Je, Katiba yetu inamruhusu Rais Samia kukaa miaka 15 Ikulu?

Nashukuru sana mkuu kwa kunirekebisha na pia kunielekeza kuhusu ufasaha wa utumiaji wa neno "kukaimu" basi ngoja kwa pamoja neno gani litafaa kutumika sawa pia ulivyoelezea kuhusu upande wa katiba ingawa mimi sina uzoefu sana na katiba nadhani kuna namna ambavyo wajuzi wa haya mambo wanapotumia maneno yaliyo katika katiba huyafanya nukuu kwa namna yao kama "kivifungu" vile unaweza ukanisaidia nukuu ili nipitie na mimi hiyo katiba au umeeleza vyema kwa namna unavyojua?
 
Ok,Nashukuru sana kwa kutumia neno kukaimu inavyoonekana sijatumia neno tajika lakini wote hueleza sijatumia neno tajika lakini hawatoi neno mbadala linalofaa kutumika ngoja tuzidi kufikiria neno mbadala kwa pamoja.
Nashukuru kwa kukubali hoja kuwa ina mashiko kwa kuzingatia mifano niliyotoa.
Kweli huenda wapo hao "viazi" kati ya waTanzania lakini kwa mfano kama wewe ni mmiliki wa chombo cha moto fundi anaweza akakushangaa kuwa hujui "differential" inavyofanya kazi na kukuita "kiazi".
Na suala la ugeni humu jamvini nadhani nipo ni mwaka wa kumi+ toka nimejiunga.
Ila nashukuru kwa mawazo yasiyo na "quotation" yeyote kutoka kwenye hiyo katiba unayoijua.
 
SSH amemkaimu nani?

Na huyo aliyekaimiwa yupo wapi, na anatarajia kurudi lini kwenye kiti chake?!

Anyway, SSH hajakaimu bali ni Rais Kamili kwa mujibu wa katiba yetu!!
Sawa mkuu hapo niiweke vipi sentensi nitoe neno kukaimu niweke neno gani? Na pia katiba imekaaje maana sikuona karatasi la kupiga kura iliyoonyesha SSH akigombea nafasi ya uraisi au niweke neno mteule?
 
P
 
Umemjibu vizuri sana ,Watanzania wengi bado hatujui katiba yetu
 
𝑴𝒌𝒖𝒖,𝒏𝒊𝒎𝒆𝒌𝒖𝒆𝒍𝒆𝒘𝒂! 𝑵𝒊𝒎𝒆𝒆𝒏𝒅𝒂 𝒎𝒑𝒂𝒌𝒂 𝒉𝒊𝒚𝒐 𝒚𝒂 𝑲𝒂𝒚𝒂𝒏𝒛𝒂 𝑷𝒊𝒏𝒅𝒂! 𝑵𝒊𝒎𝒆𝒛𝒊𝒔𝒐𝒎𝒂 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒂𝒅 𝒛𝒐𝒕𝒆 𝒌𝒘𝒂 𝒖𝒕𝒖𝒍𝒊𝒗𝒖!
 
Mkuu P unatumia nguvu sana kuwaelimisha hili
Kama muhula mmoja kwa mujibu wa katiba ni miaka mitano basi ujue kuwe mama hawajaanza muhula hata mmoja
Tukae kwa kutulia mama anaweza ushangaza ulimwengu
 
Sawa mkuu hapo niiweke vipi sentensi nitoe neno kukaimu niweke neno gani? Na pia katiba imekaaje maana sikuona karatasi la kupiga kura iliyoonyesha SSH akigombea nafasi ya uraisi au niweke neno mteule?
Naona taabu kupekua katiba ili kujua ni ibara ipi hasa, isipokuwa ibara husika inasema (nukuu isiyo rasmi)--

Ikiwa rais aliye madarakani atashindwa kuendelea na nafasi yake kama rais, kutokana ama na kuumwa, kufariki, kujihudhuru, au kuondolewa madarakani (impeachment) basi makamu wa rais ataapishwa kushika kiti urais kwa kipindi kilichobaki.

Ikiwa kipindi kilichobaki ni pungufu ya mwaka mmoja (
sina uhakika sana hap), basi rais aliyeapishwa ataruhusiwa kugombea vipindi vingine viwili.

Lakini kama kipindi kilichobaki kinafika miaka 4, rais aliyeapishwa ataruhusiwa kugombea kwa awamu moja tu
!

Sasa basi, kwavile SSH aliapishwa na atakuwa rais kwa kipindi kisichopungua miaka 4, kwa mujibu wa katiba, ataruhusikwa kugombea tena awamu 1 tu, yaani 2025 na akishinda, ataweza kuwa rais hadi 2030.
 
Mkuu P unatumia nguvu sana kuwaelimisha hili
Kama muhula mmoja kwa mujibu wa katiba ni miaka mitano basi ujue kuwe mama hawajaanza muhula hata mmoja
Tukae kwa kutulia mama anaweza ushangaza ulimwengu
Kwa mujibu wa katiba, anaruhusiwa kugombea ONLY 2025 kwa sababu, alipishwa na kuwa rais, ikiwa imebaki miaka 4 na ushee!!!
 
Afadhali vilaza au watu wasio na msimamo, spineless?
 
SSH amemkaimu nani?

Na huyo aliyekaimiwa yupo wapi, na anatarajia kurudi lini kwenye kiti chake?!

Anyway, SSH hajakaimu bali ni Rais Kamili kwa mujibu wa katiba yetu!!
Sawa mkuu hapo niiweke vipi sentensi nitoe neno kukaimu niweke neno gani? Na pia katiba imekaaje maana sikuona karatasi la kupiga kura iliyoonyesha SSH akigombea nafasi ya uraisi au niweke neno mteule?
 
Sawa mkuu hapo niiweke vipi sentensi nitoe neno kukaimu niweke neno gani? Na pia katiba imekaaje maana sikuona karatasi la kupiga kura iliyoonyesha SSH akigombea nafasi ya uraisi au niweke neno mteule?
Mbona unauliza swali ambalo nimeshakujibu hapo juu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…