafu naonesha kwamba hata nikikukubalia hoja yako, bado hoja ya Mungu kuwapo ina matatizo.
Kwa hoja yako hii kwamba kinachoweka upendeleo kati ya watu, kinachowezesha ubaya kati ya watu, kati ya wanyama na watu ni fraud, hata nikikubali kwamba natural selection ni fraud, kwa mantiki yako, bado Mungu wako naye anakuwa fraud.
Tuseme nakukubalia natural selection ni fraud, for argument's sake.
Halafu tukasema ulimwengu umeumbwa na Mungu, halafu tukaona ulimwengu huu huu tunaosema uliumbwa na Mungu bado Mungu karuhusu uwe na upendeleo kati ya watu, uwe na ubaya kati ya watu, uwe na ubaya kati ya watu na wanyama, utakubali kwamba tukitumia mantiki yako ile ile ya kuita natural selection fraud, kwa sababu imeruhusu ubaya, hata huyo Mungu naye atakuwa fraud tu, kwa sababu na yeye karuhusu ubaya?
Unaelewa kwamba hoja yako inamuita Mungu fraud?