Je, katiba inasemaje kuhusu ukomo wa Raisi kuongoza kwa hali ya sasa, je raisi tuliyenae atakuwa madarakani kwa miaka mingapi?

Je, katiba inasemaje kuhusu ukomo wa Raisi kuongoza kwa hali ya sasa, je raisi tuliyenae atakuwa madarakani kwa miaka mingapi?

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Nina hakika CCM itashinda chaguzi zote zijazo, swali langu je katiba inasemaje kwa raisi aliyeshika madaraka kutokana na kifo cha raisi aliyekuwa madarakani, kwani katiba inasema atashika madaraka mfululizo kwa miaka kumi itawapo atachaguliwa.

Kwa hivyo basi je raisi tuliyenae sasa anaweza kutuongoza kwa miaka 14 iwapo atachaguliwa katika chaguzi mbili zijazo au atatuongoza kwa miaka hii minne na miaka 5 ijayo kwa hiyo kuwa raisi kwa miaka 9?

Naona kwa sasa hili hakuna anayelizungumzia sote tumebaki kushangilia tu.Je katiba inasemaje kutokana na hali tuliyonayo sasa?
 
Hiyo inapatikana katika ibara ya 40 kifungu cha 4 ktk katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Atamaliza hii miaka mitano aliyoikutia, then 2025 atagombea yeye Kama yeye kwa vipindi viwili, yaani 2025 had 2030,

halafu 2030 hadi 2035, hapo ndio anamaliza
 
Kwa katiba ipi?! Katiba iliyopo ni ukomo wa mihula miwili, na yeye mwenyewe alinukuliwa mara kadhaa akisema ataheshimu katiba dhidi ya kujiongezea muda.

Hayupo kwasasa, tujadili yaliyopo.
Hivi unajua watumishi wote wa ikulu wa enzi ya jiwe wamejenga nyumba binafsi Chato ? uliwahi kulijua hilo na uliwahi kujiuliza kisa cha wasio wa chato kujenga majengo kule ambako si kwao na hakuna fursa zozote za kiuchumi ?

Ukipata jibu rudi tena
 
Atamaliza hii miaka mitano aliyoikutia, then 2025 atagombea yeye Kama yeye kwa vipindi viwili, yaani 2025 had 2030,

halafu 2030 hadi 2035, hapo ndio anamaliza
Taarifa za uhakika ni kwamba hata 2025 hatogombea
 
Nina hakika CCM itashinda chaguzi zote zijazo, swali langu je katiba inasemaje kwa raisi aliyeshika madaraka kutokana na kifo cha raisi aliyekuwa madarakani,kwani katiba inasema atashika madaraka mfululizo kwa miaka kumi itawapo atachaguliwa,kwa hivyo basi je raisi tuliyenae sasa anaweza kutuongoza kwa miaka 14 iwapo atachaguliwa katika chaguzi mbili zijazo au atatuongoza kwa miaka hii minne na miaka 5 ijayo kwa hiyo kuwa raisi kwa miaka 9? Naona kwa sasa hili hakuna anayelizungumzia sote tumebaki kushangilia tu.Je katiba inasemaje kutokana na hali tuliyonayo sasa?
Huyu atapiga 14 years.
Hapa anakaimu tu
 
Atamaliza hii miaka mitano aliyoikutia, then 2025 atagombea yeye Kama yeye kwa vipindi viwili, yaani 2025 had 2030,

halafu 2030 hadi 2035, hapo ndio anamaliza
Hapana mkuu, mwisho wa Samia ni 2030. Hilo ni takwa la kikatiba, apende asipende.Huu wa Sasa 2021-2025 unatambulika Kama muhula wake wa kwanza, 2025-2030 Ni muhula wake wa pili na wa mwisho
 
Hapana mkuu, mwisho wa Samia ni 2030. Hilo ni takwa la kikatiba, apende asipende.Huu wa Sasa 2021-2025 unatambulika Kama muhula wake wa kwanza, 2025-2030 Ni muhula wake wa pili na wa mwisho
We Kama nani hadi useme ivyo,
 
Taarifa za uhakika ni kwamba hata 2025 hatogombea
Ingekuwa wewe ungeweza kufanya uho uzuzu,, yaani 2025 asigombee ili kupisha wasukuma au??
Yaan katiba inamruhusu kugombea nafasi kubwa ya urais kwa mara ya tatu mfululizo, eti asigombee ili kuwafurahisha nyinyi wasukuma wenye uchu wa madaraka,

Nadhani unafahamu jopo la watu wa karibu wanaomzunguka, ambao waliteswa wakati wa utawala wa mwendazake, kwaiyo watamchukulia fomu kwa lazima ili agombee kuanza rasmi awamu yake ya sita kwa vipindi viwili vya 2025 had 2035
 
Back
Top Bottom