Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.
Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.