Embu kwanza unijibu maswali haya.hiyo katiba unayoizungumzia kuwa tuilinde ni ya mwaka gani? Kama ni ya Mwaka 1977 je inasemaje kuhusu Zanzibar?
Je Zanzibar ni Nchi au siyo Nchi? Kama ni Nchi je inatambulika umoja wa Mataifa? Ina kiti katika umoja wa Mataifa? Ina Rais ambaye huenda kule kushiriki mijadala na kutoa hotuba na pengine hata kupiga kura? Nauliza maswali haya maana umesema Zanzibar ni nchi nyingine na kufananisha kwamba ni sawa na Rais wa Kenya aje awaapishe mawaziri wake hapa Tanzania.
Swali lingine je RAIS Wa Zanzibar anaingia kwenye vikao vya Baraza la mawaziri la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama Nani?
Je kuna nchi ambayo haina jeshi lake? Kama Zanzibar ni Nchi je jeshi lake ni lipi? Mkuu wa Majeshi wake ni Nani?
Je Zanzibar hakuna ikulu ndogo? Je Zanzibar siyo Sehemu ya Tanzania?je Zanzibar hawampigia kura Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Unaposema uapisho mwingi wa mawaziri unafanyika Zanzibar unamaanisha nini? Hiyo mara nyingi ni ngapi? Unaweze ukaweka hizo takwimu zako? Je katiba imetoa mgawanyo wa kwamba mahali fulani inatakiwa pasizidi idadi ya matukio kadhaa ya kuwaapisha mawaziri? Vipi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba aliyeapishiwa kule Chato kuwa waziri wa katiba na sheria? Je ile maana yake nini?
Kila siku nakwambia wewe kuwa uache chuki zako kwa Rais wetu.kinachokusumbua na kukutesa wewe ni chuki binafsi kwa Rais wetu tangia Siku ya kwanza kabisa. Roho mbaya yako haitakufikisha popote pale. Rais wetu acha afanye kazi
.najua wewe ni Miongoni kwa wale watu waliokuwa wanatamani sana Rais wetu ashindwe kuongoza Taifa hilo na kukataliwa na watanzania.sasa moyo unakuuma sana unapoona mafanikio makubwa yaliyofikiwa ndani ya muda mfupi wa uongozi wake huku uungwaji mkono kwake ukiendelea kuongezeka kila uchao. Acha roho za kichawi hizo. Una roho mbaya sana wewe na chuki kubwa sana kwa Rais wetu.