Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

Ivi izi porojo mnazitowa wapi? Haya mambo ya kuliusisha kanisa katoliki na hisia zenu za chuki nashindwa kuelewa zinatoka wapi.
 
Unazunguka, sema ufalme wa Roma na sio Roman Catholic elewa unacho sema kiko sawa au la.
Ufalme wa Roma tangu kuanguka kwa dola ya Rumi ya kipagani mwaka 470 A.D, ilianza kuongongozwa na doctrine ya ukatoliki. Na ilipofika mwaka 538 ukatoliki ukawa na mamlaka yote ya dini na serikali, na kuanzia mwaka huo Askofu mkuu wa Roma (Pope) akawa ndiye emperor (mfalme) wa dola ya Rumi
 
Umeandika maneno mengi sana ila huna fact yoyote ya kumpinga mleta mada,kikubwa umetumia mhemko
 
Mkuu, Nabii Danieli na Mtume Yohana walipata maono tofauti kabisa ijapokuwa mmoja alionyeshwa misingi ya upotofu, na mwingine alionyeshwa kilele cha upotofu na ukengeufu. Danieli, yeye alionyeshwa dola ambazo zilipata kibali cha mbinguni kuwa na mamlaka ya kimwili juu ya ufalme wa Yuda na waongofu wa kweli wa imani ya Kiyahudi. Hali iliyopelekea kuanzishwa kwa dini rasmi ya Kiyahudi, utitiri wa madhehebu ndani yake, na vyeo vya kidini vya kibinadamu ndani ya muundo huo wa kidini.

Huku Yohana alionyeshwa kibali cha mbingu chenye mchakato ulionyesha hatua kwa hatua za jinsi ya kuibuka kwa mamlaka ya mpinga Kristo na hata kufikia hatua ya mwisho ya ukengeufu ikiambatana na vita vya kimwili dhidi ya injili ya kweli ya Kristo, na dhidi ya waongofu wenye kumtii Kristo. Alionyeshwa imani ya kweli ilipogeuzwa na kuendeshwa chini ya mfumo rasmi wa kidini na wa kimadhehebu wenye kuhitajika kusajiliwa na kupata kibali kutoka serikalini, na pia kuibuka kwa utitiri wa vyeo vya kidini vyenye hadhi ya kibinadamu ndani ya utaratibu huu wa kuogofya, ikiwemo madai ya uhalali wa kukaimu nafasi ya Kristo mwenyewe hapa duniani.

Wanyama wanne katika maono ya Danieli ni zile dola za kipagani za Babeli, Wamedi-Waajemi, Wayunani, na Rumi ambayo ilikuja kugawanyika katika mataifa. kumi ya Ulaya Magharibi, na matatu kuondolewa na kupitisha mamlaka yenye nguvu za kiserikali na kidini ya upapa. Danieli maono yake yaliwekwa muhuri, kwa hiyo hakufunuliwa kwa kina juu ya kanisa la Kristo ama uwepo wa nyakati zake.

Mnyama wa kutisha aliyeonwa na Yohana, ni muundo wenye mamlaka za kiserikali na kidini zenye kuendesha vita na kuipotosha imani ya kweli ya Kristo. Humo zipo mamlaka nyingi, ila kwa kipekee kabisa inatajwa ya USA na ya Vatikani ambazo kwa kushirikiana kwa ukaribu ndizo zitachochea kuanzishwa kwa serikali moja na dini moja ya kipagani ulimwenguni kote chini ya mpinga Kristo. Muundo wa utawala wake utaigawanya dunia yote kuwa na majimbo kumi ya kidunia ambayo yatakuwa na watawala 10 juu ya kila jimbo.
 
NAUNGA MKONO HOJA.BUT WASABATO HISTORIA YA KANISA NA MAFUNUO WANAYAJUA KWELIKWELI.NA NI MAJASIRI KUYANENA WAZIWAZI.ILA NI WABISHI.WANAABUDU SABATO.HAWA NDIO WALE MAFARISAYO NA WALIMU WA SHERIA WALIOMSULU BISHA YESU.HAWATAKI UTAKATIFU WALA KUONGOZWA NA ROHO.WENGI WAO WATABAKI WAKATI WA UNYAKUO, MAANA HAWATAKI KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.MIMI SIO MKATORIKI,NI EFATHA.
 
Kabla ya yote kwamba kanisa ndio mnyama, basi thibitishia watu mungu yupo.
 


Mimi si msabato mkuu.

Mimi ni Mkristo, Mfuasi mwaminifu wa yesu kristo.
 
Bikira Maria (Maria mama wa Yesu) aliamini amri zote kumi (including amri ya kuishika kitakatifu sabato ya siku ya saba) maisha yake yote, na pia aliamini injili ya Bwana Yesu Kristo maisha yake yote.

Siku ya saba (sabato) ina anza from sunset Friday na inaisha after sunset Saturday.
 
Mleta uzi uko sahihi.

Kwa usahihi zaidi.

Milima saba ni falme saba: Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy. In the days when apostle John received the Revelation: five have fallen (falme 5 zimeshaanguka/zimeshapita); Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece; the one is (this is Rome); the other is not yet come (this is the papacy). When he comes he must continue a short space (1,260 prophetic days which is equal to 1,260 years).

Revelation 17:11 And the beast that was, and is not, even he is the eighth, and is of the seven, and goeth into perdition. Huyu beast ambae ni the eighth and is of the seven, ni upapa "uliofufuka" baada ya kejeruhiwa mwaka 1798 (mwisho wa ile miaka 1,260). Jeraha la upapa lilianza kupona kwa kiasi fulani in 1929. Jeraha la upapa limepona kabisa after 2020 (222 years after 1798).

So the woman who sits on the seven mountains is spiritual Babylon. Spiritual Babylon ana sit on Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy (including the resurrected Papacy).

The great red dragon (wa Ufunuo 12) ni Satan. Note that ana seven crowns on his seven heads. The seven heads are Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy (including the resurrected Papacy). Satan huwa anaitwa the prince of this world. Satan yuko nyuma ya falme za dunia ambazo zina mwasi Mungu wa Biblia. Spiritual Babylon ana sit kwenye hivyo vichwa saba.

Ukifika Ufunuo 13, utaona mnyama mwingine, ambaye ana crowns kwenye pembe zake kumi (na sio kwenye vichwa vyake saba). Note that mnyama huyu wa Ufunuo 13, ni kichwa kimoja kati ya vichwa saba (vyenye crowns) vya the red dragon. Kwenye time period ya utawala wa mnyama wa Ufunuo 13, wakati wa utawala wa zile falme 6 (vichwa 6) umeshapita. Mnyama wa Ufunuo 13 anatawala pamoja na wafalme 10 (pembe 10, ndio maana pembe zake 10, zina crowns 10). Mnyama wa Ufunuo 13 ni upapa, na pembe 10 ni falme 10 za Ulaya zinazo shirikiana na upapa (angalia pia Ufunuo 17).

Watoto wa spiritual Babylon ni spiritual Egypt, Sodom, Tyre, na miji/mataifa mingine ya kidunia yaliyo mwasi Mungu wa Biblia. Watoto wa spiritual Babylon ni pamoja na makanisa yaliyojitenga na upapa, lakini bado yanafuata mafundisho ya upapa (kama kusema siku ya sabato imebadilishwa na kuwa Jumapili, kusheherekea 25th December kama Christmas etc).

Kumbuka Babylon (Babel) ilianza toka Genesis 11. 666 ni namba ya uasi wa mwanadamu dhidi ya Mungu wa Biblia. Ni namba ya uasi wa mamlaka/ufalme wa mwanadamu dhidi ya mamlaka/ufalme wa Mungu wa Biblia. Uasi huo unakataa the holy covenant and mercy, and the gospel of Jesus Christ. Uasi huo unakataa amri za Mungu (YAHWEH), na injili ya Bwana Yesu Kristo (Bwana Yahushua Mashiach). Uasi huo unakataa sabato ya siku ya saba (Jumamosi).

Soma pia vitabu vya Ranko Stefanovic (huyu ni SDA), Revelation of Jesus Christ, na Plain Revelation (google utaviona). Ni vizuri sda wote watanzania, wanaojua kiingereza kuvisoma hivi vitabu. Ranko Stefanovic amepatia vizuri zaidi (sehemu nyingi sana) kuliko Uriah Smith (huyu nae ni SDA), kwenye kitabu chake cha Daniel and the Revelation.

Ukisoma vitabu hivyo vya Ranko Stefanovic, utaelewa vizuri sana sana sana kuhusu kitabu cha Ufunuo, na 666. Kuna sehemu chache sana ana kosea:

1) Revelation 4 ina maanisha YAHWEH yuko kwenye his holy temple in heaven, na YAHWEH anatawala, na anaabudiwa (YAHWEH reigns, and is being worshiped), so it is not necessarily a judgment scene.

2) Parapanda ya 5 ina ambatana na kuja kwa roho ya mpinga kristo duniani, pamoja na ufalme wa kiroho wa mpinga kristo (yaani ufalme wa mnyama wa Ufunuo 13, ambao ni the papacy). Parapanda ya 6 ina ambatana na ujio wa roho ya nabii wa uongo, pamoja na ufalme wa kiroho wa nabii wa uongo wa Ufunuo 13 (yaani taifa la Marekani).

Ufunuo 9:16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili; nilisikia hesabu yao.

Hawa ni malaika wa Shetani 200,000,000 (mapepo wachafu, unclean spirits, evil spirits). Wanashirikiana na ufalme wa kiroho wa mpinga kristo, na pia ufalme wa kiroho wa nabii wa uongo.

3) Kuto kupatikana kwa tiara yenye title ya Vicarius Filii Dei haimaanishi kwamba title hiyo haipo. Title hiyo ni mfano wa kujikweza kwa mwanadamu dhidi ya Mungu. Kwa hiyo title hiyo ni aina ya 666. Haijalishi namba zake zinakuwa au haziwi 666 (ingawa incidentally zina kuwa 666).

Ranko Stefanovic amepatia sana zaidi ya mafundisho ya sda wenzake kuhusu story ya kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni. Ila naona ana ogopa kuwa muwazi kusema kwamba Shetani alianguka baada ya wiki ya uumbaji. Kwa sababu akisema wazi atakuwa anapingana na mafundisho ya sda wenzake.

Mapungufu ya mafundisho ya kanisa la sda ni haya:

1) Shetani na malaika zake hawa kuanguka kabla ya wiki ya uumbaji. Kwa sababu malaika wote (including Lucifer, ambae baadae ali muasi Mungu) waliumbwa siku ya pili ya wiki ya uumbaji.

2) Hakuna viumbe wengine kama binadamu kwenye sayari nyingine (kama sda wengi wanavyo fundisha).

3) "The Day of Atonement" ni tofauti na "the Day of Judgment". New tastement fulfilment of the Day of Atonement inaanza baada ya kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu, na inaisha at the end of probation period (karibia kabisa na ujio wake wapili).

Sanctuary linalokuwa cleansed in 1844, ni kanisa huku duniani. Mafundisho ya kweli (including the 10 commandments, and the seventh day sabbath) yanarudi kanisani, na mafundisho ya uongo yanaondolewa.

4) Wabatize kwa staili waliyoitumia mitume wa Yesu, mtu ana inama kidogo kwa mbele, huku amesimama, huku akidumbukia kabisa kwenye maji. Wasibatize kwa staili ya mtu kalala kwa mgongo, wana mshika na kumdumbukiza kwenye maji.

5) Wasi wapinge sda wenzao, wanao sema kwamba Yesu alizaliwa during the Feast of Tabernacles. Kwa sababu kiukweli Yesu alizaliwa during the Feast of Tabernacles.

6) Wakubali kwamba hawa hodhi ukanisa wa kweli, na kwamba endapo kuna wasabato wanaofuata biblia ambao sio sda, wasabato hao hawana tatizo.

7) Waumini wa sda wawe pia na tabia nzuri kwenye maisha yao.

8) Baadhi ya mafundisho ya mama Ellen White ni maoni yake, na sio vitu alivyo viona kwenye maono (visions). Kwa hiyo baadhi ya mafundisho yake yanaweza yasiwe sahihi. Of course mama Ellen White yuko sahihi kwenye mafundisho yake mengi.

9) Ni vizuri wakristo weusi wakajua prophesies mbali mbali za kwenye Biblia, zinazo ongelea kuhusu injili kuja Afrika. Wakristo weusi, tu avoid a white/Eurocentric view of the bible, na tuwe na a true view of the Bible, which is a biblical centric view of the bible. Wakristo weusi tujaribu pia kuwa na makanisa huru yanayojitegemea (tushirikiane na watu wengine, lakini tusiwe tegemezi kwa watu wengine).

Sda wako sahihi kabisa kabisa kabisa kwamba sabato ni siku ya saba (Jumamosi), na kwamba Bwana Yesu Kristo hakubadilisha siku ya sabato. Na kwamba mpinga Kristo ndiye aliebadilisha siku ya sabato kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza ya wiki.

Moral of the story ni: Mkristo yeyote anatakiwa kusikiliza mafundisho yanayoendana na biblia, usisikilize mafundisho ambayo hayafuati mafundisho ya biblia (hata kama ni mafundisho ya dhehebu lako).

So injili ya kweli, ni kwamba Utatu Mtakatifu upo, amri 10 zipo (hazikubadilishwa), sabato ni siku ya saba (Jumamosi), tufuate mafundisho ya Bwana Yesu Kristo kama Biblia inavyosema, na Biblia ni kitabu kitakatifu cha YAHWEH (Mungu wa Biblia). Ukristo ndio dini ya ukweli, dini nyingine zote ni za uongo.

Any way tuendelee na shughuli zetu za maisha hadi siku ya mwisho ya dunia, wakati huo huo tukiendelea kumkumbuka Bwana Yesu Kristo hadi siku hiyo atakapo rudi.
 
TUNAPOWAAMBIA UKWELI KUHUSU HILO KANISA MUWE MNAELEWA.

PAPA NI MUWAKILISHI WA SHETANI DUNIANI.
Thibitisha kwanza uwepo wa shetani then ndio tujadili kuhusu hili kanisa, la sivyo tutawafananisha na makampuni ya koka na pepsi kwamba koka ni bora kuliko pepsi na pepsi ni tamu kuliko koka.
 
Luka 4: 28 Wote waliokuwa katika lile sinagogi waliposikia hayo walikasirika sana. 29. Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini. 30. Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.
Kwa Nini walimtimua kama alikuwa msabato mwenzao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…