Kimsingi awamu ya tano ilikuwa imebakiza miaka minne ili kukamilisha ngwe ya miaka 10 ambayo ni ukomo wa mihula miwili iliyotajwa na katiba. Kwa sababu yeye ni moja ya viongozi walioomba kura kuongoza katika hii miaka 10 inayofikia tamati 2025 hawezi ku-qualify kugombea tena baada ya 2025, hili lipo wazi kabisa labda kama kuna watu watataka kupindisha hapa na pale....Nina hakika CCM itashinda chaguzi zote zijazo, swali langu je katiba inasemaje kwa raisi aliyeshika madaraka kutokana na kifo cha raisi aliyekuwa madarakani,kwani katiba inasema atashika madaraka mfululizo kwa miaka kumi itawapo atachaguliwa,kwa hivyo basi je raisi tuliyenae sasa anaweza kutuongoza kwa miaka 14 iwapo atachaguliwa katika chaguzi mbili zijazo au atatuongoza kwa miaka hii minne na miaka 5 ijayo kwa hiyo kuwa raisi kwa miaka 9? Naona kwa sasa hili hakuna anayelizungumzia sote tumebaki kushangilia tu.Je katiba inasemaje kutokana na hali tuliyonayo sasa?