Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wakuu leo katika press conference ya Ndugu Humphrey PolePole nimemsikia akisema kwamba ana taarifa kwamba kuna mgombea wa Urais ameshapata uraia wa nchi nyingine, ndio maana anachochea watu kufanya vurugu baada ya uchaguzi.
Je, sheria na kanuni za uchaguzi mkuu wa nchi yetu zinaruhusu mtu aliye na uraia pacha kugombea nafasi nyeti kama ya urais?
Kama taarifa hizi ni za ukweli, je Tume ya Uchaguzi inaweza kuingilia kati jambo hili? Kama taarifa hizi ni za uongo, je ndugu Humphrey Polepole kama msemaji kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi atasababisha chama chake kuwajibishwa kwa kutoa taarifa za uongo na upotoshaji?
Sheria ni msumeno na haina budi kukata pande zote.